Maisha huko tuendako yatakuwa magumu mno. Tujipange

Maisha huko tuendako yatakuwa magumu mno. Tujipange

Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2022
Posts
1,726
Reaction score
3,391
Juzi hapa India imepiga marufuku kuuza mchele nje ya nchi yao. India ndiye muuzaji mkubwa wa mchele duniani. Nchi tatu zinazofuatia zikijulisha kiasi zinachouza bado hazifikii kiwango inachouza India. Pia ni muuzaji mkubwa wa ngano, hii alishapiga marufuku kuuza nje siku nyingi.

Matokeo yake mchele utapanda bei kupita kiasi maana wazalishaji wakubwa nao watafuata mfano wa India. watu watakimbilia nafaka mbadala kama ngano ambazo nazo zitapanda bei balaa.

Tujitahidi kununua chakula na kutunza. Tujitahidi kuanza kuzalisha chakula nyumbani, badala ya kupanda maua tupande nyanya chungu.
 
Juzi hapa India imepiga marufuku kuuza mchele nje ya nchi yao. India ndiye muuzaji mkubwa wa mchele duniani. Nchi tatu zinazofuatia zikijulisha kiasi zinachouza...
Huu muda ni wa kulala wewe bado huko jamvin unaposti mada za msosi. Hivi kama nchi tunaelekea wapi? Yani sisi ni taifa la kupenda na kuendekeza kula kula tu. Why?

Laleni bana!
 
Sio tuendako,mda huu ninapoandika hapa ukiza dola moja inauzwa kwa TZ tsh ngapi?.Yajayo yanafurahisha sana mana nchi imekua ya kibebari zaudi.Kunaibuka tabaka la matajiri mno na maskini wa kufa MTU.
Viongozi tunaowategemea wengivwao wanapiga pesa kutengeneza vizazi vyao.
Siasa imekua kama biashara zingine
 
Juzi hapa India imepiga marufuku kuuza mchele nje ya nchi yao. India ndiye muuzaji mkubwa wa mchele duniani. Nchi tatu zinazofuatia zikijulisha kiasi zinachouza bado hazifikii kiwango inachouza India. Pia ni muuzaji mkubwa wa ngano, hii alishapiga marufuku kuuza nje siku nyingi.

Matokeo yake mchele utapanda bei kupita kiasi maana wazalishaji wakubwa nao watafuata mfano wa India. watu watakimbilia nafaka mbadala kama ngano ambazo nazo zitapanda bei balaa.

Tujitahidi kununua chakula na kutunza. Tujitahidi kuanza kuzalisha chakula nyumbani, badala ya kupanda maua tupande nyanya chungu.
India inaongoza Kwa idadi ya watu Duniani Sasa ulitegemea nini? Hii ni fursa Kwa Tanzania

Mwisho hao wahindi tofauti na mchele hawali ugali kama Tanzania,aisee ngoja niongeze mashamba ya mpunga tutpiga pesa sana.

Bashe aliwaambia miaka 10 ijayo chakula ndio itakuwa biashara kubwa Duniani,saizi gunia la mahindi huku kwetu ni Kati ya 80,000-90,000 Mungu akupe nini? Samia 5 tena .
 
Mapori ni mengi,Hadi mna mapori ya akiba!shine amkeni mkalime mpunga
 
Back
Top Bottom