Tatizo la mambo kama haya, unaweza kutoa ushauri weeee, matokeo ukaonekana una wivu na maisha ya mtu (hata kama hamna hata hicho cha kuonea wivu!). Siku ya siku unawakuta pamoja wameshikana mikono na kapu, mkwara wanasindikizana sokoni!
Anyways kwa mimi kama Dina, tupa kule funga ukurasa, songa mbele. Siwezi kuwakatalia watoto kumlilia baba yao, kwani ni ukweli usiopingika kuwa ni baba yao. Angepata 'bingo' angerudi?