Maisha hapo awali katika Mars

Pindi mtakaposhituka mtakuja jua tu hakuna kitu inaitwa sayari yaani bali ni nyimbo tu za kijinga za kukaririshana majina ya miungu ya kiroma na kigiriki!
Na mkishituka vizuri mtajua tu zaidi kuwa hayo mashirika ya anga yote ni dini moja, nia Moja, kauli moja na msimamo mmoja kunidanganya mimi mjingamjinga hapa!!
 
Kwamba ibilisi anamtumia Elon kuandaa safari ya kurudi kwenye makazi yake huko Mars kabla Yesu hajatia maguu hapo Chato
 
Lakini tujiulize why safari ya Mars kwanini imeshupaliwa sana
huko watu wanaliwahi koloni jipya,kina Musk wanataka weka rekodi kua ni Binadamu wa kwanza kutua miguu Yao huko Ili kuweza legacy kubwa,ndio maaana utaona wameikamia hiyo shoo iwe jua iwe mvua,iwe Nuru iwe kiza!
 
Ko unataka kuniqmbia
Ko unataka kuniambia shetani hawezi kufika Mars bila vyombo vya wanaanga?
 
Ko unataka kuniqmbia

Ko unataka kuniambia shetani hawezi kufika Mars bila vyombo vya wanaanga?
Mkuu Kiko Jr, kutokana na maandiko hawezi kamwe kurudi huko bila ya msaada wa binadamu. Pengine labda turejee tena kupitia nukuu ya maandiko kama vile ifuatavyo;

UFUNUO WA YOHANA 12

8 Lakini joka hilo na malaika wake walishindwa, na hatimaye hapakuwa tena na nafasi mbinguni kwa ajili yao.

9 Basi, joka hilo kuu likatupwa nje. Joka hilo ndiye yule nyoka wa kale ambaye huitwa pia Ibilisi au Shetani ambaye huudanganya ulimwengu wote. Naam, alitupwa duniani, na malaika wake wote pamoja naye.
 
kwahiyo mkuu kwanini joka Ibilisi alitupwa Duniani na wakati sayari kibao zipo tupu,Yaani huyo Mungu alitutupia Hilo joka sehemu ambayo tunaishi halafu Hapo Hapo anataka tulishinde Ili Hali yeye lilimshinda huko Mbinguni?
Hivi huyo Mungu aliwaza Nini lakini?
 
Mungu alipowaumba malaika aliwapa uhuru wa kutambua mambo mema na mabaya. Na pia aliwapa uhuru wa kuchagua katika ya hayo mawili ili wapate kuthibitisha utii wao kwake. Pale ulipotokea uasi, sio kwamba Mungu alishindwa kumuangamiza Shetani mara moja, hakufanya hivyo kwa kuwa Yeye ni Mungu mwenye haki, alimfukuza mbinguni na kumweka kifungoni kwa muda hapa duniani, ili akapate kuidhihirisha haki hiyo.

Aidha, wengi wetu wanaweza kujiuliza ni kwa nini alifanya hivyo!? Ndiyo! Hakuwa na haraka ya kuwaangamiza wale malaika waasi, kwanza ili wapate muda wa kujutia uovu wao. Lakini pili, ilikuwa ni kutoa funzo kwa wale malaika watiifu waliobakia mbinguni wapate kushihudia athari za uasi, dhambi na kuthibitisha hukumu zake za haki.

Kwa hiyo basi kuumbwa kwa mwanadamu na kuwekwa duniani ilikuwa ni kama "case study" mbinguni juu ya uasi, dhambi na hukumu za haki. Mungu aliumba kiumbe kipya ambaye ni mwanadamu, na kukipa nafasi ya kuchagua kutenda mema na mabaya kama vile ambavyo ilivyokuwa kwao malaika. Kwa hiyo kumuumba mwanadamu kwa mfano wake, ni kwamba alimuumba ili apate utashi wa kuchagua jambo jema ama baya pasipo shurti yoyote ile, ili akapate kuuthibitisha utiifu wake kwake na kwa hiari yake yeye mwenyewe.

Ndiyo maana nukuu ya maandiko hueleza kama vile ifuatavyo;

MWANZO 1

26 Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.”

27 Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke.

Adamu aliumbwa kama kithibiti juu ya uasi na dhambi, lakini Eva aliumbwa kama "weak link" juu ya hayo. Dhambi haikutokea katika kipindi ambacho Adamu alikuwa akiishi peke yake, lakini alipokuja Eva ndipo majaribu yalifanikiwa na hatimaye kumuangusha mwanadamu dhambini.

Ndiyo maana ya uwepo wa mti ule wa ujuzi wa mambo mema na mabaya. Na ndio maana Mungu alipompa upenyo Ibilisi kuleta majaribu, aliweza kumlenga Eva na wala siyo Adam.

Labda tuyarejee kwa mara nyingine maandiko ili tuweze kupata tafakari kama ifuatavyo;

MWANZO 2

15 Basi, Mwenyezi-Mungu akamtwaa huyo mwanamume, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.

16 Mwenyezi-Mungu alimwamuru huyo mwanamume, “Waweza kula matunda ya mti wowote katika bustani;

17 lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usile, maana siku utakapokula matunda ya mti huo, hakika utakufa.”

Hii ndiyo maana ninasema ulikuwa ni "case study" ambayo kupitia kwayo malaika watiifu wameweza kujifunza kuhusu hukumu za haki zitakazo tolewa kwa wale malaika waovu.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Hoja yangu ni kwamba,mbona hua mnaaminisha watu ukiwa mbinguni hakuna ubaya Wala hakuna mawazo yoyote ya uasi ni sehemu unastarehe hakuna tabu wala shida yoyote,
Huyo shetani roho ya uasi aliipata wapi,Yaani imagine upo mbinguni na Mungu,Malaika,maserafi nk
Wamekuzunguka halafu unaamua uasi hiyo inawezekanaje Ina maana mbingu nayo si salama na huko muda wowote kinanuka kama Malaika wenyewe umesema wamepewa utashi wa kuchagua jema na Baya huoni siku ikifika binadamu tumefika huko na Kuna uwezekano wa tamaa za madaraka kutuingia tukapindua meza?
Nawaza Kwa sauti hapa!
 
Kwa hiyo kulikua na jeshi la ulinzi huko hata kabla ya Lucifer kuasi.

Lilikua la kazi gani? Huko mbinguni kulikua kuna security threats pia?
 
MATHAYO 24

(Marko 13:1-2; Luka 21:5-6)

1Yesu alitoka hekaluni, na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake walimwendea, wakamwonesha majengo ya hekalu.

2Yesu akawaambia, “Sawa, mnaweza kuyatazama haya yote! Kweli nawaambieni, hakuna hata jiwe moja litakalosalia hapa juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa

Angamizo lenye amri kutoka mbinguni hufuata kanuni hii. Mbali ya maji kukaushwa pia tunashuhudia hakuna jiwe linaonekana juu ya jiwe katika sura ya sayari hii. Tunaweza kupata sura halisi kupitia "link' ifuatayo;




Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Hata hujui unachosema wewe,we angalia hata ID yako,una matatizo ya kisaikolojia asilimia mia
 
Hata hujui unachosema wewe,we angalia hata ID yako,una matatizo ya kisaikolojia asilimia mia
Nyie ndio wale Aina ya Watu mmeathirika na propaganda za dini,umejuaje kama Nina Tatizo la saikolojia Ili Hali wewe Sio daktari uliyenifanyia uchunguzi na kugundua tatizo?
Usipende kuendesha mambo Yako Kwa hisia, jaribu kuendana na chunguzi + fact
Nadhani tumeelewana!
 
nilitegemea povu kutoka Kwa mpumbavu Mmoja kama wewe ambae umeshindwa kuthibitisha upumbavu wangu ulipo Ili Hali nawe ni mpumbavu usijua lolote zaidi ya kukariri hekaya za kiyahudi huko ukijiona mwerevu kumbe ni mpumbavu na Kwa upumbavu wako unadhani siyajui na siyaelewi mambo ya kipumbavu mnayoamini na Kwa taarifa Yako ewe mpumbavu najua nje ndani hayo mambo unayodhani Mimi ni mpumbavu kwayo,
Ila Kaa ukijua niliamua kuachana na upumbavu wa kuamini vitu vya kipumbavu ambavyo havina ushahidi zaidi ya hisia na so called Imani,
Pumbavu!
 
Ngoja nisubir jibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…