Maisha bila Social Media yatawezekana?

Maisha bila Social Media yatawezekana?

TOHATO

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2016
Posts
1,336
Reaction score
4,653
Tangu tarehe 27/10/2020 Kilichokuwa kinaendelea ni kuminywa (kufungwa) kwa mitandao ya kijamii. Swala ambalo limehusishwa na uchaguzi kwa namna moja au nyingine.

Ila chaajabu ni kwamba hawajafungia Internet, maana yake ni kuwa waeza kutumia bando lako kwenye maswala mengine ila sio Social media yoyote ile ambako ndo sehemu Watanzania tulikuwa tukizitumia MB zetu katika mambo tofauti.

Umuhimu wa mitandao ya kijamii ni mkubwa sana hasa dunia ya leo. Kama sijakosea ni kwamba hata tajiri namba moja duniani utajiri wake kipindi cha corona umeongezeka maradufu kwaajili ya kuuza bidhaa mitandaoni.

Leo wako watakao ona watumiaji wa mitandao ya kijamii kama wafatiliaji umbea au wachochezi tuu kama wadaivyo ila ni swala ambalo hata aloko kijijini akilima vi maharage vyake ana adhirika,kwani kuanzia madalali,wauzaji wasambazaji wa production yake hutumia zaidi mitandao ya kijamii.

Staki kukuambia hebu kazunguke Kariakoo waulize ni kiasi gani wamepoteza tangu kuminywa kwa mitandao ya kijamii. Ila fikiria tuu hata wewe umepoteza ma ngapi ulokuwa wayapata kupitia social media.

Ni kweli tuna penda kulinda Amani ya nchi yetu ambayo wameona kubinya mitandao ya kijamii itazuiaya uvunjifu wa aman, ila ni lini mitandao hiyo ya kijamii ilishawahi sababisha hayo huku tukiwa tumeshapita baadhi ya uchaguzi na mitandao ya kijamii ikiwepo?

Kufunga mitandao ya kijamii huku tunajiunga vifurushi ambavyo wanatupa Data na hatuna sehemu pakutumia ina maana gani? Je, Mitandao ya simu wataturudishia Data zetu zilizopotea bila matumizi?

Au Ni kufunzana watanzania kuanza kuangalia video za ngono?(Maana huko ndo mahali waeza tumia MB zako kwa sasa)
Au tunaendelea kuhangaikia tumia VPN hadi lini wakati tunajinadi nchi niya amani na uhuru?

Katika hili halina u CCM au UCHADEMA, lina muumiza kila mmoja wetu. Muda ambao mitandao ya kijamii umefungwa umetosha waachie tu. Au ndo itaendelea hivyo tuanze maisha mengine mapya?

Ki ufupi mitandao ya kijamii inaumuhimu sana tofauti na hilo lengo moja ambalo Hatujawahi ona madhara yake hapo kabla.
 
Na mikoani tunatuma...Hawa watu ndio wameumia zaidi mpaka sasa.
Na mbaya imefungwa hali ya kuwa hakuna yoyote anaesema tumeiminya au kuifunga yaani mwendo wa kimya kimya.
 
Basi nilijua ni wapinzani tu ndio wamefungiwa ili wasihamasishe maandamano kumbe hadi watawala!!
Lol.
 
CHADEMA ndio wanateseka sisi CCM hatuteseki.

Lilisikika limsukule limoja kutoka lumumba
 
Back
Top Bottom