Maisha bila umasikini wa fikra

Maisha bila umasikini wa fikra

Jeef George

Member
Joined
Dec 7, 2019
Posts
47
Reaction score
60
Habari karibu katika andiko hili la story for change,Lenye kuhamasisha jamii kuelimisha na kubadili mitazamo hasi kuwa chanya yenye kuleta msukumo wa jamii iliyolala katika wimbi la umasikini na kuamka katika mafanikio ya utajiri na jamii yenye kipato.

Ndimi mwandishi wako Ndugu jeef george JF

Karibu na asante,Enenda nami hadi mwisho ujifunze uelimike na uhamasike.


Kila mtu huwa na malengo, kila mwenye malengo hutamani yafanikiwe. Hatahivyo watu wengi tunafeli kutimiza malengo haya.

Kwasasa duniani kitakwimu tupo watu billion 7.7

Asilimia 15 kati yetu ni wale wa uchumi wa kati, ambao maisha yao ni ya kawaida, wanaweza kupata mahitaji yote muhimu ya maisha huku asilimia 80 ya watu wote duniani ni maskini yaani wanategemea kufanya kazi na kupata fedha zinazoweza kuwakimu kwa siku au wanategemea msaada kutoka kwa serikali za nchi zao.

Fahamu tabia zinazopelekea umasikini.
IMG_20210923_050909_140.JPG

1. Kutumia muda mwingi kuangalia TV, sinema au tamthiliya

Dalili moja ya mtu kuwa masikini siku za mbeleni ni utaratibu wa kutumia muda mwingi kuangalia TV badala ya kufanya shughuli za kuingiza kipato au hata shughuli za ziada zenye kuongeza manufaa. Masaa hayo unaweza kuyatumia kufanya shughuli za kibunifu, na kuutengenezea thamani muda wako. kuangalia TV sio jambo baya lakini kutumia masaa mengi kuangalia TV, sinema au tamthiliya ni hasara.

2. Kununua chakula (Fast food)

Hii ni tabia nyingine ambayo ninaitaja ambayo kama hairekebishwi hupelekea umaskini. Kama haukumbuki ni lini ulipika mwenyewe nyumbani kwako kwasababu unanunua chakula wakati wote basi hiyo ni dalili mbaya.


Haya yote hupunguza ufanisi wa mtu kufanya kazi vizuri ili afanikiwe au afikie malengo yake. Madhara haya huathiri maeneo yote maisha, kiuchumi, kiakili, kijamii na hata kimahusiano.


3. Kuchelewa kuamka (uvivu)
Uvivu wako ni umasikini wako wa fikra na kutofikia malendo kwa sababu ya ulegevu wa kutimiza makusudio yako ya baadae .Miaka inakwenda uzee unafika na kwasababu tu hukutumia muda wa kutosha kama kijana awali ulipenda uvivu na kuangalia mambo yanayopoteza muda na wakati na hii ni kwasababu haukutumia vizuri muda wako wa ujana kufanya kazi na kuwekeza kwa ajili ya miaka ya mbeleni.

Ninaamini kuwa mtu kama Bill Gates, Elon Musk, Mark Zuckerberg na wengine, huamka mapema na kuanza kufanya kazi zao kwa bidii kila siku, sasa kama matajiri ambao utajiri wao ni endelevu, wanaona umuhimu wa kuamka mapema na kufanya kazi, vipi kuhusu kijana.

4. Kulaumu wengine kwa matatizo unayopitia

Wataalamu wa uchumi wanaeleza kuwa moja ya tabia zinazoweza kumfanya mtu awe maskini ni pamoja na kulaumu watu wengine kutokana na kutofanikiwa kwako.

Kuna msemo unaosema “Maisha ni jinsi unavyoamua kuyaona” hivyo kila jambo linaweza kuwa ni la manufaa kwako aidha liwe zuri au baya, kinafanya utofauti kati ya hayo mawili ni jinsi utakavyoamua kulichukulia.

Jambo baya likitokea, masikini huwa wahanga wa jambo hilo lakini matajiri hulitafakari, na kuangalia sababu halisi ya jambo hilo kutokea kisha kuhakikisha halitokei tena au likitokea haliwaathiri au hata kuhakikisha wanatumia fursa yoyote inayopatikana katika janga hilo ili kunufaika nalo.

5. Jifunze kuwekeza/kuweka akiba

Akiba ni jambo la msingi sana katika mapato yoyote yanayopatikana. Akiba ya pesa husaidia pindi likitokea tatizo, inaweza kuwa ugonjwa, safari ya dharura na kadhalika. Kama huna akiba likitokea tatizo itakubidi uuze mali yako yoyote au uchukue mkopo ili kutatua tatizo hilo.

Tofauti na kutokea kwa matatizo, kama umeweka akiba na ikatokea fursa ya wewe kutumia pesa ili kuingiza faida, utanufaika kuliko mtu asiye na akiba, na huo ndio uzuri wa kutunza akiba ya pesa.

6. Kufanya manunuzi yasiyo kwenye mpangilio.

Hii ni pamoja na kununua vitu ambavyo havikuwa kwenye bajeti au mpangilio. Kutokana na hili, wataalamu wanashauri kufanya manunuzi ukiwa tayari umeandika orodha ya vitu unavyotaka kununua na sio kwenda sokoni au dukani na kuangalia kilichopo ili ufanye manunuzi.

Pia ni kama kuchukua mkopo ili kununua vitu ambavyo havizalishi pesa, kama kuchukua mkopo kununua furniture za ndani, au gari la kutembelea na vinginevyo. hiyo ni hasara na hupelekea umasikini.

7. Kuzaa watoto wengi

Kama wewe ni kijana na una mpango wakuja kuwa na familia yenye watoto wengi, hakikisha hali yako ya uchumi iko imara kabla haujaanza kuzaa watoto hao.



Tajiri mkubwa duniani Bill gates ana watoto watatu, tajiri mwingine Warren Baffet ana watoto 3, Mark Zuckerberg ana watoto wawili, na kutokana na utajiri walionao, wanao uwezo wa kuwa na watoto zaidi ya watano.

8. Kutopima afya mara kwa mara


Inawezekana ukaona sio suala la msingi kupima afya mara kwa mara lakini hili ni suala la msingi kwa watu matajiri, kwani kuishi ukiwa na uhakika wa afya ndio msingi wa kuishi maisha ya mafanikio.

Kupima afya mara kwa mara kunasaidia kujua mapema kama una ugonjwa unaoanza mwilini mwako, hii ina faida kwani uwezekano wa kutibiwa na kupona kabisa kwa ugonjwa huo ni mkubwa zaidi lakini pia gharama utakazotumia kwa ajili ya matibabu zitakuwa nafuu kuliko ambazo zingetumika wakati ugonjwa umekuwa mkubwa.


9. Kutumia pesa kabla ya kuzipata

Kama una tabia ya kukopa pesa kipindi ambacho hauna pesa huku ukitarajia kuzilipa pindi utakapopata pesa, hiyo ni dalili ya umaskini kukunyemelea.


10. Kuwa na marafiki wasio na malengo makubwa

Marafiki huweza kukusaidia kufikia malengo yako uliyojiwekea, lakini pia huweza kufanya usifikie malengo yako hayo.

Ninakushauri kama unataka kufanikiwa hakikisha unatumia muda mwingi zaidi na marafiki ambao wana malengo makubwa ya maisha, wanawaza mambo chanya na sio mambo hasi muda wote, ambao wanakukumbusha kufanya vitu vya msingi.

Hii inaweza kuwa msaada wako kwa kutunza muda wako uliojipangia na, kutokata tamaa kwenye malengo yako ya baadae ulojiwekea.
Kuwa mbunifu zaidi, na hata kukukosoa kwa tabia ambazo zinarudisha nyumba maendeleo yako.



Nipende kukushukuru kwa kujifunza kusoma na kuelewa story for change yatupasa tubadilike kuachana na fikra mbaya zenye kuleta umasikini.

usisahau kunipigia kura asante🙏🙏🙏
 
Kwenye idadi ya watoto nakupinga wangapi wanawatoto wachache na ni maskini
 
kwa mtu mmoja, kupika ni gharama zaidi kuliko kununua
Sio kweli.

Inategemea na upishi wenyewe.

Fikiria ina Microwave, fridge na jiko la gas pekee. Hapa utakuwa umepunguza gharama kubwa sana za vyakula.

Ukipika wali, maharage, nyama, nk. Ukahifadhi kwenye fridge imepinguza gharama kubwa sana za kupika kila siku. Utatoka kazini na kupasha tu kwenye microwave dk 5 umekaa mezani unakula.

Ikiwa ni chai unatenga maji kwenye gas huku u aendelea na mambo mengine dakika 15 iko tayari unaendelea kunywa na mkate wako au mayai.

Usijiwekee mikingamo (limits) angalia kitu positively au mtizamo chanya utaona fursa
 
Kwenye idadi ya watoto nakupinga wangapi wanawatoto wachache na ni maskini
Kwenye hilo la watoto nakubaliana na wewe. Hata wengine hawana mtoto mmoja lakini maskini.

Umaskini wa mtu au utajiri upo kichwani hausabibishwi na wingi au uchache wa watoto.
 
Sio kweli.

Inategemea na upishi wenyewe.

Fikiria ina Microwave, fridge na jiko la gas pekee. Hapa utakuwa umepunguza gharama kubwa sana za vyakula.

Ukipika wali, maharage, nyama, nk. Ukahifadhi kwenye fridge imepinguza gharama kubwa sana za kupika kila siku. Utatoka kazini na kupasha tu kwenye microwave dk 5 umekaa mezani unakula.

Ikiwa ni chai unatenga maji kwenye gas huku u aendelea na mambo mengine dakika 15 iko tayari unaendelea kunywa na mkate wako au mayai.

Usijiwekee mikingamo (limits) angalia kitu positively au mtizamo chanya utaona fursa
umefikiria gharama za umeme na gesi bwashee ?
chakula cha microwave siyo fresh food
 
umefikiria gharama za umeme na gesi bwashee ?
chakula cha microwave siyo fresh food
Nikiwa naandika yote hayo nimeyawaza.

BTW unakwepa chakula cha microwave nyumbani kwako unaenda kula wali wa jana mgahawani. Kwa taarifa yako hakuna mfanyabiashara anatupa chakula (pesa au mtaji). Atakachofanya ni kukipasha au kukichanganya na alichopika leo. Hata kama ni hotel ya nyota 5. Mikate, maandazi, samaki, sosseji kuku choma au kaanga unaokula wote walio wengi sio fresh.

Ukiondoa huo ukungu kichwani unaokutanda usione gharama kubwa unayotumia kununua chakula mgahawani hauwezi kuelewa.

Kula kiporo cha nyumbani kwako kuliko kwenda kununua kiporo kwa gharama kubwa.

Unaongelea umeme na gas. Believe me, kama upo single gas ndogo utatumia miezi mitatu, kisha katika hiyo miezi mitatu matumizi ya umeme kwa microwave hayazidi elfu 5. Niambie sasa gharama inatoka wapi? Na bado unakula chakula kizuri sana.

Kwa ufupi sana. Mtoa mada kaleta huu uzi kusaidia wengi
 
Back
Top Bottom