Maisha lazima yaendelee. Ni kauli za wafanyabiashara kwenye maghorofa mawili yaliyo pembeni ya lile lililoporomoka katika soko la Kariakoo ambao sasa wanaendelea na shughuli zao za kibiashara.
Majengo hayo mawili yalitakiwa kuchunguzwa usalama wake, mara baada ya ajali ya kuporomoka kwa jengo jirani na kusababisha vifo vya watu 29, majeruhi 88 na hasara ya mali.
Jengo la upande wa kulia katika harakati za uokoaji ndilo lilitobolewa matundu chini, yaliyotumiwa na waokoaji.