Maisha baada ya kesi ya Mbowe. Nini kutiliwa maanani?

Maisha baada ya kesi ya Mbowe. Nini kutiliwa maanani?

DaudiAiko

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
372
Reaction score
310
Wanabodi,

Wanao fuatilia kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe lazima wana fahamu kwamba kuna kushinda na kushindwa. Kushinda kuna ashiria mambo mengi lakini kubwa kuliko lote ni kwamba serikali inafanya kila kilicho ndani ya uwezo wao kuzuia mikutano ya wapinzani ikiwemo mbinu wanazo zitumia kudai katiba mpya na tume huru.

Inawezekana kwamba wana CHADEMA wanakosea kwa mbinu wanazo tumia vile vile inawezekana serikali inakosea kwa njia inazo tumia kutatua tatizo hili. Kuna maswali mengi ya kujiuliza ikiwemo umuhimu wa serikali kuruhusu wapinzani kufanya shughuli zao za uenezi.

Ingawa sikubaliani na njia za kulalamika zinazo tumiwa na wana CHADEMA kudai katiba mpya na tume huru, nina amini kwamba serikali haitakiwi kuwa zuia kufanya shughuli zao za uenezi za kila siku.

Hata kama serikali inatumia vyombo vya usalama kulinda amani na utulivu, ni rahisi sana kwa yeyote kufahamu kwamba kwa kutumia vyombo viliopo, serikali inajihusisha kwa kiasi kikubwa na kampeni ndogo ndogo zinazo fanywa mara kwa mara kwa nia na madhumuni ya kuweza kuwafikia wananchi. Mazoezi ya pamoja yanayo fanywa na wana CHADEMA, mikutano ya ndani ya chama au mikutano inayofanywa mitandaoni haitakiwi kuwa tishio kwa chama tawala bali ni wito kwao kufanya kazi na kujiandaa kisiasa kwa miaka ijayo.

Mungu ni mwema, wakati wote
 
Mwenye ako na update ya kesi ya sabaya maana watanzania wameisahau kabisa
 
Wakati mwingine mnazungusha mno aisee na mizunguko inayofanya mada kuwa ngumu kueleweka.

CHADEMA wanakosea? Serikali wanakosea? Ya nini kuzunguka kote huko huku ikijulikana wapi palipo na shida!

Mbowe ashindwe kesi, kesi gani na kwa sheria gani? Unakokuita kushindwa kesi ni kutofuata sheria zilizopo, ambao huo ni uvunjifu wa sheria bila kujali nani anayefanya hivyo.

Angalia, usitegemee hali kuwa kama ulivyoizoea baada ya hapa, bila kujali Mbowe kashinda kesi au hakushinda kesi kwa hila. Usitegemee tena kwenda kupiga kura za mazingaombwe tena.
 
Back
Top Bottom