Mahitaji msaada wenu wana JF nimekwama, tafadhari nisaidieni.

NGOSWE2

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
1,323
Reaction score
1,608
Habari za muda huu wana JF.

Kama kichwa kinavyojieleza, nahitaji msaada wenu wa kitaalamu. Nina boma langu ambalo nahitaji kulipaua baada ya kukaa muda mrefu bila paa. Nimejaribu kuhesabu na mafundi kadhaa ili wafike pale site na kunipa za bati mahitaji.

Hata hivyo, kila mara wanaponitumia hesabu zao, naona kama idadi ya bati ni nyingi sana. Mtaalamu wangu wa muda mrefu, ambaye alikuwa akinisaidia kila mara, kwa sasa amekwama Zambia na mawasiliano hayapatikani. Kwa hiyo, nimewaomba mafundi wanitumie mchoro ambao naambatanisha hapa kwa uchambuzi zaidi.

Bati ninazotaka kutumia upana wa 1015mm.

Asante sana kwa msaada wenu.

66e4090d-3e03-4685-906f-6f7c2b1f3616.jpeg
 
Sawa.Ramani ya Jengo lako ikoje Mkuu?Inajengwa wapi?(Mapaa ya Geita na Data au Dodoma yako Tofauti.Geita yanazaa hewani,Hadi wajenzi wanatumia bati na Mbao mara 1.5 ya Dar au Dodoma.
 
LIPO dar es salaam Mkuu.
Na ramani ya jengo aliondokanayo aliyekuwa anasimamia ujenzi wa boma.

Ila kuna mchoro walionirushia wa kulizunguka boma ukiwa na vipimo nimeambatanisha na maelezo yangu ya mwanzo.
Sasa sijui kwa vipimo hivyo itasaidia?
66e4090d-3e03-4685-906f-6f7c2b1f3616.jpeg
 
bati za urefu wa mita 6 ziko 12
bati za urefu wa m 2.2 ziko 12
gable weka bati 2 tu za urefu wa mita 6 zitakatwa
upana ni huo huo wako pambana upate IT sheet
yaani hapo jumla ni bati za urefu wa mita 6 ni 15 tu ikizidi ni 16
 
bati urefu wa mita 6 ziko 12
bati urefu wa m 2.2 ziko 12
gable weka bati 2 tu za urefu wa mita 6 zitakatwa
upana ni huo huo wako pambana upate IT sheet
yaani jumla ni bati za urefu wa mita 6 ni 15 tu ikizidi ni 16
Tafadhari fafanua kidogo mkuu.
.Sijakuelewa kabisa. Nahitaji ufafanuzi zaidi kama hautajali mkuu.
 
Hapo zitakua bati 110, kwa mlalo wa kawaida sio kama yale ya kisukuma marefu
 
Habari za muda huu wana JF.

Kama kichwa kinavyojieleza, nahitaji msaada wenu wa kitaalamu. Nina boma langu ambalo nahitaji kulipaua baada ya kukaa muda mrefu bila paa. Nimejaribu kuhesabu na mafundi kadhaa ili wafike pale site na kunipa za bati mahitaji.

Hata hivyo, kila mara wanaponitumia hesabu zao, naona kama idadi ya bati ni nyingi sana. Mtaalamu wangu wa muda mrefu, ambaye alikuwa akinisaidia kila mara, kwa sasa amekwama Zambia na mawasiliano hayapatikani. Kwa hiyo, nimewaomba mafundi wanitumie mchoro ambao naambatanisha hapa kwa uchambuzi zaidi.

Bati ninazotaka kutumia upana wa 1015mm.

Asante sana kwa msaada wenu.

View attachment 3134740
Idadi ya bati inategemea na factors nyingi kama vile angle ya paa, urefu wa bati utakazotumia (za kupima au za futi 10) na upana wa bati ambao umeshauandika hapo juu.

Kutokana na vipimo vya jengo lako jinsi vilivyo, angle nzuri ya kutumia ni kati ya 30 degrees mpaka 35 degrees, ukitumia angle ya 45 paa lako litaenda juu sana na halitakuwa na muonekano mzuri

Hapo kwa mahesabu ya haraka haraka, kama utatumia angle ya 30 basi utatumia bati 72 za futi 10 za huo upana uliouandika

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Nashukuru sana Mkuu.
 
Back
Top Bottom