Bado tupo katika sayari ya Mars ambayo imekuwa ni kivutio kikubwa kwa sasa kuliko eneo lingine lolote lile katika anga za juu. Zipo sababu za jumla zinatolewa kuhusu hamasa hii kubwa. Katika sayari hii nyekundu ya Mirihi kunani kule?
Chombo cha uchunguzi cha ExoMars rover nacho kwa sasa kinatarajiwa kuondoka duniani mnamo tarehe 20-09-2022 na hatimaye kutarajiwa kutua katika Mars siku ya tarehe 10-06-2023. Chombo hiki kinasimamiwa na European Space Agency (ESA) kwa kushirikiana na Russian Space Agency (ROSCOSMOS) nacho pia kinatarajiwa kufanyia kazi uchunguzi wa hapo awali uliofanywa na chombo kingine cha ExoMars orbiter.
Uchaguzi wa ExoMars orbiter umebaini uwepo wa maji mengi yaliyoganda katika bonde kubwa la Valles Marineris lililopo katika sayari hii. Ushahidi wa kihistoria unaonyesha kuwa toka mwaka 1960 kuna jumla ya majaribio yapatayo 49 ambayo yamekwisha kufanyika ambapo miongoni mwa hayo, mashirika ya NASA ya USA na lile la China la CNSA ndiyo yameweza kufanikisha zoezi la vyombo vyao kutua katika ardhi ya sayari hii nyekundu.
Mashirika ya anga za juu ya nchi nyingi hapa duniani hivi sasa bado yanapigana vikumbo huko angani kwenda katika sayari hii kufanya uchunguzi. Mashirika kama lile la JAXA la Japan, Space X la USA, Canadian Space Agency, Italian Space Agency pamoja ISRO la India, yote yanaendelea na uchunguzi wa kisayansi katika sayari hii.
Hii ni miradi aghali mno na yenye kuhitaji uwekezaji wa fedha nyingi sana. Kwa nini iwe ni sayari hii tu na wala si nyingine yenye kuonyesha kuwa kivutio namna hii? Tajiri mwenye ukwasi mkubwa kuliko wote duniani, Elon Musk yeye ameahidi kupeleka watu kuishi katika sayari hii na hata kuigeuza kuwa koloni la dunia (lake binafsi!?). Huko mbeleni tutakuja kujua ni nani huyu Elon Musk, nini hasa anachokijua kuhusu siri iliyopo ndani ya sayari hii?
Kama ilivyokuwa ada hatuwezi kuangalia fununu za kihistoria zilizopo katika maandiko matakatifu na pia ushahidi uliopo katika mafundisho ya Ibilisi mwenyewe. Tukianza na Neno la Mungu tunapata tafakari ifuatayo;
A. Mafumbo ya Mungu
1 Wakorintho 2
10 Hayo ndiyo mambo Mungu aliyotufunulia kwa njia ya Roho wake. Maana Roho huchunguza kila kitu hata mafumbo ya Mungu.
11 Nani awezaye kujua mambo ya ndani ya mtu isipokuwa roho yake mtu huyo? Hali kadhalika, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.
B. Fumbo za Ibilisi
Ufunuo 2
24. Lakini nyinyi wengine mlioko huko Thiatira ambao hamfuati mafundisho yake Yezebeli na ambao hamkujifunza fumbo za Shetani, nawaambieni kwamba sitawapeni mzigo mwingine.
25. Lazima mzingatie yale mliyo nayo sasa mpaka nitakapokuja.
Tukienda katika elimu ya kipagani inavyozungumza juu ya Ibilisi tunaweza kupata jambo fulani la maana. Mathalani tukienda katika "Lucifer wiki" tunaweza kupata michango mbalimbali ya wale waliozitoa roho zao kwake.
Kupitia kwa hawa wenye kumsujudu Shetani tunaona ya kwamba kuna vitu muhimu sana ambavyo Ibilisi ataweza kuimiliki dunia yote kama yeye ndiye mungu kamili, navyo ni;
a) Pete yake maalum iliyotengezwa kwa vito vya thamani kubwa
b) Sarafu ya pentekoste (Pentecost coin)
c) Kurasa 10 zilizopotea katika biblia yake ya Codex Gigas zenye "paramount satanic pray"
d) Madini adimu yatayowezesha kufunguliwa kwa shimo la kuzimu (Rejea Ufunuo 9:1-11)
Ni kweli hapo awali shetani aliumbwa akiwa mwenye madaraka makubwa na aliishi katika maisha ya fahari kubwa sana. Tunaweza kuirejea nukuu ifuatayo kutoka katika maandiko matakatifu;
EZEKIELI 28
13 Ulikaa Edeni, bustani ya Mungu.
Ulipambwa kwa kila namna ya johari,
akiki, topazi, yaspi, zabarajadi, berili,
sardoniki, johari ya rangi ya samawati, almasi na zumaridi.
Ulikuwa na mapambo ya dhahabu.
Yote uliwekewa tayari siku ulipoumbwa.
14 Nilimteua malaika kukulinda,
uliishi katika mlima wangu mtakatifu
na kutembea juu ya vito vinavyometameta.
15 Uliishi maisha yasiyo na lawama,
tangu siku ile ulipoumbwa,
hadi ulipoanza kufanya uovu.
16 Ufanisi wa biashara yako
ulikujaza dhuluma, ukatenda dhambi.
Kwa hiyo nilikufukuza kama kinyaa,
mbali na mlima wangu mtakatifu.
Na yule malaika aliyekulinda
akakufukuzia mbali na vito vinavyometameta.
17 Ulikuwa na kiburi
kwa sababu ya uzuri wako.
Uliharibu hekima yako kwa sababu ya fahari yako.
Nilikubwaga chini udongoni,
nikakufanya kuwa kioja kwa wafalme.
Ipo sababu yenye kuamsha shahuku hii kubwa ya kwenda katika sayari hii nyekundu ya Mirihi. Lakini kubwa kuliko zote ni hiyo ya funguo za kuzimu kama inavyorejewa katika maandiko matakatifu;
Ufunuo wa Yohana 9
1 Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona bnyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.
2 Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.
Sent from my Nokia 2.3 using
JamiiForums mobile app