Mahitaji na Anasa

Mahitaji na Anasa

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
459
Reaction score
653
NEEDS

Haya ni mahitaji muhimu ambayo mwanadamu anayahitaji ili aweze kuishi.

Mfano: Tunahitaji maji ili tuweze kuishi, tunahitaji chakula ili tuweze kuishi.

WANTS

Vitu ambavyo mwanadamu anatamani kuvimiliki sasahivi au baadae hivi ndio tunaviweka kwenye kundi la wants. Unaweza ukaishi vizuri tu bila kuwa navyo, japo utaridhika ukiweza kuwa navyo. Ni muhimu sana kujua katika maisha yako kipi unahitaji kuwa nacho (NEEDS) na kipi unataka kuwa nacho (WANTS). Kujua tofauti kati ya NEEDS na WANTS kutakusaidia:

1. Kujua ni aina gani ya biashara itafanikiwa zaidi ukiifungua

Mfano: Kwenye sekta ya usafiri

Watu wanahitaji huduma ya usafiri ila wanatamani kumiliki magari yao binafsi.

2. Itakusaidia kujua kitu cha kukipa kipaumbele.

Mfano: Unahitaji saa ila unatamani kumiliki smart watch.

3. Itakusaidia kufikia malengo nk

Kwahiyo ni muhimu mtu kujua ni kipi unakihitaji katika maisha yako na kipi unakitamani ila unaweza kuishi bila kuwa nacho.

Kumbuka mda mwengine kuna NEEDS na WANTS zinatofautiana baina ya watu kutokana na

1.Mazingira Kuna mazingira ni lazima mtu kumiliki usafiri binafsi na kuna mazingira sio lazima mtu kumiliki usafiri binafsi.

2.Kipato

Mtu mwenye kipato kikubwa inamlazimu kuwa na financial advisor

Karibuni kutoa mifano ya needs na wants katika maisha yetu ya kila siku.

#wants #needs
 
Back
Top Bottom