Sultan Sayyid Said wa Oman (aliyehamisha mji mkuu kutoka Oman kuja Zanzibar mnamo 1840) aliwahi kushirikiana na Waingereza waliomsaidia dhidi ya maadui Waarabu. 1845 alikubali madai ya Waingereza hataruhusu biashara ya watumwa nje ya Afrika ya Mashariki. (Wakati ule Uingereza ilijaribu kulazimisha nchi zote kuachana na kuchukua watumwa kutoka Afrika, kama maandalizi ya kukomesha utumwa mwenyewe). Sayyid Said aliona faida kuwa na uhusiano mzuri na Wazungu uliomleta faida kubwa; Zanzibar ilikuwa haraka kitovu cha biashara ya kimataifa katika Afrika ya Mashariki. Hata hivyo, uchumi wa Sayyid Said ulitegemea kazi ya watumwa kutoka bara , pamoja na biashara ya watumwa kutoka bara hadi Unguja na Pemba. Lakini utumwa huo haukupingwa bado na Waingereza
Hao mapadre wa Roho Mtakatifu (Spiritan Fathers) alipokea vizuri maana alijua hao ni Wafaransa, Wafaransa na Waingereza si marafiki hivyo alitaka kuepukana kuwategemea Waingereza pekee. Aliwahi pia kufanya mkataba na MArekani.
Hivyo aliwaruhusu kuwa na kituo Zanzibar mjini mnamo 1860; 1868 aliwaruhusu kununua maeneo pale Bagamoyo kwa kusudi la kupokea watumwa waliokolewa kutoka meli na jahazi. Maana manowari wa Uingereza zilipitapita kwenye pwani za Afrika na kukamata jahazi ya watumwa zilizoelekea Uarabuni au kwenye visiwa vya Bahari Hindi. Watumwa walirudishwa kwenye nchi kavu na kwa kawaida kukabidhiwa kwa wamisionari. walioanzisha hivyo vijiji vya pekee (kama Rabai-Mombasa na kwanza Unguja, baadaye Bagamoyo). Maana Utumwa bado uliendelea na mtu bila ukoo kwenye pwani alikuwa hatarini kukamatwa na kuwa mtumwa tena.