Mahojiano mubashara kati ya mchezaji wa zamani Mtemi Ramadhani na TBC

Mahojiano mubashara kati ya mchezaji wa zamani Mtemi Ramadhani na TBC

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Nilishuhudia mahojiano haya kwa kweli nilifurahia sana jinsi wachezaji wa zamani walivyokuwa wamejitolea kwa hali na mali kwa ajili ya nchi yao. Alichoshauri ni kuwa siku hizi wachezaji wetu hawafanyi mazoezi kikamilifu na mazoezi yao ni mepesi sana.

Alitoa mfano wa wachezaji wa Uganda wanavyofanya mazoezi hata mara tatu kwa siku kinyume na wachezaji wetu wa kitaifa. Alizidi kutoa mfano kuwa huko nyuma timu kama za Botwana, Syecheles na nyingine nyingi hazikuwa tishio kwa timu yetu, leo hii timu hizo ndizo zimekuwa tishio kwetu. Amesifia sana kipindi cha uongozi wa Tenga kuwa walijali kazi na siyo fedha kinyume na uongozi uliofuata. Walipotoka kwenye uongozi waliacha fedha za kutosha pale TFF.

Mtemi Ramadhani ni Simba damu na ni msomi mwenye digirii na uwezo anao. WanaSimba mpeni wadhifa kwenye Klabu ili klabu iweze kusonga mbele.
 
Walifanya kazi kubwa gani akati nchi yetu haijawai twaa kikombe chochote??
 
Back
Top Bottom