Naomba kujua ni kwanini hasa umekuwa na uamuzi wa kuachana kabisa na Ubunge na kutogombea tena; na kama hayo ni maamuzi yako na hujaeshinikizwa na kitu ama mtu yeyote. Je utaendeshaje maisha yako ya kisiasa nje ya Bunge na nje ya taasisi ya Urais?
Wakati nagombea Ubunge mwaka 2005 niliwaambia wapigakura wangu kuwa nitakuwa Mbunge wao kwa vipindi viwili tu. Niliwaambia nina ndoto za kuja kuwa Rais wa nchi yetu baadaye. Hivyo haya ni makubaliano yangu na wapigakura wangu. Nia yangu ni kupisha wengine nao wakimbize kijiti cha maendeleo ya Jimbo letu na Mkoa wetu. Nimesema mara kwa mara kwamba ukiachana na siasa kazi ninayoipenda zaidi ni ualimu. Nitakapomaliza Ubunge na Urais nitakwenda kufundisha. Ninajiandaa vilivyo kwa suala hilo. Nitapenda kufanya tafiti, kusoma, kuandika na kufundisha. Hivi sasa tunaandaa mpango wa kuanzisha Chuo Kikuu cha Ziwa Tanganyika (Lake Tnaganyika University) mkoani Kigoma. Nitafurahi kama nitakuwa mmoja wa wahadhiri wa mwanzo wa chuo hiki kufundisha Watanzania Uchumi wa Rasilimali.
Sina wasiwasi pia wa kuendesha maisha maana mimi ni mwanachama wa NSSF, ninajichangia kwa hiari toka nilipoacha kazi katika Shirika la FES mwaka 2004. Ikifika mwaka 2015 nitakuwa nimetimiza &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];points' za kulipwa pensheni. Nashukuru kwamba nilikwepa ushawishi wa kujitoa kwenye mafao. Naamini nitaendesha maisha yangu kwa kazi za kufundisha, kuuza vitabu, consultancies na pensheni niliyojiwekea akiba.
CHADEMA kina utaratibu gani wa kutangaza nafasi za wagombea katika ngazi mbali mbali hasa ya urais?
Chama chetu hakina utaratibu wowote hivi sasa wa kutangaza nia za watu kutaka kugombea nafasi yeyote. Juzi tumekutana Morogoro na kukubaliana kuwa tutatengeneza utaratibu wa watu kutangaza nia zao wanapootaka kugombea nafasi yeyote ya uongozi. Nadhani huu ni uamuzi mzuri wa chama maana kuna watu wana wasiwasi usio na msingi kabisa kuwa kuwa na wagombea wengi kwenye chama ni kuvuruga chama. Lakini watu hao hao wanashangilia kweli wakiona demokrasia inavyotekelezwa kwenye nchi nyingine kama Marekani. Watanzania wanapenda kuona demokrasia inatekelezwa lakini wanaogopa kuitekeleza wao. Uamuzi wa Morogoro kuhusu mwongozo kwa wagombea utatusaidia sana kuondoa mashaka kama haya.
Katika moja ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];school of thought', inasemekana umetangaza haraka nia ya kugombea Urais kwa misingi ya kuwa Dr. Slaa hana tena mpango huo na kwamba nje ya Slaa huoni zaidi yako ambaye anaweza wakilisha vema. Unalizungumziaje hili mkuu?
Slaa hakuwahi kutangaza nia ya kugombea Urais wakati wowote ule wa maisha yake. Mwaka 2010 Tulimwomba kama chama. Chama kinaweza kumwomba tena na tukifikia mwafaka ndio atakuwa huyo na sote lazima tumwunge mkono. Mimi nimetangaza kwa kuwa ninautaka Urais na hivyo nakiomba chama kiniteue. Pia chama kina viongozi wengine wazuri tu. Tundu Lissu na Mnyika wamesema hawautaki Urais. Ndugu Mbowe yeye hajasema kama anautaka au la. Kumbuka hata mwaka 2005 Mbowe tulimlazimisha, yeye alitaka aendelee kuwa Mbunge wa Hai. Sisi tukamwambia kuwa lazima abebe chama. Nakumbuka mimi binafsi niligombana naye maana aliposema yeye atagombea Hai, nikamwuliza kwa chama gani? Maana kama hutaki kukibeba chama kwenye Urais tutachukua kadi yetu. Ndio! Nilimwambia hivyo kwenye secretariat ya chama. Akakasirika kweli, lakini baadaye alinielewa na mafanikio tuliyoyapata ni makubwa sana baada yeye kugombea. Kwa hiyo hiyo School of Thought ni hisia tu za watu. CHADEMA ina watu wengi sana wenye uwezo wa kuwa maRais. Kitila Mkumbo mnamwonaje? Au mpaka watu wawe Bungeni. Huyu ni hazina ya chama na nchi. Chama kinaweza kusema, Zitto hapana, mwunge mkono Kitila. Nitafanya hivyo. The Party deploys for or against your wishes and every member must oblige a JUST deployment. I will.
Ikitokea kuwa hujateuliwa na chama chako (CHADEMA) kugombea Urais 2015 kwa tiketi ya chama hicho, una nia ya kutafuta chama kingine kitakachokuruhusu kugombea nafasi hii ya Urais?
Nisipoteuliwa na chama kugombea Urais nitamfanyia kampeni mgombea atakayeteuliwa na chama. Siamini katika kuhama vyama ili kutimiza malengo ya kisiasa na ndio maana mimi sijawahi kuwa chama kingine chochote zaidi ya CHADEMA maisha yangu yote. Mwanasiasa anayehama vyama ili kupata uteuzi anafuata vyeo na sio muumini wa sera ya chama husika.Vile vile Urais kwangu mimi sio an end in itself, it is a means ya kuleta mabadiliko ya hali ya maisha katika nchi yetu. Kama ilivyokuwa kwa Ubunge, ambapo nimehudumia wananchi na kuleta mabadiliko makubwa sana ndani ya muda mfupi na sasa nataka kuachia wengine, Urais nao ni hivyo hivyo, kutaka kufanya transformation ya nchi yetu, radical transformation katika uchumi, siasa na jamii. Nataka kuionyesha dunia kuwa tunaweza kuondokana na umasikini in our life time. Sasa kama chama kina mtu mwingine mwenye mwona kama huu, mimi nitamuunga mkono na kumsaidia kuifanya kazi hii.
Kabla ya uchaguzi wa 2010 ulishawahi tangaza kutogombea tena ubunge 2010; ni kitu gani kilifanya ubadilishe huo msimamo?
Mwaka 2009 niliamua kuwa ni bora niache ubunge ili nifanye shahada yangu ya uzamivu na kasha nifanye machapisho. Unajua niliingia Ubunge nikiwa na umri wa miaka 29 tu. Kazi niliyofanya kwenye Bunge la Tisa ilikuwa inanizidi kimo kwa kweli. Nilikuta Bunge limelala sana. Lilikuwa Bunge la status quo. Halikuwa Bunge vibrant kabisa. Siku ya kwanza tu nimeingia Bungeni sikulipenda. Hamu iliniisha. Lakini nikasema ngoja nibadili modus operandi ya Bunge. Nikaanza kutoa hoja kali kali Bungeni na hatimaye nikasimamishwa Bunge. Nafurahi kwamba Wabunge wengine walifuata kasi yangu. Mnakumbuka kuna wabunge walikuwa wanasema &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];hatuwezi kumwachia Zitto Kabwe peke yake kazi ya kuibua ufisadi' nk. Sasa baada ya kuona nimefanikiwa nikasema basi term moja inatosha. Badaye nikapata ushawishi kuwa hapana, nenda Geita au Kahama au Kinondoni. Nikafanya utafiti wangu nikaona mwenyewe kuwa niende Geita. Viongozi wa chama kutoka Geita wakaenda kuwaona wenzao Kigoma wakakataliwa. Wazee wakanikumbusha kuwa, makubaliano yetu yalikuwa mihula 2. Ikabidi nitimize ahadi hiyo ya mihula 2. Haikuwa matakwa yangu. Mpaka sasa nime abandon PHD yangu maana sina muda na siasa zangu mimi huwa naacha kila kitu kinacho weza kuni divert, hivyo nakosa muda wa kusoma na kuandika.
Tokana na kauli yako hivi karibuni kuhusu kwamba Uongozi wa nchi hautakiwi kuwa mikononi mwa watanzania waliozaliwa kabla ya uhuru; Je kulikuwa na ulazima kutamka haya? Huoni kwamba iwapo utafanikiwa kuwa rais wa nchi yetu, urais wako unaweza kuja kutuletea generational conflicts (misuguano/migongano/mifarakano ya vizazi)?
Mimi ninaamini kabisa kuwa Rais ajaye wa Tanzania ni lazima atokane na kizazi cha baada ya uhuru. Nchi inahitaji a fresh start. Misuguano ndio huleta maendeleo. Hebu tazama nchi hii, Asilimia 70 ya Watanzania wapo chini ya umri wa miaka 29! Asilimia 65 ya wapiga kura wapo kati ya umri wa miaka 18 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 40. Hili ni Taifa la vijana. Nusu ya Watanzania wapo chini ya umri wa miaka 17! Unaweza kusema hili ni Taifa la watoto. Hawa wazee wetu walipokuwa wanachukua nchi walikuwa vijana. Mwalimu alikuwa Waziri Mkuu akiwa na miaka 39, Mzee Kawawa alikuwa Waziri Mkuu akiwa na miaka 37. Waziri Mkuu wakati huo ndio alikuwa Mkuu wa Serikali maana Mkuu wa nchi alikuwa Malkia wa Uingereza. Angalia mafanikio ya Mwalimu Nyerere na Kawawa kati ya mwaka 1961 na 1971 halafu pima na baada ya hapo mpaka wanastaafu. Tusibwabwaje tu bila evidence. Ndio maana leo Marekani Rais wao ni kijana. Uingereza Waziri Mkuu wao kijana ingawa mataifa haya yana wazee wengi zaidi kuliko sisi. Ninaweza kutamba kwamba mimi ni mmoja wa wanasiasa ambao ninaheshimu sana wazee. Uliza wazee waliopo na waliokuwapo Bungeni ni mwanasiasa gani kijana anatumia muda mwingi nao. Mwulize mzee Sarungi, bahati mbaya mzee Makwetta amefariki. Mwulize dokta Salim, mwulize Mzee Warioba. Wao pia wananiambia, Zitto huu ni wakati wenu. Sisi tulifanya yetu.
Kuna watu lazima watafsiri chochote atakachosema Zitto. Hata hili ninaloandika hapa mtasikia, watasema tu. Kuna watu wanaumwa ugonjwa wa zittophobiasis ni lazima waseme. Mtasikia tu wanasema hivi sasa. Sasa wanaotaka kutafsiri kauli yangu wana mambo yao, lakini ninaamini kabisa kuwa changamoto za sasa za Taifa zinahitaji Rais wa kizazi cha baada ya Uhuru. Wazee watatupa ushauri. This country has to move very fast. We need an ambitous young man, visionery and focused to transform this country. Tunaweza kuwa na Spika mzee ili adhibiti kasi kama inakwenda sana, lakini sio CEO wa nchi. How Old was Lumumba? How old was Kagame? How old is Kabila?
Let us be serious guys. Mnataka tutambae? Wazee wameishi maisha yao. Wameishi yetu na sasa tunataka kuwakopesha maisha ya watoto wetu?