Mahusiano na dada wa kambo

HideYoKids

Member
Joined
Jan 11, 2025
Posts
52
Reaction score
72
Habari wa ndugu, Heri ya mwaka mpya natumaini wazima ,

Nimekuja na hii mada sio kwa lengo la kujisifia au kutangaza dhambi ya zinaa ninazofanya nimekuja na huu uzi sababu nahitaji ushauri pengine msaada wa kimawazo maana nahisi sio kawaida

Nisikuchoshe nipunguze maneno ni hivi kipindi nipo sekondari mama aliachana na baba baada ya kipindi kupita akaolewa tena na huyo mume aliyemuoa alikuwa ana binti yake alizaa na mwanamke mwengine mimi na mama wote tuliamia kwenye familia hiyo ambapo ni baba anaishi na binti yake makamu yangu hata kidato tulikuwa kimoja, Sasa sijui kuishi ndugu wawili wakike na wakiume wasio wa damu inachangia au shetani au ni tamaa zetu mbovu tulijikuta mimi na huyo binti ambaye ni dada yangu wa kambo tunaingia kwenye mchezo mchafu.

Tulifanya kwa siri . Kipindi wazazi walikuwa hawapo tulikuwa tunafanya mapenzi sana saa nyingine binti ananyata usiku anakuja chumbani kwangu saa nyengine naenda chumbani kwake saa nyengine sebuleni ikawa ndio michezo yetu mpka tukanogewa tukajikuta tunapendana maana hizi constant casual sex na mtu mmoja lazima mcatch feelings . So ikaenda ikaenda ye akapata mahusiano mapya na mimi pia lakini bado roho zetu hazikuridhika ilibidi dada yangu aachane na mtu wake na alikuwa na wivu na mimi na hakutaka kujihusisha na mahusiano ikafikia kipindi nikaenda chuo na yeye mkoa tofauti bado tukawa tunafatana kitendo cha mimi na yeye kuwa mbali kinatuumiza moyo in short tunapendana sana

Mama yangu hakufanikiwa kuzaa na huyo baba wa kambo na walikuja kuachana lakini sisi hatukuacha mawasiliano na mahusiano wote tumekuwa na mahusiano na watu mbalimbali lakini tumeshindwa maana kila mmoja moyo wake yupo kwa mwenzake .sasa tunajitegemea kila mtu yupo kwake lakini tumeshindwa kuachana

Natamani kumuoa lakini alikuwa dada yangu wa kambo na tayari baba yake alishaachana na mama yangu natamani tusipendane lakini tunashindwa , mahusiano yetu ya siri toka tuna miaka 17 na sasa ni watu wazima jamii itanichukuliaje ikijua ?nifanye nini nimsahau? nimchukie au pengine tunahitaji msaada wa kisaikolojia hata sielewi maana wote tulipanga tuachane lakini imeshindikana sometimes najuta kwa nini nilikutana naye au kwa nini mama yangu alikubali kuolewa na baba yake .


Natamani nimkimbie nibadili mawasiliano lakini atafanya juu atanipata saa nyengine nashindwa kujificha kuna kipindi tuliachana tulishindwa maana tulikuwa katika hali mbaya sana kiufupi tunapendana sana na tunatamani uhusiano wetu uwe wazi tuoane lakini ndio hivyo sio sawa katika jamii.

Ni hayo tu samahani kwa ambao bandiko hili litawakwaza
 
Muoe huyo sio ndugu yako.Hiyo ilikua njia ya kukutanishwa na mkeo mtarajiwa
 
Hilo suala wazazi wenu hawatakuwa tayari.
Baba wa huyo dada yako alikulea kama mtoto wake, namama yako akamlea huyo binti kama mwanae, hii mnaleta aibu kwa wazazi wenu na jamii nzima.

Usije kushangaa wazazi wakawalaani mkijifanya mnapendana sana na kutowasikiliza.
Kama mtaendelea kulana kimasikhara endeleeni ila suala la kuoa, utamfanya mama yako akuone ni mtoto mjinga na huna akili.
 
Kweli Kuna kusoma na kuelewa
 
Una bahati sana Mkuu mshukuru sana Mama yako, hapo hauna hata haja ya kutoa mahari unaoa tu.
Nina bahati mbaya kukutana naye pengine nisingekuwa katika hali hii . ukilinganisha huyo dada ni dada yangu wa kambo


Sometime nawaza pengine mama asingeolewa na baba huyo nikakutana na huyo binti kwa njia nyingine pengine ningekuwa ni mtu mwenye bahati dunia hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…