Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 31,009
- 60,629
Kuna kipindi nilikua naangalia mdada kamkuta mtu aliyebeba vitu kwa mikono yote miwili anasumbuka kufungua mlango, akafungua alafu akaufunga nyuma yake kana kwamba hakukua na mtu mwingine pale japo alimwona, anapenda kuchungulia chungulia (snooping around) vitu vya watu wengine akijua haonekani. Alipoulizwa ye ni mtu wa aina gani (kabla hajajua alikua anaangaliwa) akajibu mzuri na mstaarabu, baada ya kuonyeshwa video akaishia kulia huku akilalamika kwamba anajijua mwenyewe ni mtu mzuri na blah blah nyingine.
Wewe kama wewe unajichukualia ni mtu mzuri na mstaarabu kwa ndugu, jamaa,marafiki na hata watu wengine unaokutana nao?Unajitahidi kua mstaarabu hata kidogo au hujali?
Unadhani hao watu wakiulizwa kuhusu wewe wengi wao watajibu kwamba wewe ni mtu mzuri/mstaarabu au kinyume cha hapo?
Kama leo hii mtu angekurecord kwa siri wakaonyeshwa watu wasiokufahamu, unadhani wangesema nini kuhusu wewe?
Binafsi hua najitahidi kwa kiasi changu, hata kumshikia mtu aliyepo nyuma yangu mlango, kumuokotea kitu au kumwambia samahani nikimgonga. Na bahati nzuri na mie hua nafanyiwa, wiki hii tu nimedondosha vitu mara mbili nikaokotewa, kuna siku nilisahau kadi yangu ya benki dukani mtu akanikimbizia. . . vitu kama hivi hua vinanifanya nitabasamu hata kama sikua kwenye mood nzuri. Au rafiki anaekumbuka kukujulia hali siku ya pili baada ya kumwambia unaumwa, mtu anaekumbuka na kukumbusha mambo yako ya maana na vitu kama hivyo. It just makes me happy to know there are really nice, caring and decent people out there. I hope YOU are one of them.
Week end njema.