Mahusiano ah.............

ehh! eti nyie wanaume kwann msihamie huko huko kikaeleweka umemchoka mkeo?

yaani mwanaume kageuka keyholder, jamani, kama haya ammbo mtu hujayapitia utaona kama filamu za kihindi, ngoja likukumbe.
 
ehh! eti nyie wanaume kwann msihamie huko huko kikaeleweka umemchoka mkeo?

Inawezekana akihamia uko ladha ya small house itaisha kwahiyo ndio maana inakuwa COME AND GO, GO AND COME
 

sasa mbona huyu mbaba mwenzenu kalifumbia jicho hili jambo, kafumwa bado anaendelea...mhh..Baba E, mie mwanamke hawara akinitumia msg kunijulisha kama yupo na mr kwa kweli kutachimbika, atapatikanika tu kwenye anga zangu hata awe anaishi rombo mpakani.
 
Acha mpenzi ....mwenyewe anasema anamuomba huyo bi mdogo amuachie mume wake la sivyo atakapomkamata atamfanya kitu asichoweza kuamini na hata kama kitapelekea kuachwa na mumewe hatojali.Sasa watu wakawa wanamwuliza kwa nini unajipa presha wakati kama mume kakutelekeza (kwa maana ya kuwa hamjali kuamka wala kulala yake ingawa yupo nyumbani) kwa miaka sita na bado umemudu maisha ya nini kujipa presha? unajua kajibuje...............nampenda mume wangu!!
 
Kuna sehemu lazima something is wrong

hauwezi kurekebisha?..jamani humu ndani kuna mengi ukisema tu tatiz olimetokea bac soln ni kupata nyumba ndogo itatumaliza kabisa, na haya magonjwa God forbid.
 
nyamao unasema tu kutachimbika wapi unafikiri mambo yote yanahitaji ubabe inaweza ikawa ubabe wako ndo ulimkimbiza hlafu mi naamini kudili na nyumba ndogo sio suluhisho utapoteza muda wako maana mara nyingi hawa wapo kimaslahi zaidi hangaika na mmeo
 
 

Umemsemea Babu Asprin maneno yake yote.

Ntakuzawadia JOSEFINA wa Baa Mpya.
 

HA HA HA HA nyumba ndogo bwana zikikukamata dah sijui uwa wanakuwa na nini wale
Hapo sasa ndo mnapochetuka ati...unapokandya kwa mkeo nyumba ndogo inavidaka aohhh kumbe mkeo anakupangia ratiba .basi mie utapata kuanzia tarehe 1 hadi 1 ya mwezi... kama mkeo hafui kufuli zako anakuachia ufue mwenyewe basi nyumba ndogo anazivaa kabisa mwashare...mara oh mke wangu mie bwana tukimaliza anakimbilia kuoga yeye......basi small house atakuwekea thermos uchagoni usipate shida ya kwenda hadi bafuni.... sasa hayo yote ndo unaona ah mwanamke si huyu kumbe ndo umempa majibu mwenyewe.
 

Amenifurahisha sana hapo kwamba anampenda ila akimkamata mwizi wake ndio balaa
 
nyamao unasema tu kutachimbika wapi unafikiri mambo yote yanahitaji ubabe inaweza ikawa ubabe wako ndo ulimkimbiza hlafu mi naamini kudili na nyumba ndogo sio suluhisho utapoteza muda wako maana mara nyingi hawa wapo kimaslahi zaidi hangaika na mmeo

pale atakaponikosea heshima kama huyu ni deal nae, ale huko huko na anyamaze sio mpaka anitumie sms nijue, kwa dizain hii nitaanza nae then namalizia na mhucka, ikifikia hapo ni kwamba nipo kwenye stage ya kuharibu so akijickia kukusanya vinguo vyake akaanze lyf jipya itanisaidia zaidi, pale nyumbani ctatoka hata kama akiamua kuishi hapo lakini acje mwezi, tutabanana pale pale mpaka kieleweke, nani akahangaike saa hivi kumimbizana na watoto?
 
Umemsemea Babu Asprin maneno yake yote.

Ntakuzawadia JOSEFINA wa Baa Mpya.

Babu taratibu!

JOSEE mh! acha tu ::: Jana Ndovu na Serengeti ziliisha nadhani kwa sababu ya JOSEE! Kama kuna mashindano ya kunywa vile!
 

HA HA HA HA Risasi zile zile lakini bunduki tofauti
 
hapa ndo huwa nawashangaa watu hivi ukioa au kuolewa basi ndo mwisho wa kupenda tunaamua na kuamini kwamba huyu niliyepata takuwa msaidizi na rafiki na unaamua kufunga milango sasa hapa ndo huwa tunajichanganya ivi huwa tunajiulizaga tulikuwa sahihi kwenye maamuzi yetu na kama tulikosea ni wapi turekebishe kutumia nguvu nyingi/ubabe ndo kutarudisha mapenzi atapigana na wangapi mamamtu akikuchoka haijalishi ni mmeo au mkeo atatoa lolote mdomoni sasa hapo kazi kwako kufanyia kazi kwa busara na kutafuta positive ways za kutibu majeraha yako
 
 
ehh! eti nyie wanaume kwann msihamie huko huko kikaeleweka umemchoka mkeo?

Ndo maana nakwambia hapo juu ukiona mwanaume anamkandia mke wake nyumbani hiyo nigia ya kukupata wewe na kisha akutafune
 

hivi halafu kwannn watoke nje na bado watudhalilishe kwa kutupaka maneno ya ajabu ajabu, ndio mbinu pekee iliyobakia ya kutuchafua ili hao wanawake wachanue vizuri, jamani jamani hapana mambo ni magumu kwemye hii sector.
 
Hakuna kisicho na sababu. been there myself.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…