Kwamacho
Member
- Apr 11, 2020
- 80
- 126
Ndugu zangu, napenda kushiriki hali yangu na ninaomba ushauri wenu.
Nimekuwa nikilelewa na bibi yangu tangu nikiwa na umri wa miaka 2 na sasa nina miaka 24 na wazazi wangu wote wapo hai mpaka sasa. Sijawahi kuonana na baba yangu kabisa ingawaje kwa sasa tunawasiliana katika simu, Mama yangu nafahamu alipo ila yupo busy sana na maisha yake na utafutaji labda kwasababu anajua ninalelewa na bibi ambaye ni mama yake hivyo sipati msaada wowote zaidi ya ninaopata kutoka kwa bibi yangu.
Bibi ndie ananisimamia kwa kila kitu na amekua ndio nguzo yangu kuu.
Nimesomeshwa shule ya msingi na bibi yangu hadi nilipohitimu na kuendelea na masomo ya sekondari lakini kuanzia hapo bibi yangu alimpatia mtu mwingine majukumu ya kunisimamia wakati wa masomo ya sekondari na rasmi nilianza kusimamiwa na kaka wa mama yangu ambaye ni mjomba.
Nimepitia mengi sana katika maisha nilipokua sekondari kwasababu nilikua kama mkimbizi au yatima na nilipopitia magumu na kukosa nuru niliulizwa wazazi wangu wako wapi wanisaidie.
Nilipiga moyo konde hadi Mungu aliponisaidia katika masomo yangu yangu ya sekondari na uvumilivu wangu ukanifanya nifanye vyema ili niendelee na masomo ya kidato cha tano.
Kuanzia hapo nilipata nafasi ya kurudi kwa bibi ambaye alitamani niendelee na masomo nikiwa karibu yake.
Kutoka hapo Nipo karibu kuhitimu diploma yangu ya Udaktari na nguvu zote ni bibi yangu pekee ambaye hajataka kumpatia majukumu mtu mwingine yoyote ingawaje kipindi hiki nipo masomoni ndio kipindi kigumu cha maisha hata kuafford kandambili ni tatizo sana lakini kikubwa ni bibi anapambana ada inalipwa na kodi ya chumba inalipwa pale inapopatikana.
Baba yangu amekuwa hajaniunga mkono kifedha kwa muda mrefu hata kuna wakati nilisikia ametumia zaidi ya milioni 2 kwa siku kwaajili ya kula kunywa na wanawake nisikumbukwe hata kwa elfu moja.
Ni miezi miwili imebaki nihitimu masomo yangu ya chuo na maandalizi ya kusherehekea mafanikio hayo kutimiza ndoto niliyokua nayo kwa mda mrefu.
Lakini napewa taarifa natakiwa niandike mahitaji yangu yote siku hio ya kusherehekea na baba yangu ambaye anajiandaa na safari kusherehekea pamoja na mimi na ndie atakaegharamikia kila kitu.
Bibi hajahafiki suala hilo ila wazazi walimuambia mimi ni mtu mzima natakiwa kuchagua mimi cha kufanya, bibi kanieleza hatokua msaada katika kusherehekea zaidi anashughulika na deni la ada ninalodaiwa pekee na mama pia hatokua msaada kwakua hana pesa yoyote.
Sina mpango wa kusherehekea mafanikio yangu siku itakapowadia ila nimechanganyikiwa sana na aina hii ya mahusiano ya wazazi hasa baba.
Ningependa kusikia maoni yenu na ushauri juu ya jinsi ya kushughulikia hali hii. Asanteni kwa msaada wenu."