Habari wana JF
Bila kupoteza muda nijikite moja kwa moja kwenye kilichonifanya kuandika yumkini nikapata ufumbuzi wa changamoto yangu.
mwenzenu kuna kitu ambacho kimekuwa kikinisumbua miaka mingi sana japo kuwa mwanzoni nilikichukulia poa sana lakini kumbe nilikuwa nakosea.
Once napoamua kuwa na mahusiano najijuta napitia kipindi kigumu sana kiuchumi na hata miradi yangu yote inakufa nakuwa ni mtu wa madeni yasiyolipika kila mirija yangu ya kuingizia kipato inaziba lakini nikiwa single mambo yangu yanaenda vizuri sana
Mwanzo nilijua labda ni hali ya kawaida tu kwenye maisha kuna kupanda na kushuka hadi nikafika mbali nikawaza kuna msemo wa nabii hakubaliki kwao.
Nikatoka hadi nje ya nchi kupambana zaidi lakini bado hali ilikuwa sio kabisa.
Nikiwa nje ya nchi ilitokea kutofautiana na mwanamke niliyekuwa naye katika mahusiano sababu wakati tunaanza mahusiano nilikuwa vizuri sana kiuchumi, sasa baada ya kuona siku hadi siku nadrop financially akanihisi nina mwanamke mwingine ndipo nikakopeleka pesa, mwishowe niachwa😔
Baada tu ya kuwa single mambo yangu yakanza kwenda vizuri sana zaidi ya mwanzo pesa ilikuwa inaonekana, miradi ilikuwa inaenda vizuri kabisa tabasamu likarudi nikasema sasa ngoja nitafute mwanamke nioe kabisa mapambano yaendelee.
Nilifanikiwa kumpata niliyemwona anafaa kuwa ubavu wangu, nikiwa kwenye process za kupeleka mahari moja ya mradi wangu uliokuwa unaniingizia pesa nzuri uliingiwa na mdudu changamoto, sijakaa sawa miradi mingine ikaanza kusizi na kufa kabisa kilichonishtua zaidi kuna mradi wa nyumba za kupangisha zilikuwa zimekamilika tayari kwa kupangisha mvua ilipiga zikaenda na maji zote.
Ikabidi nirudi nchini kwanza kutuliza komwe langu na kutafari zaidi, baada ya miezi kadhaa mwanamke niliyekuwa naye kwenye mahusiano naye akaanza kuniona kama hanielewi vile, ikabidi nikae naye na kuzungumza kwa kina lakini mazungumzo yangu aliyapokea tofauti na nilivyotarajia kwani alireact sana na kusema kwahiyo yeye ndiye anayeleta nuksi kwenye mafanikio yangu,, nimwambia no, nikajitahidi kumwelewesha vizuri hakunielewa nikaachwa kwa mara ya pili.
Bahati mbaya ni kwamba sina wazazi pande zote mbili hivyo nikiwa kwenye nyakati ngumu huwa napenda kujipa muda na kuhama mazingira na mimi ni mtu ambaye sina marafiki kabisa hivyo nikarudi tena nje ya nchi kupambana na maisha nikaendelea kuwa single taratibu nikaona mambo yangu yanaanza kurudi kwenye mstari.
mpaka sasa nina miaka 33 ilifaa niwe na mke na watoto kabisa lakini kikwazo ni hiyo hali nayokutana nayo kila napoamua kujihusisha na mahusiano.
Naombeni ushauri wenu tafadhali
Mawasiliano zaidi: joshuapeter2506@gmail.com