Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Zama zile za kati, mahitaji ya mwanadamu ya msingi yalikuwa matatu tu. Lakini sasa mambo yamebadilika kabisa.
Leo tunahitaji internet kama hutaji muhimu la mawasiliano, bila internet mawasiliano yetu yako kwenye mashaka makubwa sana.
Maisha ya leo bila kuwa na biashara au KAZI, wewe ni mfu na utadharaulika na kila MTU. KAZI sio lazima uwe umeajiriwa, chochote unachokifanya na kukuingizia kipato ni KAZI.
Leo bila kusafiri hali ni tete. Unawezaje kutoka Gongo la Mboto hadi kazini kwako Posta?
Kwenye dunia yetu ya sasa Usalama ni Jambo la msingi sana. Tunawezaje kufanya shughuli zetu kwenye mazingira ambayo Panya Road wanapita mchana kweupe wakipora Mali, kupiga watu, kubaka na kujeruhi?
Haki pia ni hitaji muhimu la mwanadamu licha ya kwamba halipatikani kirahisi.
Ila tukae tukijua kwamba amani ni tunda la haki. Bila haki hakuna amani.