PiedPiper77
Senior Member
- Jan 8, 2025
- 146
- 196
===
KWANINI FREEMAN MBOWE HASTAHILI KUCHAGULIWA TENA?
(Isomwe na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na Wanachama wote)
Na Mwandishi wetu.
Chama chochote cha Kisiasa popote pale Duniani lengo lake kuu la kufanya Siasa ni kushika dola.
Na Kiongozi Mkuu anayeongoza Chama cha Siasa aidha Chama Tawala ama Chama cha Upinzani, hupimwa kwa namba ya mafanikio yake.
Na inapotokea Kiongozi huyo anataka kugombea nafasi yoyote ndani ya Chama, namba za mafanikio (kwa muda huo anaomaliza Uongozi zinambemba zaidi)Lakini ikiwa huna namba zinazokubeba katika awamu ya Uongozi unaomaliza, huna sababu tena ya kurudi kuomba kura mbele ya Wajumbe.
Mhe. Freeman Mbowe amebebwa na namba (tangible evidence) za mafanikio kwa awamu tatu lakini sasa, namba zimemkataa. Siku zote "namba hazidanganyi".
Nitawapa mifano kadhaa hapa ya namba zilizokuwa zinambeba Freeman Mbowe.
WABUNGE, MADIWANI & HALMASHAURI ZA CHADEMA
Mwaka 2005 Wabunge 11, Madiwani 103, Halmashauri 02.
Mwaka 2010 Wabunge 48, Madiwani 467, Halmashauri 7
Mwaka 2015 Wabunge 70, Madiwani 1,133 na Halmashauri 14
Zile sifa zote unazosikia wakina Mhe. John Heche, Mhe. Tundu Lissu Mhe. Godbless Lema wanamwagia Mhe. Mbowe ni pamoja na mafanikio kama haya.
Hakika, kufikia hapa Freeman Mbowe alikuwa amekikuza Chama hadi kufikia viwango vya juu sana
Na kwa maoni yangu, baada ya hapa alipaswa sasa kumkabidhi kijiti Mtu mwingine aendelee na ujenzi na ustawi wa Chama. Lakini hakutaka kuacha bado akaendelea. Ili sasa na yeye ale matunda ya kazi zake.
Wakati huo wote CHADEMA ilikuwa na Watu mahiri sana waliokuwa wanaogopwa kuanzia Bungeni mpaka nje ya Bunge.
Wanaogopwa mpaka na Serikali katika masuala ya mijadala ya Kitaifa na misimamo ya kutetea haki za Watu.
Watu waliokuwa wanakemea rushwa hadharani na gizani.
CHADEMA ilikuwa na Watu kama hawa;
Sasa nakuonesha namba zilivyokuja kumkataa Freeman Mbowe na tangu hapo Wanachama wa CHADEMA, Watanzania na wadau wa Siasa za CHADEMA wakaona ipo haja ya kufanya mabadiliko ya Uongozi.
Mwaka 2019 Uchaguzi wa Serikali za Mitaa CHADEMA haikuwa na Mwenyekiti wa Mtaa, Kijiji wala Mjumbe Nchi nzima. CCM ikaachiwa ijitawale.
Mwaka 2020 Mbunge 01, Madiwani wasiofika 100 Nchi nzima, bila Halmashauri.
Mwaka 2024 kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. CHADEMA imepata Vijiji 97 tu Nchi nzima kati ya Vijiji 12,280 vilivyofanya Uchaguzi.
Vitongoji 853 kati ya Vitongoji 63,849.
Hizi ndizo namba zilizomkataa Freeman Mbowe.
Hazimbebi kabisa kwa miaka mitano yote.
Kwa takwimu hizi, ni dola ipi hiyo tunayotamani kuishika?
Hebu fikiria hata ungekuwa ni wewe, unaambiwa Kiongozi wako amefanya maridhiano na Chama Tawala, halafu unakuja Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mnanyang'anywa Mitaa na Vijiji karibu vyote.
Wewe unaweza kumuelewa mtu anayetaka akuaminishe kuwa, hayo maridhiano yameleta faida kwa Chama ilihali hamjapiga hatua hata moja kuelekea lengo mama, ambalo ni kushika dola?
Swali la msingi ni kwamba, ikiwa Mwaka 2019 CCM ilipora Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na hakuna kitu alifanya.
Mwaka 2020, CCM ikapora tena Uchaguzi Mkuu na hakuna kitu alifanya.
Mwaka 2024, CCM imepora kwa mara nyingine Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na hakuna kitu amefanya.
Je, anataka aamiwe kupewa Uenyekiti wa Chama kwa mara nyingine ili akatuletee manufaa gani tena?
Ukipewa Uenyekiti wa Chama tena, maana yake ni kwamba tutegemee kuporwa Uchaguzi Mkuu wa 2025 pamoja na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2029 na hakuna kitu utafanya.
Lakini kumbuka lengo la Chama cha Siasa ni "kushika dola".
Na kwa jinsi ulivyoongoza kwa miaka ya hivi karibuni, umetuongoza katika kuporwa dola sio kushika dola.
Ni dhahiri kuwa hakuna dalili ya kushika dola.
Na ndio maana Wanachama na Watanzania wanatamani kuona Chama hiki kinakabidhiwa kwa Mtu mwingine ambaye ni Mhe.Tundu Lissu na yeye akimbizane nacho katika kukijenga na kukiimarisha upya ili tuone matokeo yake pia.
Mhe. Freeman Mbowe akiwa anazungumza huwa anapenda kutumia maneno ya kwamba "Chama cha Siasa ni sawa na Timu ya mpira" kwamba kila mmoja anacheza katika nafasi yake ikiwa ni kipa, beki au forward.
Sasa nataka kumkumbusha Freeman kuwa, ni kweli Chama cha Siasa ni kama Timu ya Mpira wa miguu.
Lakini akumbuke kuwa, yeye kama Mwenyekiti ndiye Kocha Mkuu wa Timu hiyo ya Mpira.
Ninampongeza kwakuwa, aliipandisha Timu kutoka kucheza ndondo Cup hadi kufika viwango vya juu vya kucheza kwenye Ligi Kuu.
Imefanya vizuri ikawa na Matokeo mazuri nusura kubeba kombe.
Lakini ghafla kwa miaka mitano baadae, timu yetu (CHADEMA) inaenda kushuka daraja.
Kwahiyo wenye Timu wameamua kumpuzisha Kocha ili aletwe Kocha mpya wa kuokoa Timu isishuke daraja.
Mwisho, Mhe. Freeman, hebu kaa tafakari uangalie Watu ulionao sasa kwenye Siasa kama kweli ni taswira ya Watu wanaokwenda kushika dola?
Yaani kuanzia hapo Makao Makuu, Maafisa na Viongozi wengine. Je, ukishika dola hao ulionao sasa ndio watakuwa Maafisa wa Serikali? Surely??
Yaani leo hii;
Yaani umeamua kuwaundia zengwe Watu ambao ni "prominent figure" kwenye Chama hiki na wamekuwa ni icon ya CHADEMA kwenye Nchi halafu unategemea kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti?
Yaani leo hii, huwataki tena wakina;
Jamii ya Watanzania na Wanachama hawawezi kukuelewa wala kukuamini tena.
Kwasasa hao ni Wapinzani wanaoaminika sana kwenye Jamii.
Kuwatenga ni kufanya kosa kubwa sana.
Fanya tafakuri ya kina, jiulize ni kwanini Chama kinatenegeza Watu halafu wanaondoka kwenye hiki Chama?
Fanya tafakuri, kwanini sasa hivi zaidi ya 80% ya Vijana hawakuhitaji tena kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Chama hiki?
Rejea matukio ya ukumbini ya Mkutano Mkuu wa BAVICHA Taifa. Vijana wanamuimba na kumshangilia zaidi Tundu Lissu maana ndiye nana imani naye kwasasa.
Ulisema kwa mujibu wa takwimu za Sensa, kwasasa 75% ya Population ni Vijana.
Sasa hao Vijana hawakuhitaji tena, jiulize unagombea ili ukafanye kazi na nani???
Ukipata majibu, bado hujachelewa unaweza kuamua hata hiyo tarehe 21/01/2025 ukiwa ukumbini.
Joseph Mohonia
Kijana wa Chama.
15/01/2025
mohoniajoseph@gmail.com

- Prof. Abdallah Safari
- Dkt. Wilbroad Peter Silaa
- Dkt. Vincent Mashinji
- Joshua Nassari
- David Silinde
- Anthony Komu
- Joseph Selasini
- Wilfred Lwakatare
- Halima Mdee

- Daniel Naftali amekuwa mbadala wa Dkt. Vincent Mashinji??
- Yericko Nyerere amekuwa mbadala wa Prof. Safari??
- Martine Maranja Masese amekuwa mbadala wa Joseph Selasini?
- Ntobi amekuwa mbadala wa Peter Msigwa? Like seriously???
Yaani umeamua kuwaundia zengwe Watu ambao ni "prominent figure" kwenye Chama hiki na wamekuwa ni icon ya CHADEMA kwenye Nchi halafu unategemea kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti?
Yaani leo hii, huwataki tena wakina;
- Mhe. Tundu Lissu
- Mhe. John Heche
- Mhe. Godbless Lema
- Mhe. Peter Msigwa