Christopher Cyrilo
Member
- Oct 5, 2015
- 90
- 482
Hii ni sehemu ya pili katika muendelezo wa makala inayohusu uhusiano baina ya taifa tajiri na lenye nguvu duniani, Marekani na moja kati ya mataifa masikini duniani, Tanzania. Katika makala iliyopita niligusia kwa juujuu, maeneo ambayo uhusiano ulikuwa mzuri, hasa kwenye huduma za kijamii; Elimu, Afya na Mazingira. Niligusia pia maeneo ambayo mahusiano yalisuasua, ambayo ni maeneo ya ulinzi na usalama,na bila kusahau Intelijensia.
Bila shaka, Marekani walizidiwa nguvu na mahasimu wao wa Sovieti (Urusi) na Uchina katika kueneza itikadi zao, lakini hawakuacha kushirikiana na Tanzania katika maeneo meingine kama ilivyoelezwa hapo mwanzo. Kushindwa kwa Marekani katika kueneza itikadi ndani ya Tanzania kulichangiwa na uongozi wa Mwalimu Nyerere ambao uliegemea zaidi katika siasa za ujamaa, zenye mfanano na siasa za kikomunisti za Urusi na Uchina.
Katika Nyaraka za CIA zilizotolewa hadharani januari ya 2017, zinaeleza namna CIA walivyomtazama Nyerere kwa jicho hasi. Nyaraka hizo zinaonesha namna CIA walivyofuatilia kwa karibu uongozi wa Nyerere, na jinsi walivyotazama orodha ya watu wenye nafasi ya kumrithi ili kuwaingiza madarakani, ikibidi kwa kumpindua Mwalimu Nyerere. Hata Hivyo Rais aliyefuata, Ali Hassan Mwinyi, hakuwepo kwenye orodha hiyo ya CIA.
¶Misaada ya Marekani kwa Tanzania kupitia USAID|
Baadhi ya misaada ya kibinadamu waliotoa Marekani ni pamoja na kujenga Chuo cha Kilimo Morogoro(Morogoro Agricultural College) mwaka 1965, ambacho baadae mwaka 1984 kilitwa Sokoine University of Agriculture (SUA). Wakati huo, asilimia 90 ya watanzania walitegemea kilimo. Taasisi nyingine zilizojengwa na USAID ni pamoja na Chuo cha utumishi wa umma mjini Dar es Salaam, na vyuo vya elimu mjini Dar es Salaam na Iringa. Mwaka 1966 kwa niaba ya USAID, taasisi ya tafiti ya Stanford, ilifanya tathmini ya ujenzi wa barabara ya Tanzania hadi Zambia (TANZAM) na mwaka 1973 barabara hiyo ilikamilika.
Miaka ya 1970, USAID ilijikita zaidi katika ujenzi wa vituo vya afya hasa maeneo ya vijijini, pamoja na kutoa na mafunzo kwa wataalamu wa afya. Ujenzi wa barabara ya TANZAM ulilenga pamoja na mambo mengine, kuunganisha mikoa ya kusini na maeneo mengine ya nchi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na mawasiliano.
Miaka ya 1980, Majukumu ya USAID yaliongezeka baada ya kuingia kwa janga la UKIMWI. Ndipo ulipoanzishwa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Maambukizi ya UKIMWI/National AIDS Control Program (NACP) pamoja na kampeni za kutoa elimu dhidi ya ukimwi (EDU) na kusambaza kondomu bure.
Demokrasia na utawala bora pia vilianza kupewa kipaumbele miaka hiyo ya 1980 na kushika kasi miaka ya 1990. USAID ilishawishi serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi kuelekea mpango wa ugatuzi wa madaraka (Decentralization) na kurahisisha mifumo ya utawala vijijini, kisha mwaka 1995, USAID ilisaidia kuweka mipango ya ukusanyaji kodi, na kudhibiti upotevu wa mapato.
Mipango hiyo ilipelekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania/ Tanzania Revenue Authority iliyoanza kazi rasmi Julai 1, 1996 chini ya Rais mpya Benjamin William Mkapa. Wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa, uhusiano wa Marekani na Tanzania ulikuwa bora kuliko kipindi chochote nyuma, bila kusahau kwamba maboresho hayo yalianza kwa Rais aliyetangulia, Ali Hassan Mwinyi.
Mwaka 2003, mafanikio makubwa ya USAID yalionekana katika sekta ya afya baada ya kuanzishwa kwa mfuko wa dharura wa rais wa Marekani (President’s Emergence Plan for AIDS Relief (PEPFAR)). Mfuko huu unachangia asilimia 95 ya fedha za USAIDS katika miradi ya inayohusu VVU/UKIMWI nchini Tanzania. Miradi hii inahusisha matibabu na kujikinga na VVU, Ushauri nasaha na upimaji, elimu ya kujikinga na VVU kwa makundi yaliyo katika hatari ya maambukizi, matibabu ya kifua kikuu na tohara kwa wanaume.
Mwaka 2005, USAID ilianzisha mpango wa kudhibiti Malaria Tanzania bara na Visiwani. Kwa kushirikiana na mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria, pamoja na kituo cha kudhiti maradhi cha Marekani (CDC), USAID ilisambaza vyandarua milioni 5 nchini kote kwa mwaka 2006. Pia mpango huo ulihusiaha kufadhili filamu za kusaidia kutoa elimu dhidi ya malaria, mfano filamu ya CHUMO ya mwaka 2011 iliyowahusisha wasanii Hussein Mketi au Sharo Milionea (†), Jokate Mwegelo, Yusufu Mlela na Jafari Makati. Filamu hiyo iliongozwa na Jordan Rider ambaye ni mtoto wa John Rider aliyeongoza filamu maalufu ya Neria (1993).
Mpango wa kudhibiti malaria umesaidia kupunguza vifo vya watoto kwa asilimia 28 kwa kipindi cha mwaka 2006 hadi 2010. Kwa Zanzibar, mpango huo umepunguza kiwango cha Malaria na kufikia asilimia 1, karibu sawa na kutokomeza kabisa ugonjwa huo. Orodha ya misaada ya kibinadamu kutoka Marekani ni ndefu, lakini sio lengo la andiko hili kueleza wingi wa misaada kutoka Marekani, lakini baadae nitaeleza sababu za Marekani kutoa misaada katika nchi masikini ikiwemo Tanzania. Niharakishe tu kusema kuwa Marekani ndio nchi inayoongoza kutoa misaada ya kiuchumi na ulinzi.
Tangu mwaka 2005, nchi 92 duniani zimepokea misaada ya jumla ya dola bilioni 18.25 na nchi zingine 143 zimepokea misada ya jumla ya dola bilioni 18.23. Nchi masikini na zenye uchumi wa kati ndio hupokea misaada. Tanzania ipo nafasi ya nne katika kupokea misaada ya kiuchumi, ikitanguliwa na Afghanstan, Jordan na Kenya.
Marekani wanaitaja Tanzania kama mdau muhimu katika mashirikiano yake. Mwaka 2011 ulianzishwa mpango ulioitwa Feed the future, unaohusu utoaji wa misaada katika sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kuelimisha wakulima wadogowadogo, kuongeza soko la bidhaa za kilimo na kuongeza matumizi ya teknolojia ya kilimo kwa wakulima wadogo na wakubwa. Mipango mingine inayotarajiwa kuanzishwa ni ‘Power Africa’ na ‘Let Girls Learn’.
¶Mahusiano katika ulinzi, usalama na Intelijensia/Jicho la CIA ndani ya Tanzania|
Mambo mengi yalitokea katika kipindi cha mwishoni mwa miaka ya 1990 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kulitokea kifo cha msaidizi wa Osama bin Laden aliyeitwa Abu Ubayda Al-Banshiri (jina halisi; Ali Al-Amin Ali Al-Rashid) katika ajali ya MV bukoba huko Mwanza, Tanzania. Mtu huyu aliyekuwa wa pili mwenye nguvu katika Al Qaeda, alikuwa akifuatiliwa na mawakala wa CIA. Tanzania ilikuwa tayari inahifadhi magaidi bila kujua, na hivyo kuwa kituo cha operesheni za kijasusi za CIA.
Mara nyingi uwepo wa magaidi na majasusi wa nchi fulani katika nchi nyingine huwa siri. Na kwa hiyo watu hao huwa na shughuli za kuzugia, hasa shughuli za kidiplomasia. Wanaweza pia kuwa watumishi katika taasisi za umma au binafsi, au mashirika yasio ya kiserikali, au wafanyabiashara. Wanaweza pia kuwa makahaba (Mfano, wasichana 600 wa kitutsi waliotumwa Tanzania kuanzisha mahusiano ya kingono na viongozi wa kiserikali na bunge, ili maamuzi yao yasaidie sera za Rwanda. Uchina wamewahi kufanya hivyo dhidi ya Uingereza).
Kwa hivyo, linapokuja suala la mahusiano katika ulinzi na usalama, bila kusahau intelijensia, utaona kwamba Marekani ilifanya ushushushu kwa kipindi kirefu ndani ya Tanzania bila kushirikiana moja kwa moja na vyombo vya ulinzi na usalama. Moja kati ya mambo yaliyowaumiza kichwa CIA ni namna ya kumuendesha Mwalimu Nyerere vile wanavyotaka au ikibidi kumuondoa madarakani na kuweka mtu atakayekwenda sawa na sera za Marekani.
Pamoja na kuwa mtu aliyeheshimiwa Afrika na duniani, Nyerere aliandikwa kwa wino mwekundu katika kurasa za nyaraka za CIA. Watu ndani ya shirika hilo la kijasusi walimshangaa Nyerere mwenye elimu ya Magharibi lakini mwenye sera za kikomunisti. Mtazamo huo hasi wa CIA kwa Nyerere hauishii katika sera zake za kikomunisti na kijamaa, bali hata katika mapambano yake dhidi ya ukoloni kusini mwa Afrika. Nyerere aliruhusu Tanzania kuwa kambi la mafunzo kwa vikundi vya ukombozi kusini mwa Afrika.
Makundi hayo ni pamoja na ‘u-Mkhoto wa Sizwe’ la Afrika Kusini, lilokuwa kundi la kijeshi la chama cha ANC, dhidi ya sera za kibaguzi za Makaburu wa Afrika Kusini. Marekani haiukuwa ikipinga serikali ya makaburu. Ingawa CIA ilipenda kuona ukoloni unaondoka Afrika ili kurahisisha upatikanaji wa soko la bidhaa za Marekani, lakini walitafsiri kitendo cha Nyerere kuratibu mapambano ya kivita kama ‘Ushabiki uliopitiliza’/Fanatic. Kwa upande wake, Nyerere pia hakuwa na mtazamo chanya kwa wamarekani, pengine ni matokeo ya kazi ya wachina na warusi.
Inawezekana kwamba Nyerere alianza kuitazama Marekani kwa jicho hasi tangu yalipotokea mauaji ya rafiki yake, John F Kennedy mwaka 1963. Nyerere alilaani vikali mauaji ya Kennedy na tangu hapo alianza kupinga sera nyingi za mataifa ya magharibi.
Jambo lingine lilowaumiza vichwa majasusi wa CIA ni namna warusi na wachina walivyokita mizizi ndani ya Tanzania. China ilikuwa nchi ya kwanza kujenga ubalozi nchini Tanzania mara tu baada ya Tanzania kujipatia uhuru wake.
Julai 1971 CIA walifanya uchunguzi wa siri ndani ya jeshi la Tanzania na kugundua kuwa Uchina ndio iliongoza kuipatia Tanzania silaha za kivita, na kusaidia mafunzo ya kijeshi. Wachina walifanikiwa kutengeneza urafiki wa kufa na kuzikana na Mwalimu Nyerere hadi pale uhusiano wao ulipoingia dosari mwaka 1978. Mwaka huo, Nyerere alikataa mpango wa China wa kuisaidia waasi wa Angola kupitia Tanzania. Ndipo China ikaanza kupunguza misaada ya kijeshi nchini Tanzania. Miaka miwili nyuma, yaani 1976, China ilikuwa imekamilisha ujenzi wa reli ya Tanzania hadi Zambia (Tazara).
Kwa upande wao Urusi walisaidia uchumi na mafunzo kwa vikundi vya ukombozi kusini mwa Afrika. Warusi na Wachina waliifanya Tanzania kuwa kituo kikuu cha kufanya shughuli zao katika nchi za kusini mwa Afrika, kwa sababu ya ushawishi aliokuwa nawo Mwalimu Nyerere, na kwa sababu Tanzania ilikuwa kama kiranja wa nchi zingine kusini mwa Afrika.
Nyaraka nyingine zinaonesha namna CIA walivyoandaa orodha ya mtu wa kumrithi Mwalimu Nyerere endapo angestaafu au wangemuondoa.
Mwaka 1982,CIA ilichapisha nyaraka yenye kurasa 25 iliyoitwa “ Tanzania: Nyerere and Beyond (Tanzania: Wakati na baada ya Nyerere) ambayo iligusia uwezekano wa Nyerere kuondoka madarakani kwa hiari au kwa mapinduzi ya kijeshi. Taarifa hiyo ilisema; Nguvu ya Nyerere inapungua kutokana na serikali yake kushindwa kushughurikia changamoto nyingi za kiuchumi. Upinzani dhidi yake umeongezeka miongoni mwa Raia, maofisa wa jeshi na viongozi wa kiserikali. Nyaraka hiyo pia ilikuwa na orodha ya watu ambao wangeweza kumrithi Nyerere, lengo ni kuwafanyia upembuzi watu hao, na kuwavutia upande wa Marekani.
Orodha hiyo ilijumisha;
• Edward Sokoine aliyekuwa waziri mkuu mstaafu kabla ya kurejea tena.
• David Musuguri, aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.
• Kighoma Malima, aliyekuwa waziri wa mipango na uchumi.
• Paul Bomani, aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Marekani.
• Cleopa Msuya, aliyekuwa waziri mkuu.
• Benjamin Mkapa aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Canada.
•Joseph Butiku aliyekuwa msaidizi binafsi wa Rais Nyerere.
Hata hivyo, kwa mshangao wa CIA, mtu aliyemrithi Nyerere hakuwamo katika orodha yao, pengine kwa sababu Ali Hassan Mwinyi alikuwa makamu wa Rais wa muungano na pia Rais wa Zanzibar, kwahiyo isingetarajiwa aachie nafasi hasa ya Uongozi wa Zanzibar na kuwa Rais wa muungano kabla ya muda wake kwisha. Hata hivyo, inaonesha Nyerere hakupenda kurithiwa na Mwinyi, bali Salim Ahmed Salim ambaye pia hakuwamo katika orodha ya CIA.
Oktoba 1986, mwaka mmoja baada ya Nyerere kujiuzulu na nafasi yake kuchukuliwa na Ali Hassan Mwinyi, CIA walifanya uchunguzi na kugundua kuwa Nyerere bado ana nguvu na ushawishi ndani ya serikali, hata baada ya kung’oka madarakani.
Wakati wa uongozi wa Rais Mwinyi, Mahusiano ya Tanzania na Urusi katika ulinzi na usalama yalianza kupungua. Moja ya sababu zilizopelekea jambo hilo ni kupungua kwa ushawishi wa Tanzania kwa nchi za kusini mwa Afrika. Serikali ya Moscow iliona Tanzania ikipoteza nafasi yake kama kiranja katika umoja wa Afrika, na kwa hiyo ikapata mashaka ya kuendelea na mashirikiano. Sambamba na hilo, uchumi wa Urusi ulikuwa unayumba.
CIA walimuona Mwinyi kama kiongozi dhaifu, lakini walimpenda kwa sababu alianza kubadili mifumo ya kijamaa na kuachana na sera za azimio la Arusha. Mapendekezo ya CIA kwa serikali ya Marekani yalikuwa kuongeza misaada ya kiuchumi kwa serikali ya mwinyi, kuipatia mikopo kutoka Benki ya dunia na shirika la fedha duniani, IMF ili kumvuta zaidi upande wa magharibi.
CIA walifuatilia kila hatua ya Rais Mwinyi, kuanzia katikati ya mwaka 1986 katika matembezi yake ya kwanza mjini Nairobi kuonana na Rais Daniel Arap Moi na kuanzisha upya mashirikaino ya kibiashara yaliyozolota baada ya kuvunjika kwa Jumuia ya Afrika Mashariki. CIA pia waligundua kwamba kuna tatizo katika uhusiano wa Mwinyi na Nyerere. Mwinyi alikuwa mtiifu halisi kwa Nyerere lakini sera zake zilikuwa kinyume.
Moja kati ya migogoro mikubwa ya Mwinyi na Nyerere uliibuka baada ya Mwinyi kuwa mshirika wa Mobutu Sese Seko wakati Nyerere aliunga mkono vikundi vya kijeshi vilivyompinga Mobutu. Mwinyi aliona si vibaya kufanya biashara na Zaire endapo Tanzania ingenufaika. Kwa mujibu wa CIA, Ndani ya Tanzania kulikuwa na marais wawili, Nyerere alikuwa akiongoza na kuaminiwa zaidi hasa katika masuala ya sera za nje, huku mwinyi akiongoza kwa kivuli cha Nyerere na mara chache kufanya vile anavyotaka. Hilo lilikuwa tatizo.
Intelijensia ya Tanzania, tangu miaka ya 1960 hadi miaka ya 1980 ilikuwa mshirika wa karibu wa KGB (Shirika la kijasusi la Urusi) na washirika wengine; Ujerumani mashariki, Bulgaria, Cuba nk. Ushirikiano huo ulifanikiwa kuharibu mahusiano ya Tanzania na Marekani katika maeneo ya Ulinzi na Usalama, na diplomasia. Mbinu zilizotumika ni pamoja na kuratibu maandiko yanayochochea chuki dhidi ya Marekani katika magazeti na majarida ndani ya Tanzania, kuandaa misemo ya kuharibu sifa za Marekani na kuisambaza mitaani, pamoja na kusambaza kwa maofisa wa serikali ya Tanzania taarifa mbaya zinazohusu wanadiplomasia wa kimarekani waliopo nchini.
Hadi mwaka 1985, CIA hawakuona dalili za Intelijensia ya Tanzania kupunguza mashirikiano na KGB ya Urusi, pamoja na kwamba mashirikiano mengine kati ya Tanzania na Urusi yalikuwa yamepungua.
Kingunge Ngombale Mwiru, aliyekuwa kiongozi wa vijana wa CCM alionwa kama mtu muhimu katika ushirikiano wa CCM na Urusi. Kupitia yeye, majasusi wa KGB na maofisa wa Bulgaria waliweza kuandaa viongozi wa chama wenye mlengo wa kikomunisti, hasa kutoka katika umoja wa vijana na vyama vya wafanayakazi. Kwa mikakati ya KGB, Urusi iliweza kufadhili mikutano ya Chama, shughuli za maadhimisho, semina na matamasha ya filamu zenye mlengo wa kikomunisti kila mwaka. KGB walimpa Kingune jina la ‘Red Ideologue’ kutokana na itikadi zake kali za mlengo wa kushoto.
CIA waliamini kwamba Intelijensia ya Tanzania itaendelea kushirikiana na KGB kwa miaka kadhaa, ingawa kutokana na upembuzi wao, waliona mwisho wa mashirikiano hayo unakaribia, na kwa hiyo hawakuingilia. Pengine mashirikiano hayo yalikolezwa na misaada ya kielimu ambayo Tanzania ilipokea kutoka Urusi na washirika wake. Mathalani, hadi mwaka 1985, watanzania 3000 walikuwa wamepatiwa elimu ya juu kwa ufadhili, huko Urusi, Cuba, Romania, Hungary, Yougoslavia na Ujerumani mashariki. Hata hivyo utafiti wa CIA ulionesha kuwa hakuna mtanzania hata mmoja aliyesoma katika nchi hizo, aliyekuwa kwenye nafasi za juu za uongozi ndani ya serikali ya Tanzania na hata katika chama cha mapinduzi.
Viongozi wengi wa juu walikuwa na umri mkubwa, na walipata elimu ya magharibi wakati wa mkoloni na baadae kidogo. Wahitimu wengi kutoka Urusi na nchi zingine za kikomunisti walikuwa vijana, na kwa hiyo CIA waliona uwezekano wa vijana hao kushika madaraka baadae kidogo. Hatua zilipaswa kuchukuliwa kudhibiti uwezekano huo.
Itaendelea.