Mahusiano ya kidugu ya Watanzania: Kanisa la kwanza Tanzania lilitolewa kiwanja na Waislamu

Mahusiano ya kidugu ya Watanzania: Kanisa la kwanza Tanzania lilitolewa kiwanja na Waislamu

Taso

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2010
Posts
2,507
Reaction score
2,412
Sio tu Tanzania, ni kanisa la kwanza Afrika Mashariki.

HOLY GHOST CHURCH
KANISA KATOLIKI
BAGAMOYO, TANZANIA

LILIJENGWA 1872

1629757697716.jpeg

Wakiongozwa na Sultan Majidd binafsi, Waislamu wa Bagamoyo waliwagawia kiwanja Wakristo wajenga kanisa mwaka 1868. Lilijengwa na wamishenari wa Kifaransa na kukamilika 1872.

Wamishenari hawa walikuwa na kampeni ya kupiga vita biashara ya utumwa kwa kutumia kanisa katika Afrika Mashariki.

Bagamoyo palikuwa kitovu cha biashara ya utumwa.
 
Nilienda hapo zamani kutembea ule mnyororo sijui umemezwa woote na ule mbuyu.
 
Hivi wakati ule kulikua na shida ya viwanja?

Ilikuaje Sultan Majidd aliyekua akiwauza Waislamu wa Bagamoyo aiachie biashara yake kirahisi hadi aamue kuwasaidia Wamishenari waliokuwa na kampeni ya kupiga vita biashara ya utumwa kwa kutumia kanisa?

Natamani kujua kama ni wakati ulifika au nini kilimfika Sultan
 
Sultan Sayyid Said wa Oman (aliyehamisha mji mkuu kutoka Oman kuja Zanzibar mnamo 1840) aliwahi kushirikiana na Waingereza waliomsaidia dhidi ya maadui Waarabu. 1845 alikubali madai ya Waingereza hataruhusu biashara ya watumwa nje ya Afrika ya Mashariki. (Wakati ule Uingereza ilijaribu kulazimisha nchi zote kuachana na kuchukua watumwa kutoka Afrika, kama maandalizi ya kukomesha utumwa mwenyewe).

Sayyid Said aliona faida kuwa na uhusiano mzuri na Wazungu uliomleta faida kubwa; Zanzibar ilikuwa haraka kitovu cha biashara ya kimataifa katika Afrika ya Mashariki. Hata hivyo, uchumi wa Sayyid Said ulitegemea kazi ya watumwa kutoka bara , pamoja na biashara ya watumwa kutoka bara hadi Unguja na Pemba. Lakini utumwa huo haukupingwa bado na Waingereza

Hao mapadre wa Roho Mtakatifu (Spiritan Fathers) alipokea vizuri maana alijua hao ni Wafaransa, Wafaransa na Waingereza si marafiki hivyo alitaka kuepukana kuwategemea Waingereza pekee. Aliwahi pia kufanya mkataba na Marekani.

Hivyo aliwaruhusu kuwa na kituo Zanzibar mjini mnamo 1860; 1868 aliwaruhusu kununua maeneo pale Bagamoyo kwa kusudi la kupokea watumwa waliokolewa kutoka meli na jahazi. Maana manowari wa Uingereza zilipitapita kwenye pwani za Afrika na kukamata jahazi ya watumwa zilizoelekea Uarabuni au kwenye visiwa vya Bahari Hindi. Watumwa walirudishwa kwenye nchi kavu na kwa kawaida kukabidhiwa kwa wamisionari. walioanzisha hivyo vijiji vya pekee (kama Rabai-Mombasa na kwanza Unguja, baadaye Bagamoyo). Maana Utumwa bado uliendelea na mtu bila ukoo kwenye pwani alikuwa hatarini kukamatwa na kuwa mtumwa tena.
 
Sultan Sayyid Said wa Oman (aliyehamisha mji mkuu kutoka Oman kuja Zanzibar mnamo 1840) aliwahi kushirikiana na Waingereza waliomsaidia dhidi ya maadui Waarabu. 1845 alikubali madai ya Waingereza hataruhusu biashara ya watumwa nje ya Afrika ya Mashariki. (Wakati ule Uingereza ilijaribu kulazimisha nchi zote kuachana na kuchukua watumwa kutoka Afrika, kama maandalizi ya kukomesha utumwa mwenyewe). Sayyid Said aliona faida kuwa na uhusiano mzuri na Wazungu uliomleta faida kubwa; Zanzibar ilikuwa haraka kitovu cha biashara ya kimataifa katika Afrika ya Mashariki. Hata hivyo, uchumi wa Sayyid Said ulitegemea kazi ya watumwa kutoka bara , pamoja na biashara ya watumwa kutoka bara hadi Unguja na Pemba. Lakini utumwa huo haukupingwa bado na Waingereza

Hao mapadre wa Roho Mtakatifu (Spiritan Fathers) alipokea vizuri maana alijua hao ni Wafaransa, Wafaransa na Waingereza si marafiki hivyo alitaka kuepukana kuwategemea Waingereza pekee. Aliwahi pia kufanya mkataba na MArekani.
Hivyo aliwaruhusu kuwa na kituo Zanzibar mjini mnamo 1860; 1868 aliwaruhusu kununua maeneo pale Bagamoyo kwa kusudi la kupokea watumwa waliokolewa kutoka meli na jahazi. Maana manowari wa Uingereza zilipitapita kwenye pwani za Afrika na kukamata jahazi ya watumwa zilizoelekea Uarabuni au kwenye visiwa vya Bahari Hindi. Watumwa walirudishwa kwenye nchi kavu na kwa kawaida kukabidhiwa kwa wamisionari. walioanzisha hivyo vijiji vya pekee (kama Rabai-Mombasa na kwanza Unguja, baadaye Bagamoyo). Maana Utumwa bado uliendelea na mtu bila ukoo kwenye pwani alikuwa hatarini kukamatwa na kuwa mtumwa tena.
🙏
 
Back
Top Bottom