MAHUSIANO: kazi Kweli kweli......!!

Mi pia nina mshkaji mtoto wa mamkubwa hatoki. Alikuja akasema anakaa wiki sasa ana miezi mi 2. Sijaoa na wala sina mke na yy hana shughuli. Hasomi alf hata kazi hatafuti. Tena kwa mizinga huyo. Cjui mwisho wake itakuwaje.

Mlie Tyming!
 
watu wa musoma ndo zao,yaani nina dingi mdogo mke wake ni wa huko musoma..ukienda kwake ni full wageni wa upande wa mkewe,..mpe pole huyo mdada

duh!Inatisha Aisee!
 
Pangisha, waachieni nyumba ili mama mkwe aendelee kualika ndugu zake kwa uhuru!
Kama mums anawapenda ndugu zake awape huduma wakiwa kwao lakini sio wakubanebane!

Mpango Mzima!
 
Khaaaaaaaaaaaaa.....

Mumeo ndo pekee mwenye uwezo wa kuokoa ndoa yako.....

Akisimama kama mwanaume, hata mngekua mnaishi na kijiji hapo kwako wote wangefuata sheria zenu........ Lakini ukiwa na mume dhaifu matokeo yake ndo hayo.....

Bibie vumilia tu......
Hapo unatakiwa ujali mumeo na wanao tu...uweke hg specific kwa wanao na boss ni wewe tu sio mama mkwe...

Kuhusu maji mbonma simple?? Hakikisha una maji ya kukutosha wewe na mumeo,na wanao....

Formula ni asiyefanya kazi na asile...

Vitu vyako valuables vifungie au mpelekee mama yako avihifadhi....

Kama ulikuwa unachangia matumizi ya nyumba acha, hela yako dunduliza nunua kiwanja......

Kisha sali sana mumeo asifumbe macho, akivuta tu umeumia....
 

hlo Neno Zito Sana Bila Shaka Alifanyie Kazi!
 
Hapo pagumu mama
Hivi watu wengine huwa wanashindwaje kukaa kwao jamani?
napenda wageni ila hii too much
..Hivi kama mie nina kwetu kwanini nikajaze mzigo kwa watu ..
 

mweee.....nimeudhika sana kwa kweli.....raha ya mume mkae ndani mwenu muanzishe familia yenu......ndugu wakija leo kesho waondoke......mama mkwe kuja kukaa kwangu hilo ni kosa la jinai.....coz hata mama yangu hawezi kukubali kukaa kwangu......
 
hata hao wakigoma kuna shemeji yangu kaacha nyumba kahama na mkewe kwenda kusoma nje na nyumba akapangisha maana alikuwa wageni wanafika mpaka 20 du sasa wakati wanawaambia kuwa wameamua kuhamia nje mmja wao analalamika oh nilijua maish ayangu yataishia njiani alikuw anakula na kulala anaambiwa apelekwe shule hataki du,yaani maisha hayo nimabaya sana ukichinja hata kakuku huwezi kafaidi ,kha inabodi kuwasaidia mimi binafsi ni mhanga wa hili jambo ila ikifika pomonni nawafukuza au naweka mkakati kuwa hapa ni kulala tu kula utajua mwenyewe!
 

Pole sana kwa yaliyokukuta! Kuna mtu ninayemfahamu aliwahi kupitia tatizo Kama Lako isipokuwa yeye alikuwa ni mume mtu, mke wake alileta wazazi wake hapo nyumbani na wadogo zake. Isipokuwa hiyo familia ya mke walikuwa wastaarabu na waelewaji. Ila mume alikuwa uncomfortable, so akaamua na mke wake wawaache ndugu wa mke hapo na wao wakaenda kupanga kwingine, na ikumbukwe hata nyumba waliyowaachia ndugu wanalipia rent pia na matumizi wanapeleka. Ila for the sake of children waliamua kufanya hivyo and now they are happy and peaceful. So ukiweza mdada jaribu kufanya hivyo au wazo lingine, punguza hao wadogo kwa kuwapeleka boarding school. Funga na kuomba kwa ajili ya hili Mungu atakuonyesha njia, it is a very challenging situation lakini Ndoa lazima iokolewe, Mungu hapendi Watu waachane! Good luck.
 

Hii Nayo ukiweza fanya..sometimes inabidi uwe aggressive..wapende yes, ila na wao lazma wawajibike!
 
mweee.....nimeudhika sana kwa kweli.....raha ya mume mkae ndani mwenu muanzishe familia yenu......ndugu wakija leo kesho waondoke......mama mkwe kuja kukaa kwangu hilo ni kosa la jinai.....coz hata mama yangu hawezi kukubali kukaa kwangu......
We hujakasirika kama mimi kha
 
Kuna baadhi ya makabila yanasifika kwa hii tabia, ukiolewa ujue umeolewa na ukoo mzima na ukioa ujue umeoa ukoo mzima, lakini huyo bi dada aliona hali halisi toka mwanzo kwa nini alikubali??
 
kuishi na ndugu lawama katika maisha ya ndoa bora muishi peke yenu ndugu wahudumiwe huko waliko angalau kunakuwa na amani. pili wanaume inabidi tuwe na msimamo hasa tunapoishi na ndugu. mshauri mumeo mhame na watoto mkae mbali kidogo. ila hatma ya amani na furaha ya moyoni mwako iko mikononi mwako ndoa isikuweke kifungoni za JF changanya na zako
 
Pangisha, waachieni nyumba ili mama mkwe aendelee kualika ndugu zake kwa uhuru!
Kama mums anawapenda ndugu zake awape huduma wakiwa kwao lakini sio wakubanebane!

hata ukipanga nyumba watakufuata tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…