Mahita na Kingai si Makada wa CCM kweli?

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Kwa Mlolongo wa kesi ya Mbowe na wenzake jinsi ambavyo imeibua hisia za watanzania kua iko siasa na chuki ndani yake, nimelazimika kuuliza maswali haya kwa sababu kadha wa kadha ikiwemo kuwapiga na kuwaumiza walinzi wa Mbowe na wenzinge haijulikani walipo hivi sasa.

Najua kabisa bila shaka kua IGP mstaafu mzee Mahita ni kada kindaki Ndaki wa CCM, ana mtoto wake ni Mbunge viti maalumu CCM na aliwahi kua DC anaitwa Mboni mahita, napateje shaka kua Ispekta Mahita Omari Mahita aliyewateua walinzi wa Mbowe si kada wa CCM?

Ramadhani Kingai kuna siku aliyekua mbunge wa Arusha Godbless alisema wakiwa Arusha aliwahi kumtisha akamwambia kuwe yeye Kingai ni Kada wa CCM, kipindi hicho akiwa RCO Arusha, Kingai huyu huyu si ndiye alimwambia Mbowe hachomoki kwenye kesi yake?

Najaribu kuunganisha dots, huu ni ugaidi wa aina gani? Hakuna chuki za kisiasa kweli hapa? Huu upigaji wa vijana wa watu ambao mpaka sasa kwa mtiririko wa ushaidi wao inaonesha hawajawahi kuvunja sheria yeyote ya nchi, hawakuwahi kutekeleza tukio lolote linalohatarisha amani ya nchi. Walipigwa kiasi walikua wanaenda kumlinda Mbowe?

Unampigaje na kumuimiza mtu hajatekeleza tukio lolote hata kama unamhisi? Hivi ikibainika hawa vijana hawakuwahi kufanya tukio lolote baya,Kingai na wenzake watawalipa nini? Kwanini walitoka nje ya ubinadamu kiasi hicho?
 
Kingai na Mahita watafute pa kukimbilia maana hawako salama tena baada ya siri za matendo yao kwa hao jamaa kujulikana. Wameingia cha kike, walizoea kuwafanyia makada wa Chadema na maisha yanasonga mbele lakini sasa wamewagusa wasio gusika.
Kwani wanadhani ni Adamoo pekee aliyepata "Battle confusion"? Wako wengi mtaani na makambini.
Kisasi hakiepukiki .......
 
Nyerere alianzisha CCM ila wakati fulani mwanae Makongoro alikuwa mbunge wa NCCR Mageuzi chini ya Mrema. Haji Manara ni mtoto wa mnazi wa yanga Sunday Manara. Babu wa Haji Manara alikuwa Kiongozi wa Simba ila Bintie alikuwa mpenzi wa yanga mpaka akazaa na Sunday Manara. Hivyo hoja yako haina mashiko
 
Hao wala haina kuuliza ni makada wa CCM. Tatizo ni kuona ukada unawatoa utu. Yawezekana wameahidiwa vyeo ili watekeleze unyama wao huo. Mungu na awalipe kwa unyama wao huo.
Mswahili huwa afanyi kisicho na maslai nacho
 
Wakajifiche tuu tena ikiwezekana na familia zao zote maana waliopotea bila kujulikana ni wengi sana, ile nchi sijui ilikuwa inaelekea wapi
 
Kingai na Mahita watafute pa kukimbilia maana hawako salama tena baada ya siri za matendo yao kwa hao jamaa kujulikana. Wameingia cha kike, walizoea kuwafanyia makada wa Chadema na maisha yanasonga mbele lakini sasa wamewagusa wasio gusika.
Kwani wanadhani ni Adamoo pekee aliyepata "Battle confusion"? Wako wengi mtaani na makambini.
Kisasi hakiepukiki .......
Hawa wote walikuwa wanasaka vyeo Kwa kumfurahisha mwendazake.
 
Kwa Mlolongo wa kesi ya Mbowe na wenzake jinsi ambavyo imeibua hisia za watanzania kua iko siasa na chuki ndani yake, nimelazimika kuuliza maswali haya kwa sababu kadha wa kadha ikiwemo kuwapiga na kuwaumiza walinzi wa Mbowe na wenzinge haijulikani walipo hivi sasa.

Najua kabisa bila shaka kua IGP mstaafu mzee Mahita ni kada kindaki Ndaki wa CCM, ana mtoto wake ni Mbunge viti maalumu CCM na aliwahi kua DC anaitwa Mboni mahita, napateje shaka kua Ispekta Mahita Omari Mahita aliyewateua walinzi wa Mbowe si kada wa CCM?
Ramadhani Kingai kuna siku aliyekua mbunge wa Arusha Godbless alisema wakiwa Arusha aliwahi kumtisha akamwambia kuwe yeye Kingai ni Kada wa CCM, kipindi hicho akiwa RCO Arusha, Kingai huyu huyu si ndiye alimwambia Mbowe hachomoki kwenye kesi yake?

Najaribu kuunganisha dots, huu ni ugaidi wa aina gani? Hakuna chuki za kisiasa kweli hapa? Huu upigaji wa vijana wa watu ambao mpaka sasa kwa mtiririko wa ushaidi wao inaonesha hawajawahi kuvunja sheria yeyote ya nchi, hawakuwahi kutekeleza tukio lolote linalohatarisha amani ya nchi. Walipigwa kiasi walikua wanaenda kumlinda Mbowe?

Unampigaje na kumuimiza mtu hajatekeleza tukio lolote hata kama unamhisi? Hivi ikibainika hawa vijana hawakuwahi kufanya tukio lolote baya,Kingai na wenzake watawalipa nini? Kwanini walitoka nje ya ubinadamu kiasi hicho?
Kuna uwezekano mkubwa wanaweza wakawa ni makada, ila mkuu kwa kukukumbusha tu ni kwamba MBONI Mhita na sii Mahita, unayemzungumzia wewe ambaye ameshawahi kuwa DC nadhani kule Iringa kama sikosei, hana mahusiano yoyote na familia ya mzee Mahita whatsoever.
 
Yule Dada anaitwa Mboni Mhita alikuwa ni mbunge wa jimbo la Handeni vijijijini. Mahita ni mtu wa Morogoro wakati yule Dada ni mtu wa Handeni.
 
Kingai akiwa Rco Arusha aluwahi kumwambia Mh Lema kwamba yeye Kingai ni Ccm kindakindaki
 
Kingai na Mahita ndo wale watu wasiojulikana tuliokuwa tunataka kuwajua.. kweli chini ya jua hakuna siri
 
Kuna uwezekano mkubwa wanaweza wakawa ni makada, ila mkuu kwa kukukumbusha tu ni kwamba MBONI Mhita na sii Mahita, unayemzungumzia wewe ambaye ameshawahi kuwa DC nadhani kule Iringa kama sikosei, hana mahusiano yoyote na familia ya mzee Mahita whatsoever.
Unamwita mzee mahita...anaheshima gani ya kuitwa mzee yule jamaa...damu ya uovu inatiririka miongoni mwao. Kwake na watoto wake
 
Back
Top Bottom