Maisha Bora kwa kila Mtanzania; Bei ya Gas yapaa!

Ibrah

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2007
Posts
2,730
Reaction score
530
Wadau, jana nimeenda Orxy kununua gas ya kupikia (LPG) ya kilo 25. Nilipigwa na butwaa kukuta bei imepanda kutoka wastani wa 35,000/- hadi shs 40,000/-. Kwa kawaida mimi hutumia mtungi wa kilo 40 lakini kutokana na hali halisi ilibidi nikajaze mtungi wa kilo 25 ndipo nikakutana na mshangao huo!

Bei ya gas kwa kilo 38/40 sasa imefika shilingi 101,000/- kutoka shs 70,000/- mwaka 2006/07, shilingi 94,000/- mwaka 2009 na sasa shs 101,000/-. Hizi ni bei za Arusha/ Moshi.

Sijui wakati Rais wetu anaondoka mwaka 2015 (kama ataupata tena mwaka huu) atatuacha kwenye hali gani.
 
Umenishtua sana maana na mie gesi yangu home imeisha na mwezi huu umekaa vibaya sana. Duh! Mkaa nao uko juu vibaya sana, umeme thubutu kupikia utajuta kuzaliwa. Ama kweli haya maisha bora kwa mafisadi tu
 
Tutakuwa kama Nigeria ambako wanachimba mafuta lakini wananchi wanapanga foleni kupata mafuta!! Gas inachimbwa Songosongo wala hatuagizi toka nje inakuwaje bei yake inakuwa juu kiasi hicho kama sio ufisadi wa viongozi wetu? Tuliambiwa tukianza kutumia gas kuzalisha umeme bei ya nishati hiyo ingepungua lakini cha kushangaza tunaambiwa umeme unapandishwa bei!! Viongozi wetu mnatufikisha pabaya mahala ambapo maisha yetu hayatakuwa na maana na hapo ndio patakuwa hapatoshi na itabidi pachimbike!!
 
Tusubiri ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Hapo ndiyo Watanzania tutalia kilio cha kusaga na meno maana jamaa anajua atakuwa anamaliza awamu yake na atajaa kiburi cha hali ya juu huku hali ya maisha ya Watanzania walio wengi ikizidi kuwa ngumu. Si ajabu kabisa kukuta hii gas yetu kama inauzwa nchi za jirani huko bei inaweza kuwa poa sana ukilinganisha na Tanzania.
 
Hii gas ya kutoka Songosongo nayo bei kama hivyo? Sasa motisha wa kutumia rasilimali zetu uko wapi?
 
Tutakuwa kama Nigeria ambako wanachimba mafuta lakini wananchi wanapanga foleni kupata mafuta!! Gas inachimbwa Songosongo wala hatuagizi toka nje inakuwaje bei yake inakuwa juu kiasi hicho kama sio ufisadi wa viongozi wetu? Tuliambiwa tukianza kutumia gas kuzalisha umeme bei ya nishati hiyo ingepungua lakini cha kushangaza tunaambiwa umeme unapandishwa bei!! Viongozi wetu mnatufikisha pabaya mahala ambapo maisha yetu hayatakuwa na maana na hapo ndio patakuwa hapatoshi na itabidi pachimbike!!

Navyofahamu ni kwamba, gesi inayozalishwa songosongo haiuzwi kama wengi tunavyodhani. Gesi ya Oryx inatoka India. Ges ya songosongo inazalisha umeme. Sidhani kama inatumika kwa matumizi mengine zaidi ya hayo.

Ila kulikua na mpango mwingine wa kuchimba gesi ambayo ingetumika majumbani, ila sijajua umefikia wapi.

Kama nimekosea mahali, au nipo outdated, please correct me!
 
Back
Top Bottom