Mahusiano ya Diamond na Clouds FM yatakuwa salama?

galton

Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
80
Reaction score
126
Kulingana na hivi karibuni msanii mkali bongo, Diamond platnums kutoa wimbo wake mpya unaoitwa "bora nikae kimya" huku ndani ya ngoma hiyo akiwa ameitetea serikali na mkuu wa mkoa paul makonda ,ambao ni maadui wakubwa wa wananchi pamoja na kituo cha radio na Tv nchini ,clouds media ,je urafiki wa diamond na ruge pamoja na wafanya kazi wa clouds bado utakua salama?
 
Urafiki utabaki pale pale kwasababu kuna biashara diamond unafanya na Kusaga!
ila huo wimbo sidhani kama utachezwa.....
 

Warumi tumekushtukia.
 
Urafiki utabaki pale pale kwasababu kuna biashara diamond unafanya na Kusaga!
ila huo wimbo sidhani kama utachezwa.....
Siku hiyo hiyo Diamond ametoa ulichezwa mara mbili, binafsi sijawahi kuusikia sehemu yoyote zaidi ya Clouds mara mbili, na TBC Taifa mara moja tena kwenye daladala

- Jamani alipofika Diamond ni biashara tosha na hasuswi, na ndio maana hata show zao nyingi anakataa
 
Nilijua watamshit, ila siku hizi hawamfagilii kivilee coz ya makonda
 

Wewe koma, mie sio maadui zangu. Siasa zenu za uchonganishi peleka hukohuko kwa wachonganishi wenzio.
 
ni kweli yanaweza kuzorota ila kikubwa kinachoangaliwa ni biashara. mfano tangu siku za nyuma Ali Kiba yupo karibu na Lady JD lakini Kiba bado yupo nao fresh tu clouds.
 
Acha uongo, umesema Rais na Makonda ni maadui wakubwa wa wananchi!! Huo uadui unauthibitishaje? Umetumia kigezo gani kusema hao watu ni adui kwa wananchi?.
Next time usilete hisia zako binafsi na kuwasemea watu zaidi ya mil 50
 

Tafadhali sana usidhani wote tunawaza kama wewe, kama una chuki ni za kwako binafsi. Mimi binafsi huniambii kitu kwa CCM, Serikali ya CCM na Mkuu wa mkoa Makonda. Niwachukie hawa halaf nimpende nani????????????????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…