Maisha baada ya mfungo wa mwezi Ramadhan

Maisha baada ya mfungo wa mwezi Ramadhan

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari.

Ramadhan Kareem! Amani iwe nanyi nyote.

Ni imani watu walikuwa na mfungo wa Ramadhan wa kheri kabisa toka mwanzo hadi siku ya kesho tunategemea watamaliza na kheri pia.

Kipindi chote cha mfungo watu walikuwa wenye kujizuia na maovu kwa kadiri ya uwezo wa Mungu alivyomjalia mtu.

Uzinzi, ulevi pamoja na lugha chafu zilipungua kwa kiasi kikubwa watu walijitahidi kuacha kwa muda wote wa Ramadhan bila kujali dini.

Watu walitumia lugha nzuri kwa kila mtu aliyekutana naye.

Hivyo hivyo napenda kuwakumbusha maisha hayajabadilika tupo kwenye siku zile zile yaani tulivyokuwa tunaishi kipindi cha mfungo basi fanya vile vile hata baada ya mfungo.

Maisha baada ya mfungo wa Ramadhan haina maana ilikuwa ni mapumziko ya kutofanya mambo ya ajabu.

Ulivyokuwa unafanya kipindi hicho chote jitahidi kuishi tena vile vile kuna changamoto za maudhi ya watu ila kila siku jitahidi kutumia lugha nzuri/ kujizuia kutenda mabaya.

Swala la ulevi pia jitathimini kwa kina kama uliacha kipindi cha mfungo sasa kwanini baada ya mfungo uanze tena ulevi?

Kama ni majungu na uzinzi uliacha kipindi cha mfungo kwanini tena baada ya mfungo urudie kufanya mambo ambayo unajua hayafai hata kidogo?

Nawatakia sikukuu njema siku hiyo ya kesho/kesho kutwa.

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu
 
tunawatakia kila la heri ndugu zetu waislam kwa kumalizia mfungo, ni matumaini yetu kuwa mtayaishi yale yote mliyo jifunza wakati wa mwezi mtukufu.
 
Back
Top Bottom