JamiiTalks Mahojiano JF: Historia ya Elimu ya Mhe. Khamis Kagasheki - #1

JamiiTalks Mahojiano JF: Historia ya Elimu ya Mhe. Khamis Kagasheki - #1

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
SWALI: Tueleze historia ya Elimu yako





(Katika maandishi kutokana na video hii)



Kabla sijajibu, mimi kwanza nataka, kwa kweli nitoe shukrani za dhati kwamba, JamiiForums wameweza kunialika, kunipa nafasi ya kuweza kuzungumza, sio tu na watanzania kipitia katika JamiiForums lakini ni kama unazungumza na ulimwengu kwa sababu ni forum moja ambayo wanaingia watu wengi, wanaweka michango mingi ya kisiasa, kijamii na kadhalika, kwa hio, kwa hilo nalitolea shukrani.

Mimi, mimi ni kama jina langu lilivyo, ni Khamis, baba yangu alikuwa mzee Juma Swedi Kagasheki. Nimezaliwa Bukoba, nimezaliwa pale hospitali ya serikali pale Bukoba mwaka 1951 na nimekuwa pale Bukoba, nimeanza masomo yangu nikiwa mdogo na nilisoma katika shule ilikuwa inaitwa shule ya Mabatini, maana ilikuwa mabatini kwa sababu ilikuwa ni shule haina kuta, haina nini isipokuwa yote kuanzia chini ni mabati tu mpaka juu ni mabati, kwa hiyo ilikuwa nyakati zile.

Lakini kuna shule zilikuwa zinajengwa pale, wakati ule kulikuwa wa-missionery ndo wanajenga lakini pia kuna shule moja ya Muslim school ilikuwa inajengwa pale, kwa hio niliweza kusoma mimi Mabatini halafu nikasoma Primary school darasa la kwanza mpaka darasa la pili actually katika hio shule lakini nikaja nikahama nikaenda katika shule ilikuwa inaitwa wakati ule Indian public school, ilikuwa ni shule ya wahindi ya pale Bukoba mjini.

Kwa hio nikasoma pale, baadae ikaja kutoka from being an Indian public school ikawa inaitwa Grewo primary School, na Grewo alikuwa muhindi mmoja ambae alikuwa based in India, ambae alikuwa actually ndio mwenye shule. Kwa hio nikasoma pale masomo yangu ya Primary, nikafaulu vizuri, nikaenda shule ya serikali, government school ambayo inaitwa Nyakato secondary school ipo pale Bukoba lakini kwa jiografia ya sasa hivi iko Bukoba vijijini, kwa sasa hivi. Kwa hio nikasoma pale lakini nilisoma form one na form two, form three na form four nikaenda Kahoro secondary school ambayo iko katika jimbo la Bukoba mjini.

Kwa hio ni shule yangu, hata nnapokwenda nafika pale kutizama hali halisi ilivyo pale shuleni, kutizama mabadiliko ambayo yamekuwepo na kadhalika, kwa hio nilisoma mpaka pale nikaweza kufaulu katika vipindi vya, actually ambavyo nilishinda, ilikuwa kipindi cha History, kilikuwa kipindi cha Kiswahili, kilikuwa kipindi cha Kiingereza na ilikuwa kidogo hesabu.

Nikatoka pale, kwa kuwa tulikuwa na jamaa families zetu alikuwa Uganda Masaka. Kwa hio nikaenda high school Masaka, na pale nikasoma, ile ilikuwa shule ya kikatoliki, ST. Benard's college.

Na kwa kweli wana misingi mizuri, mimi niseme, kwa hio nilipomaliza pale Uganda Masaka ambapo ilikuwa ni shule ya kikatoliki na mpaka leo lakini naona wameweza kupanua zaidi, imekuwa actually chuo kikuu.

Nikaenda New York, nivyokwenda New York, nilikwenda katika chuo kinaitwa Fordham university. Hiki ni chuo cha wakatoliki lakini ma-jesuits na niseme kwamba inasaidia, kwa sababu ilinipa background moja nzuri sana kwa sababu ya nidhamu ambayo hawa majesuits walikuwa nayo kwa hio nikaweza kusoma pale, nikaweza kupata degree yangu ya bachelors katika economics lakini pia na political science na nilivyomaliza tu pale Fordham university nikawa nime-apply kujoint foreign services lakini kwa kuwa wakati niko New York na nilipokuwa nikisoma nilikuwa bado nafanya kazi katika ubalozi wa Tanzania lakini kwa upande wa research, nilikuwa nawafanyia research katika maeneo mbali mbali.

Katika maswala ambayo walikuwa nayo katika security council, katika maswala ambayo walikuwa nayo katika upande wa general assembly ya umoja wa mataifa, kwa hio baada ya kufanya pale nikaomba kazi na nikapewa kazi, nikaingia foreign na nikafanya kazi na ninaweza kusema hio ndio ilikuwa mwanzo wangu actually wa kuingia katika foreign service lakini upande wa demokrasia zaidi sio upande wa siasa zaidi.

Lakini nishukuru wakati ule Mwalimu alikua bado yuko madarakani kwa hio tuliweza kuona misimamo ya Tanzania, katika maeneo mbalimbali, katika maswala mbalimbali ya kidunia na wakati ule ilikuwa maswala makubwa, maswala ya liberation ya Africa na kadhalika. Kwa hio niweze kusema hio iliweza kunijengea tu nafasi nzuri na opportunities kuzipata.

Ajabu, mzee marehemu baba yangu, alikuwa ni muislamu of course ndo mana na mimi nikawa muislamu, lakini lilipokuja katika swala la elimu, ilikuwa ni kwamba tafuta elimu na ukiweza kupata, pata mahala ambapo ni bora katika kupata elimu. Na sijui sasa, lakini hayo ni mambo mengine, siwezi nikaweka judgement yangu lakini kwa kweli shule za kidini wakati ule , niseme kwamba kulikuwa na nidhamu kubwa sana lakini pia nilikuwa sikwenda kusoma dini, kusema kwamba nilikuwa nakwenda kusomea dini fulani, isipokuwa ni masomo ambayo yalikuwa yanatoka pale na masomo ambayo yamekuja kusaidia, ni masomo ya dunia, ni masomo ya mwenendo mzima lakini pia kulikuwa na nidhamu, shule zote hizo nimekwenda.

Kwa mfano shule ya high school niliyokwenda kulikuwa na utaratibu mzima wa kuwa na ibada, misa ya kila asubuhi, hiyo ilikuwa inakuwepo na ile shule, university ya ma-jesuit, of course wao walikuwa ndio wengi ambao ndio walikuwa wanaendesha masomo lakini kuliwa hakuna kusema unamlazimisha mtu kwamba lazime awe mkatoliki au awe mkristo, kubwa lilikuwa kutoa elimu na mimi kitu ambacho nilikuwa naki-pursue ni elimu, na niseme kwamba nashukuru kwa sababu misingi mikubwa na ile nidhamu kubwa ambayo niliipata kutoka katika hizi institution mbili zilikuwa ni za kikatoliki, mimi nasema ni kitu ambacho ni siku zote, ntajivunia sana kwa sababu, kwa kweli nidhamu, nidhamu ya masomo, nidhamu ya ufatiliaji, nidhamu ya utendaji na unakuta kwamba kila kitu kilikwenda kwa utaratibu ambao ulikuwa ni mzuri tu.


*Zingatia hii ni swali la kwanza katika orodha ya maswali yaliyojibiwa. Kwa taarifa zaidi tembelea
- https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...iforums-na-khamis-kagasheki.html#post12846285
 
Last edited by a moderator:
Kazi nzuri sana JamiiForums,video imetulia sana na mheshimiwa mbunge wangu katendea haki Mahojiano.

Sina maoni mengi kuhusu hili kwasababu bado kuna mahojiano makubwa zaidi yanakuja ila nimependa alivyosema katika kutafuta elimu pamoja na familia yake kuwa ya Kiislam ilibidi atafute sehemu ambayo angepata elimu yenye misingi bora ndio maana kwa wakati ule alisoma shule za Kikatoliki ambazo ndio zina elimu bora na misingi yenye kujenga.

Misingi hiyo ndio imemfanya mpaka sasa kuwa bora katika siasa.

Nadhani mahojiano haya yatatoa mwanga kwa wanasiasa wengine wengi ambayo watapenda mahojiano live na JamiiForums.

Hongereni sana JF. Tunasubiri video za mahojiano mengine kwa hamu.
 
Mkuu,

Mtu wa kwanza kuhojiwa alikuwa ni Zitto Kabwe (tembelea - https://www.jamiiforums.com/great-t...he-zitto-zuberi-kabwe-katika-jamiiforums.html).

Kabla na baada ya Zitto, kila aliyetafutwa kwa ajili ya mahojiano changamoto ilikuwa uwezo wa kujibu kupitia maandishi. Hivyo project iliishia hapo na kuamua kutafuta mbadala ambao ungekuwa ni rahisi kufikisha maswali/maoni ya wana'JamiiForums na yakasikilizwa kwa mhojiwa.

wanaukabila sana hawa watu wa ziwa magharibi naona faunda wa forum kaanzia kwao,utasikia anafuata mama tiba,mchungaji mwanamke,balozi mashilingi,mmea dk amani, mjasiriamali nazir wa ticis makontena nk (jokes)
 
Daaah, Naona Mh Kagasheki kapata Elimu kwa mtindo wa Jakaya Kikwete.. Safi sana

Elimu Kwanza Dini baadaye..!!!!

BACK TANGANYIKA
 
Mkuu,

Mtu wa kwanza kuhojiwa alikuwa ni Zitto Kabwe (tembelea - https://www.jamiiforums.com/great-t...he-zitto-zuberi-kabwe-katika-jamiiforums.html).

Kabla na baada ya Zitto, kila aliyetafutwa kwa ajili ya mahojiano changamoto ilikuwa uwezo wa kujibu kupitia maandishi. Hivyo project iliishia hapo na kuamua kutafuta mbadala ambao ungekuwa ni rahisi kufikisha maswali/maoni ya wana'JamiiForums na yakasikilizwa kwa mhojiwa.
mkuu nilikuwa na joke tu kuchangamsha mada
 
Mh.Kagasheki kipi kilikufanya uame Nyakato na kwenda Kahororo na mtihani wa kidato cha nne uliufanyia wapi? Je unaweza dhibitisha kwa watanzania kuwa vyeti vyako ni halali na nivya hapa Tanzania?
 
Mimi nasubiri kwa hamu kipengele E, operesheni tokomeza maana maneno yamekua mengi hasa kipindi hiki cha lala salama..
 
Mimi nasubiri kwa hamu kipengele E, operesheni tokomeza maana maneno yamekua mengi hasa kipindi hiki cha lala salama..

Lala Salama!! Kwamba kuna watu walihusika moja kwa moja kwenye mauaji yaliyotokea kwenye hiyo operesheni lakini bado hawakutaka kuwajibika moja kwa moja na sasa hivi wanatia either kwenye urais na ubunge?

Hii operesheni ilichafua taswira ya viongozi wengi lakini ajabu waliowajibika walikuwa wachache mh. Kagasheki akiwa mmoja wapo.

Tumsubiri tusikie atanena nini.
 
Primary - shule ya wahindi

Secondary - Serikari(Nyakato), Lutheran(Kahororo), Cathoric(St.Benard)

University - Catholic (Fordham)

Mzee Kagasheki alikuwa anaona mbali.

Nimewahi kusikia humu kuwa wakristo waliwakandamiza waislam - sijui kwa vipi.
 
Back
Top Bottom