Mahusiano ya elimu na ukoloni mamboleo

Mahusiano ya elimu na ukoloni mamboleo

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
ELIMU YETU NDIYO MSINGI WA UKOLONI MAMBO LEO.

Na Elius Ndabila
0768239284

Msingi mkubwa wa Maendeleo Duniani kote ni elimu. Hapa tunazungumzia elimu rasimi na isiyo rasimi mhimu ni ile elimu inayosaidia kumuondolea mtu mwamvuri wa ujinga na kumjengea uwezo wa kutazama mambo kwa mawanda mapana. Hivyo kitu kinachoondoa ujinga ni elimu.

Elimu ya Afrika inatazamwa bado kuwa haiwaandai Watu kuondolewa ujinga kwa falsafa ya mtazamo wa kiafrika, bali inawaanda kutengeneza mazingira ya kuondoa ujinga kwa falsafa ya tamaduni za kigeni ambazo msingi wake ni kuendelea kuikalia Afrika.

Tunahitaji kutumia sana elimu yetu ya asili katika kupambana na harakati za kujikomboa katika ukoloni mambo leo ambao umeota mizizi katika fikra zetu kuwa bila nchi za Magharibi hatuwezi kuendelea. Lakini pia ni mhimu kujua mifumo ya elimu ya wenzetu inayoweza kuhuisha elimu yetu. Lakini ni mbaya kuchukua kila kitu kutoka mataifa makubwa huku tukiacha asili ya elimu yetu iliyowapa farao umaarufu.

Mwanafalsafa Plato aliwahi kusema hivi "Kila kitu kitazalishwa kwa kiasi kikubwa na ubora, na kwa urahisi zaidi, wakati kila mtu anafanya kazi katika kazi moja, kwa mujibu wa zawadi zake za kawaida, na kwa wakati mzuri, bila kuingilia kati na kitu chochote kingine.Ujasiri ni kujua nini usiogope."

Hoja hapa ni kuwa ieleweke kwamba Afrika kwa muda mrefu ilitawaliwa na mataifa ya Magharibi ambayo kabla ya kuja waliwatanguliza vitangulizi vya mabeberu kama Wapelelezi ambao walikuja kwa ajili ya kupeleleza bara la Afrika na kuanzisha Chama Cha International African Association, baadae wakaja Wamisionari ambao walikuja kueneza Ukiristo na kuua Dini za asili na baadae baadaye wakaja Wafanyabiashara.Mataifa haya ambayo yaliifanya Afrika kuwa koloni lao hawakuwa tiyari kuiachia Afrika kwani walitumia Afrika kama bara la kutafuta malighafi ya viwanda vyao na soko kwa ajili ya bidhaa zao.

Haya yalifanyika baada ya kufanikiwa kuua utamaduni wa Afrika. Maeneo mengi Afrika yalipiga hatua kubwa kinaendelea ukilinganisha na Ulaya. Kwa mfano dola za Soghai, Kumasi n.k zilikuwa na Maendeleo makubwa katika teknolojia ya ufuaji chuma.

Kutokana na kuto kuwa tiyari kuondoka Afrika ndiyo maana tunaona zipo nchi za kiafrika zilipata Uhuru wake kwa njia ya mtutu wa Bunduki na zipo ambazo zilipata kwa njia ya mazungumzo. Ugumu huu wa kuto taka kuiachia Afrika kuendelea kutawaliwa ni wazi kuwa Mataifa haya yalikuwa bado yanaihitaji Afrika kwa ajili ya Maendeleo yao.

Mataifa haya ambayo yalikuwa yameikalia Afrika yalijua fika kuwa ipo siku nchi za Afrika zitakuja kudai uhuru wao kama ilivyokuwa kwa Marekani iliyokuwa chini ya Uingereza. Hivyo mataifa haya yalianza kutengeneza mazingira ambayo yangefanya pamoja na Afrika kuwa huru, lakini bado waendelee kuwa Wajinga kwenye baadhi ya vitu ili kupelekea ukoloni mpya wa mambo leo.

Mwanzoni nimejaribu kugusia suala la Elimu kuwa elimu ndio msingi wa kila kitu. Tanzania tumeweza kwenda mbali zaidi kwa kusema elimu ni ufunguo wa maisha. Lakini ukweli ni kuwa bado elimu yetu Afrika si ufunguo wa maisha bali kufuli la maisha.

Elimu yetu msingi wake mkubwa iliandaliwa na mataifa ambayo toka mwanzo yalitutawala. Mataifa ambayo yalitamani kuikalia Afrika, ila tuliyaondoa kwa nguvu. Je, unadhani mataifa ambayo tuliyaondoa kwa nguvu yangetamani kutupatia mitaala ya elimu ambayo ingetuandaa kutujenga na kupambana na mazingira? Rahashaa!

Elimu tuliyoachiwa bado ni ile ambayo msingi wake mkubwa ni kuuchukia Uafrika na kuutukuza uzungu. Ni Elimu ambayo inathamini zaidi mambo ya Wazungu ambao ndio chimbuko la Utumwa wa Afrika kuliko Uafrika wetu.

Hujawahi kushuhudia mtu akiziamini zaidi habari mataifa makubwa kuliko za Afrika? Mtu akisikiliza habari za Al Jezira ambazo zinaikosoa Afrika anaziamini kuliko habari ambayo angesukilizia TBC. Si kosa lake bali ni kosa la elimu tuliyoachiwa.

Ili kuleta nguvu ya kujiamini na kufanya mambo yenu kwa kujiamulia jambo la kwanza unahitajika umoja au ushirikiano wenye nguvu. Afrika mipaka yetu ilichorwa na watu waliotutawala. Walifanikiwa kutugawa kwa misingi ya nchi. Mataifa yenye nguvu Duniani yameungana ndipo yakatengeneza himaya kubwa. Inawezekana Afrika kuungana ikachukua miaka mingi kulingana na mizizi ya kutugawa ilivyo jichimbia aridhini. Lakini tunaweza kuanza kuamua Afrika Mashariki au nchi za Kusini mwa Afrika kuwa nchi Moja ya shirikisho ili kujiimalisha kinguvu.

Hujawahi kuona Afrika watu wakiziamini sana dawa za kutoka nje kuliko dawa zetu za asili? Lakini tumeshawahi kujiuliza Babu zetu kabla ya ujio wa mataifa haya kuikalia Afrika je, hizi dawa hazikuwasidia?

Afrika ili kuweza kupona, tunahitaji kuufanyia marekebisho makubwa mtaala huu wa elimu. Mitaala inayoamini katika teknolojia ya Wazungu na kuua teknolojia za Afrika hauwezi kutuondolea umaskini, maradhi, ujinga n.k. Tunaweza kuondoa haya yote kwa kutumia elimu yetu ya Afrika ambayo itaendana na uhalisia wa mazingira yetu.

Ukitaka kumtawala mtu ni lazima uanze kumtawala kwenye ufahamu. Afrika tumeshatawaliwa kwenye ufahamu, lakini kwa kuwa sasa tunaweza kuona na kutambua haya ni muda mwafaka wa kuanza kuangalia mazingira ya kutoka huku. Hivi kujua kuwa kilimo cha Kilimo cha Mahindi Brazil inatusaidia nini? Au miwa India?

Leo nchi za kiafrika zimeingia kwenye mikataba mingi ya Umoja wa Mataifa, mikataba ambayo inaleta vikwazo kwenye kila hatua ambayo Afrika inatamani kufika. Jambo lolote ukitaka kufanya lazima uangalie mkataba wa Umoja wa Mataifa. Hata Bwana la Umeme la Nyerere utakumbukwa Magufuli alikutana na Upinzani mwingi. Lakini hata leo akitokea Mtanzania kuunda ndege haiwezi kuruka mpaka wao watoe ridhaa.

Msingi wa haya yote ni utakatishaji wa elimu ya kigeni ambayo ilikuja kufubaza elimu yetu na kuamini kuwa haifai. Kutokana na kutakatisha elimu yao kwetu leo Afrika ni ngumu kujinasua kutoka kwenye munyororo huu ambao lengo lake ni kuifanya Afrika kuendelea kufuata kile kinachofanyika huko.

Ili kuondokana na utumwa huu wa fikra ambao umezaa ukoloni mambo leo, ni lazima Afrika tukatafuta nguvu ya pamoja na kuamua kufanya mambo yetu wenyewe na kutumia teknolojia ya urithi wetu. Tulishindwa kuboresha teknolojia na Elimu ya babu zetu, tukakubali kuingia kwenye mtego wa vitangulizi vya ukoloni.

Utakubaliana nami kuwa zamani Misri ndiyo nchi ya mwanzo kabisa kuingia kwenye teknolojia. Ni nchi ya kwanza kugundua hesabu Duniani, lakini leo Misri iko wapi baada ya elimu ya Magharibi kuifikia Afrika. Inawezekana usielewe kirahisi, lakini maarifa yetu yalifubazwa na matayariyo ya ukoloni mambo leo.

Afrika katika Karne ya kumi na tisa jamii nyingi za kiafrika zilikuwa zimekwisha piga hatua kubwa katika kutawala mazingira hata bila kuwepo watu tunaowaabudu leo. Mapinduzi makubwa katika teknolojia yalijidhihirisha katika matumizi ya zana imara ambazo zilibuniwa na kugunduliwa na Waafrika wenyewe. Lakini baadae tuliua Vipawa hivi kwa kusema havifai ila vilivyotoka nje. Wakati tungeendelea na ubunifu ule pengine sasa Afrika tungekuwa tunaunda hata ndege.

Bara la Afrika ni bara lililojaliwa rasilimali nyingi ikiwemo ardhi yenye rutuba. Bara hili lina nchi karibia 60 mpaka sasa na karibu nchi zote hizi inakabiliwa na umaskini mkubwa.

Kweli juhudi kubwa imefanyika tangu uhuru ili kuwakomboa waafrika kiuchumi, kielimu, kijamii n.k lakini bado wananchi hawajaweza kupata huduma stahiki. Bara hili limekumbwa na vita visivyoisha vya wenyewe kwa wenyewe, njaa na magonjwa ya milipuko yasiyoisha na miundombinu mibovu.

Watu wengi wa bara hili wanaishi kwenye umaskini mkubwa ambao umesababisha elimu duni, afya duni, maji yasiyo salama wala kutosheleza,vifo vya watoto wachanga na akina mama n.k. Nchi za Bara la Afrika zimekuwa zikijishughulisha na biashara na mabara mengine ukiachilia mbali biashara kati ya nchi na nchi ndani ya bara hili. Biashara hizi zimekuwa na faida kwa nchi zilizoendelea na kwa watu wachache sana wa bara la Afrika.

Ni ukweli kuwa Badala ya kulinda na kuongeza rasilimali, viongozi wengi wa bara hili wamekuwa mstari wa mbele kutumia vibaya rasilimali za wananchi kwa kushirikiana na nchi zilizoendelea. Wakati wenzetu wa mabara mengine wanapigana kuwekeza kwa ajili ya vizazi vyao vijavyo, baadhi ya Waafrika wanapigana na kuuana wao kwa wao huku baadhi ya waliopewa ridhaa ya kuongoza wenzao wakiwaibia waliowapa ridhaa hiyo rasilimali zao na kupeleka nje ya bara.

Walichokifanya Mtemi Kimweri na Mangungu ndicho hicho hichokinachoendelea kufanyika kwa wakati huu. Baadhi ya viongozi wa Afrika ni makuhadi wa nchi zilizoendelea Nchi zinazoendelea kwa pamoja zinapoteza kiasi cha dola za Kimarekani bilioni 1 kwa mwaka kwa uhamishaji haramu wa fedha na bara la Afrika pekee linapoteza dola za Kimarekani milioni 60 kwa mwaka kwenda mataifa tajiri kupitia mapato ya bidhaa (mauzo) na mapato ya kodi Mcgroarty, (2015).

Swali ni je nani huyu anaziibia nchi zetu? Je ni mgeni? Ukweli ni kuwa kuwa elimu yetu mitaala yetu ya elimu hailengi kuamini kuwa akili akili zenye amali ya Afrika haiwezi kututoa bali elimu ya Magharibi ambayo imetutengenezea fikira zenye mirija ya ukoloni mambo leo.
 
Back
Top Bottom