Mahojiano na waliopigiwa kura kuhusu mauaji ya albino

Mahojiano na waliopigiwa kura kuhusu mauaji ya albino

Kyachakiche

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2009
Posts
986
Reaction score
208
MDADISI: Ehee, na wewe tueleze unahusikaje na ulitumwa na nani!
MSHUKIWA:Sihusiki sana mh, nilikuwa natekeleza matakwa ya mkuu wangu.
MDADISI: Ni nani huyo mkubwa wako? Mtaje ili wewe uwe huru.
MSHUKIWA: Kamanda wangu mh.( huku akimtaja)
MDADISI: Heh! haiwezekani.( Kimoyoyomoyo, nitahoji vipi mkubwa wangu!!!)
Hata hivyo anaamua kumhoji baada ya kupata go ahead!
MDADISI: Mh Kamanda, wewe unahusikaje na hili?
KAMANDA: Niliagizawa na mkuu wangu nimsaidie ili aweze kupanda cheo.
MDADISI: Kumsaidia kwa namna gani?
KAMANDA: Ili apande cheo!
MDADISI: Unaweza kumtaja huyo mkuu wako?
KAMANDA: Ki itifaki sitoweza kumtaja!
MDADISI: Una maanisha ni ( anamtaja)
KAMANDA: Haswaa, tena yule anakuja! ( huku akimnyoshea kidole)
MDADISI: Ok, ngoja ni mwite, Karibu mkubwa!
MKUBWA: Aksante.
MDADISI: Mbona uko huku?
MKUBWA: Nafuatilia mauaji ya Albino.
MDADISI: Tuambie mkuu, wewe unahusikaje kwenye hili?
MKUBWA: Mimi siyo msemaji wa Wizara, labda waziri mwenye dhamana, tena atakuwa hapa muda si mrefu.( mara waziri anaingia).
MDADISI: Mh. Waziri, karibu sana. Nini maoni yako kufuatia upigaji wa kura za kuwafichua wanaojihusisha na mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi?
WAZIRI: Eeh; nafikiri ni mapema mno kulizungmzia hili. Ninachoweza kusema ni kuwa serikali ina mkono mrefu, itawakamata tu!
MDADISI: Mbona uko huku, kunani?
WAZIRI: Natafuta njia ya kushinda katika uchaguzi ujao.
MDADISI: Unatafuta kutoka kwa nani!
WAZIRI: Wewe vipi! Si kwa hoo ndgu zetu waganga wa kienyeji!
MDADISI: Watakusaidiaje?
WAZIRI: Ndiyo maana tumeitisha kura pamoja na mambo mengine kutaka kujua pia ni akina nani wanataka kuchukua majimbo yetu na ni kina nani wanawafadhili!
MDADISI: Ooooh! kumbeeee!
 
MDADISI: Ehee, na wewe tueleze unahusikaje na ulitumwa na nani!
MSHUKIWA:Sihusiki sana mh, nilikuwa natekeleza matakwa ya mkuu wangu.
MDADISI: Ni nani huyo mkubwa wako? Mtaje ili wewe uwe huru.
MSHUKIWA: Kamanda wangu mh.( huku akimtaja)
MDADISI: Heh! haiwezekani.( Kimoyoyomoyo, nitahoji vipi mkubwa wangu!!!)
Hata hivyo anaamua kumhoji baada ya kupata go ahead!
MDADISI: Mh Kamanda, wewe unahusikaje na hili?
! kumbeeee!

Mkuu,
Baadhi ya hawa ni albino.
Hawana tofauti na watu wengine.
Imani potofu ndo tatizo.

collage3.jpg
 
Mkuu,
Baadhi ya hawa ni albino.
Hawana tofauti na watu wengine.
Imani potofu ndo tatizo.

collage3.jpg
Ni kweli mkuu hawana tofauti na binadamu wengine ila ni unyama na uroho wa mali. Hapo nilitaka kuchokonoa chanzo hasa cha haya mauaji ya kikatili ni nini na ni akina nani wanahusika au kufadhili.
 
Back
Top Bottom