Jamaa wa Kongoi.com wamechapisha mahojiano na mwanamziki Ebrahim Makunja aka Ras Makunja, mwasisi wa bendi ya The Ngoma Africa Band, kwenye mtandao wa Kongoi.com.
Katika mahojiano haya, Ras Makunja anagusia masuala ya mziki wa dansi na pia ule wa kizazi kipya. Zaidi, msanii huyu anachambua matatizo yanayofanya mziki wa Tanzania kutokuweza kufunika soko la kimataifa hadi hivi sasa.