Mahusiano yanayokuja kwako huwa yana sababu maalumu.

Mahusiano yanayokuja kwako huwa yana sababu maalumu.

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Wengi huwa tunashindwa kulitambua hili, hasa pale tunapokuwa wapofu wa huko tuendako.

Ndipo wahenga wakaja na msemo, ukiona nyani mzee juwa amekwepa mishale mingi.

Ikitokea mtu amekuja kwako kimahusiano, mpokee vizuri na umjibu vizuri kama kuna kisababishi chochote kitakacho kwamisha mahusiano yenu yasiendelee. Ikiwa labda una mahusiano tayari n.k

Mfanye huyo mtu aondoke kwako kwa furaha, akijua kweli sababu ulizozitoa ni sahihi kwa yeye kutokuwa na wewe.

Pia msiwekeane uadui, zaidi tu ya kuwa marafiki wakawaida.

Mfano, Ijumaa nilitoka kwenye starehe zangu usiku ikanipelekea kulala mpaka saa nane mchana Jumamosi; simu niliweka mlio wa taratibu ili isinisumbue katika usingizi wangu.

Nashtuka usingizini, kuangalia kwenye simu nikakuta namba ya rafiki yangu wa zamani na za wengine wakiwa wamenitafuta.

Kuangalia kwenye ujumbe, kukawa na jumbe mbali mbali, mojawapo ni huyu rafiki yangu, ikieleza,''......nina hali mbaya sana nakuomba uje hospitali...... chumba namba.....''

Kukawa pia ujumbe mwingine kutoka kwenye namba nyingine, ambao ulikuwa unasisitiza hali ya huyo mgonjwa na kusisitiza zaidi niweze kufika, kwa sababu kwa sasa hawezi ata kuongea.

Nikatafakari sana, nikaona kwa sababu tunapigania uhai na si mahusiano, na uhai ni muhimu zaidi kwa sababu changamoto za kiafya zitamkuta kila mmoja hapa duniani, ikabidi nipige simu ili kupata uhakika zaidi kinachoendelea.

Simu ilipokelewa na mtu mwingine, na kunijulisha hali ya mgonjwa si nzuri. Wakanipa maelekezo, nami nikawajibu nitafika muda si mrefu ingawa kichwani nilikuwa siko vizuri kutokana na mkesha wa vinywaji kwa siku iliyopita.

Baada ya kujiandaa, ikabidi nielekee hospitali; baada ya kufika nikaulizia chumba husika, nikaelekezwa.

Kuingia ndani nikamkuta mgonjwa na dada mmoja hivi; mgonjwa alitabasamu sana baada ya kuniona, nikamshika shavuni kama mjuavyo tena wapenzi wakikutana huwa tuna salamu zetu.

Yule dada ndio akawa ananielezea hali ilivyokuwa, na wakati huo kuna vipimo vingine vilikuwa vinaendelea. Kutokana na ukubwa wa mwili, changamoto ilikuwa kwenye presha.

Akawa anaendelea kupata matibabu, baadaye doktari akafika akatuomba tutoke kidogo ili wafanye kazi yao.

Kwa mazingira ya hospitali yalikuwa yako vizuri na yanashawishi uendelee kuwepo, kwa sababu huduma zote muhimu zipo ndani ya chumba.

Kwa kuwa nilikuwa sijaenda na salio, ikabidi nitumie muda ule kuamisha salio kidogo kutoka bank kuja kwenye simu, ili angalau nami nitoe mchango wangu katika kupigania uhai wake.

Baada ya muda tukaruhusiwa kuingia ili kuendelea kuwa karibu na mgonjwa. Muda niliokuwa pale, afya ya mgonjwa ikaanza kuimarika taratibu, mara anyooshe mkono wake akitaka kunishika mkono n.k

Nilikaa kama masaa matatu hivi, ndipo baadaye nikaenda kwa daktari kuulizia gharama, ikabidi nilipe.

Wakati namuaga mgonjwa, na kuwajulisha nimelipa bili akajikuta analia kwa macho ya furaha.

kwa sasa anaendelea vizuri, na ameshatoka, na ameweza kuongea na kuniomba tuweze kuonana zaidi.

Hii inatafsiri, wapo watu wanaoweza kutenda matendo ya huruma ambapo kwa sasa huwezi kuwatambua, mpaka pale jambo litakapo kukuta.

Tupunguze mbwembwe.

 
Bado theme kamili sijaipata
Mpo kwenye mahusiano?
Au umewah kumkataa au kukataliwq?
 
Back
Top Bottom