upupu255
Senior Member
- Sep 4, 2024
- 119
- 144
Maimuna Pathan, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi, mapema jana Februari 27, 2025, amekabidhi kiasi cha shilingi milioni 2 kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi wa UWT Wilaya ya Liwale katika jitihada za kuhakikisha Watumishi wanaishi katika makazi bora.
Vilevile Mheshimiwa Pathan (Mb) akiwa sambamba na Mheshimiwa Tecla Ungele (Mb) wamekabidhi Majiko ya Gesi 68 kwa Wakazi wa Liwale ikiwa Sehemu ya Kuunga Mkono Jitihada Za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika kuhakikisha Watanzania wanatumia Nishati safi yakupikia na Kuondokana na Matumizi ya Mkaa ama Kuni ambapo kwa kiasi kikubwa yanaharibu Uoto wa Asili au uharibifu mkubwa wa maliasili ambapo zoeli hilo la makabidhiano limefanyika kwenye Baraza la UWT Liwale.
Ameshukuru kwa dhamana waliyompa na UWT Wilaya ya Liwale wanaendelea kumuunga mkono kwa kazi nzuri anazozifanya na kujitolea kwake kwa maslahi mapana ya Wanaliwale.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mheshimiwa Maimuna Pathan anajivunia ushirikiano wa karibu na Mbunge mwenzake wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi, MheshimiwaTecla Ungele, ambaye pia walishirikiana pamoja katika zoezi la kugawa mitungi ya gesi 68 kwa UWT Wilaya ya Liwale ili kuwezesha matumizi ya nishati safi.
Kwa upande wake, Bi. Anna Ndumbalo, Katibu wa UWT Wilaya ya Liwale, ametoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Maimuna Pathan mchango wake wa Milioni 2 kuwa utasaidia kumaliza ujenzi wa nyumba ya katibu na kusema kuwa bado wanahitaji nguvu za ziada kutoka kwa viongozi na wanaccm kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati.