Mahita na Kingai si Makada wa CCM kweli?

Wanaachaje kwa mfano? Ila nakuwa na shaka na ukaribu wa Kiangi na huyu Mtoto wa Mahita, katika namna ya kwamba ukaribu wao, je Kiangi hakuingia kwenye ajira ya polisi wakati wa IGP Mahita akiwa madarakani? na je ni vigezo gani vilitumika kumpandisha mpaka cheo alichonacho cha ACP?
 
[Unampigaje na kumuimiza mtu hajatekeleza tukio lolote hata kama unamhisi? Hivi ikibainika hawa vijana hawakuwahi kufanya tukio lolote baya,Kingai na wenzake watawalipa nini? Kwanini walitoka nje ya ubinadamu kiasi hicho?]MANENO YAMENIUMA MNO AYA MKUU NINA MAUMIVU SANA NA MATENDO MAOVU YA HAWA POLISI.
 
Yule Dada anaitwa Mboni Mhita alikuwa ni mbunge wa jimbo la Handeni vijijijini. Mahita ni mtu wa Morogoro wakati yule Dada ni mtu wa Handeni.
Kulikuwa na mhita wawili miaka ya nyuma nyuma.
Dr mhita, mkurugenzi hali ya hewa, Mhita naibu waziri wa jk.
Bila shaka huyu anaweza kuwa Binti ya hao si Mahita
 
Kulikuwa na mhita wawili miaka ya nyuma nyuma.
Dr mhita, mkurugenzi hali ya hewa, Mhita naibu waziri wa jk.
Bila shaka huyu anaweza kuwa Binti ya hao si Mahita
Kweli ni binti yao. Mzee Mhita alishatangulia mbele ya haki.
 
Katika nchi hii sio rahisi ukapewa cheo cha kuwa CDF, COS au CO jeshini au RPC, RCO, OCD, OC CID au hata OCS ktk jeshi la polisi au afisa wa ngazi yoyote ktk Tiss kama wewe sio mwanachama wa ccm.🚫

Ndio maana leo hii hivyo vyombo vya usalama vimekosa mno weledi na heshima yao kwa jamii inashuka kila uchao kwa jinsi ambavyo ushabiki wao wa kisiasa unavyo athiri vibaya utendaji wao wa kazi.

Inasikitisha kuona kwamba leo hii hivi vyombo ndivyo vimekuwa vinara wa kukikongoja chama cha ccm ambacho ni kama kimeshakufa tayari, kiendelee kung'ang'ania madarakani kinyume na matakwa ya wananchi.
 
Cha ajabu sheria zao zinawakataza kuwa wanachama wa chama chochote lakini matendo yao yanawaonyesha ni ccm damu damu.
 
Kwa nini mbowe hatakiwi kuwa na walinzi ila kina amber rutty wanatembea na mabodigadi?
 
Wekeni hata picha zao tukikutana nao mitaani hata kuwazomea tu inatosha.. ya kingai nimeona bado huyo mahita...
Na kama vp kama wapi IG au Fb wekeni a/c zao hapa tukawachane
 
Umesema "Mahita aliwateua walinzi wa Mbowe"?
 
Kwa Mlolongo wa kesi ya Mbowe na wenzake jinsi ambavyo imeibua hisia za watanzania kua iko siasa na chuki ndani yake,
Kuna kiongozi mmoja ndiyo alizikoleza sana hizi siasa za chuki mbaya, na kwa kweli alifanikiwa kuligawa taifa kwa misingi ya kisiasa kwa kiwango kikubwa - bado hadi leo hii tunahangaika ili kuliweka sawa.

Tume huru ya maridhiano inahitajia sasa ili kila mmoja atoe la moyoni - na kama kusameheana basi tufanye hivyo kama taifa ili tusonge mbele pamoja. Wa CDM asiwe adui wa CCM - na wa CCM asijione kwamba yeye ndiyo mwenye hati milki ya Tanzania kwamba anaweza kuhitimisha ndoto ama maisha ya wenzake wa vyama vingine wakati wowote anaotaka yeye.

Police pia wapige magoti na wawaombe radhi wale wate waliowafanyika unyanyasaji, mateso na wengine kupotea - hii Tanzania ni yetu sote... ili kwa pamoja basi tuitangazie Dunia kwamba sisi ni wamoja na UGAIDI nchini kwetu haupo, kilichokuwepo danadana za kisiasa na kukomoana.
 
Cha ajabu sheria zao zinawakataza kuwa wanachama wa chama chochote lakini matendo yao yanawaonyesha ni ccm damu damu.
Kuna watu katika nchi hii wanaojiona kuwa juu ya sheria na hivyo wanaona kwamba wao hawapaswi kufuata sheria, wako watu wa ccm, polisi na usalama wa taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…