Mahusiano na Ushirikina, umakini unahitajika

Mahusiano na Ushirikina, umakini unahitajika

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Copy&paste👇umakini unahitajika sana.

Nyie mwenzenu 😭😭😭😭😭😭natamani kulia mimi yamenikuta

Mwenzenu nipo kwenye mahusiano na kaka mmoja mkoa fulani. Yeye ni mfanya biashara mkubwa tu wa mbao Malawi kuleta Tanzania

Miaka mingi nipo nae sijawahi kuona maajabu Kama niliyoyaona jana. Nyie mwenzenu naomba mniombee nahisi kufa

Alinipigia simu kabla sijaonana nae akaniambia hizo shanga ulizonazo sizipendi tafuta shanga nyeupe zitakupendeza mie tena nikakubali.

Akasema kesho tuonane nimekumis ndo Jana sasa.

Nikajiandaa mapema akaja kunichukua home, tuaondoka mbaka mjini

Akaniuliza shanga wanauzaje leo ni

nataka uwe umevaa shanga nyeupe nikasema sawa.

Nikamwambia bei yake akanipa nikanunue pale tulipo kuwepo ni maeneo hayo hayo Kuna wauzaji wa hizo shanga

Basi tukaenjoy weee kama mida ya saa 5 ndo tukarudi kwake kulala. Basi tulifika me nikataka kuoga ndo nilale akanikatalia akasema vua hizo shanga zako

Vaa hizi nyeupe mie chap nikavaa anazotaka, Nikapanda kitandani nikalala naye akalala

Tukazagamuana tulivyomaliza tu akaniambia vua shanga hizo nipe

Hee nikashtuka tena kunakuzitoa kumbe

Nikagoma akawa mkali ghafla basi nikazitoa nikampa akaweka chini ya mto wa kulalia🙆🙆🙆🙆
Tukalala mpaka asubuhi mida ya saa 12 nikaamka Ili niondoke niende kwangu nijiandae kwenda kazin

Na yeye akaamka muda ule ule nikasema ngoja niziibe shanga niondoke nazo hazikuwepo pale na yeye alivyoamka hakuzishika kabisa na kwasababu alikuwa mtupu hata kusema ameamka kahamisha sio kweli.

Nikamuuliza kwann shanga umeniambia nikupe tena na ulininunulia mwenyewe akasema we tulia sio Kila kitu ujue, nikifanikiwa na wewe umefanikiwa nyie mwenzenu nimeshinda leo kazini Sina Raha najitahidi kumuuliza hasemi ukweli

Anazunguka zunguka tu
Tena asubuhi alinipeleka yeye mwenyewe nyumbani akanisubir nijiandae akanipeleka kazin

Imefika saa saba kaniuliza unakula Nini nikuletee nikamwambia chochote

Akasema sawa,kweli akaleta chakula sijala mpaka sasa nakiogopa.

ana Nia gani huyu simuelewi.
 
Wafanyabiashara wakubwa wengi wana mambo mazito sana na huyo mwenzako yawezekana yupo kwenye anga hatari za ushirikina. Watu hawa wanapewa masharti mengi na magumu ili kujipatia utajiri na wanaweza kuambiwa hata wamtoe kafara mtoto, ndugu au rafiki wa karibu ili mambo yao yawe safi.

Jinsi shanga zilivyotoweka inasema mambo mengi ila haya machache:
1.Kwamba ana uwezo wa kutuma shanga hizo kwenda atakako akiwa hapo ndani
2. Ana uwezo wa kukufanya ulale usijue kinachoendelea
3. Anaamka usiku bila wewe kujua na kwenda vikaoni.

Manake huyo ni mchawi, au hata freemason (wana nguvu zaidi ya wachawi wa kawaida)

Kama umeshamshukia hivyo basi kuwa mwangalifu sana na anza maombi ya kujitenganisha naye.

Niulize tu itasaidia zaidi kujua kuhusu huyo bwana:
1. Utajiri wake ulianza lini?
2. Makadirio ya utajiri wake yapo vipi?
3. Je wewe au yeye mpo vp kuhusu masuala ya dini?
4. Yeye hutumia vipi fedha anazopata? Mtu wa starehe nyingi?
 
Ameshakwambia akifanikiwa na wewe utafanikiwa.
Akiyatimba na wewe utayatimba.
 
Back
Top Bottom