Mahusiano hayataki nguvu nyingi ikiwa upendo upo kati, ukiona hivyo hamishia hizo nguvu kwenye biashara

Mahusiano hayataki nguvu nyingi ikiwa upendo upo kati, ukiona hivyo hamishia hizo nguvu kwenye biashara

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
Nguvu tunazotumia kuwekeza sehemu tusipotakiwa huwa ni kubwa sana kiasi kwamba hizo nguvu zingewekezwa pengine zingeleta matokeo chanya na makubwa.

UKIONA UNATUMIA NGUVU NYINGI NI DALILI KUWA UPO UNALAZIMISHA USIPOTAKIWA.

Usilazimishe usipotakiwa na usifanye hili kosa tena kwa sababu itakugharimu kiuchumi, muda mpaka fikra kutafuta kipi kitamfanya akuone wewe ndiye anayekuhitaji.

UKIONA UNATUMIA NGUVU KUBWA JUA UPO UNALAZIMISHA USIPOTAKIWA, MAHUSIANO HAYATAKI NGUVU BALI KUELEWANA TU LUGHA.

Ukihusiana na ambaye mnaelewana lugha zitakuwepo changamoto tu za kawaida kama ilivyo kuwa hakuna safari nyoofu ila mkipishana basi mmoja ataumia sana kwa sababu kwenye mijadala kumi basi miwili tu ndio italeta furahi ila nane yote itawaacha na majonzi.

JIFANYIE TATHIMINI YA NGUVU UNAYOTUMIA KWENYE MAHUSIANO NI ZAIDI YA KAWAIDA?

Mahusiano yanayofanya uyafikirie sana na kutumia vitu sana ili kupendwa jua upo UNALAZIMISHA.

#Mwanasayansi Saul kalivubha.
#Fikia Ndoto Zako.
 
Back
Top Bottom