Maisha lazima yaendelee: Namna bora ya kujikinga na Corona katika ngazi ya familia

Maisha lazima yaendelee: Namna bora ya kujikinga na Corona katika ngazi ya familia

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
NAMNA FAMILIA ZINAVYOWEZA KUISHI HUKU ZIKIENDELA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA CORONAVIRUS

Kila mwanafamilia ana jukumu la kujilinda na kuwalinda watu wote kutokana na maambukizi ya CoronaVirus. Suala lolote la Kitaifa linaanzia kwenye ngazi ya familia kwa kila mmoja kuchukua tahadhari.

Kwa kipindi hiki ambacho shughuli zinarudi kufanyika kama awali, kila familia inahitaji kuwa na vifaa na vitu vingine vya muhimu katika kuendela kujikinga na virusi hivi
  • Dawa na boksi la huduma ya kwanza
Unashauriwa kuwa na dawa za kupunguza maumivu, dawa za vitamin C, kipima joto (Thermometer) na pia unashauriwa kunywa maji mara kwa mara. Kama ulikuwa kwenye dozi yoyote unashauriwa kuwa na dozi ya siku zisizopungua 30 ili kukusaidia kutotoka mara kwa mara nyumbani
  • Vifaa vya kufanyia usafi
Kila familia inashauriwa kuwa na vifaa vya kufanyiwa usafi (Disinfectant); Hizi hutumika kusafisha sehemu zinazoguswa mra kwa mara na watu. Mfano vitasa vya milango ya nyumba na magari (kama nyumbani kuna gari), viti, swichi za taa, karo la bafuni na chooni kwa ujumla

Pia, unashauriwa kuwa na ndoo (yenye koki) ya maji masafi nje ya nyumba, sabuni na tissue au kuwepo kwa sanitizer. Hizi zitasaidia katika kuhakikisha kuwa kila mtu anaporudi nyumbani kujisafisha mikono yake kabla ya kuingia ndani
  • Chakula
Matunda na mboga za majani ni muhimu kuwa navyo ndani; Ni muhimu kwasababu husaidia katika kuongeza vitamin na kusaidia kuimarisha kinga ya mwili. Kuwa na vyakula vya nafaka ndani na vyakula vilivyokaushwa; Kuwa na mahindi, unga wa mahindi, maharage, kunde na vyakula kama hivyi kukusaidia kutokwenda sokoni mara kwa mara. Kuwa na vyakula vilivyokaushwa kama samaki.

Kwa wenye uwezo wa kuwa na viungo vya kwenye makopo ni muhimu kuwa navyo. Nyanya, viungo vya mboga na vingine vinaweza kuwa kwenye makopo na kukaa kwa muda mrefu. Kama huwezi kuwa na viungo hivyo basi muda wa kwenda kununua nenda kwenye genge au soko lisilo na watu wengi

Wageni au Wapangaji wenza

Kitu muhimu cha kuzingatika katika familia na kuhakikisha kuwa kama inawezekana kutopokea wageni. Ugonjwa wa Corona unaweza usioneshe dalili hadi kwa siku 14. Kama inawezekana ni vizuri kutopokea wageni wapya nyumbani hadi hapo utakapokuwa na uhakika kuwa hakuna kabisa maambukizi ya Virusi vya Corona nchini

Ikiwa unakaa kwenye nyumba yenye wapangaji wengi kaa nao mbali (Wape nafasi) hususani pale mnapokutana kwa kusamiliana. Usipeane mikono, usiende ndani kwa mtu na usiruhusu mtu kuja ndani kwako. Hakikisha unajisafisha mikono kabla ya kuingia ndani mwako

Kutoka Nyumbani

Ushauri wa kwanza kutoka kwa Wataalamu ni kwamba usitoke nyumbani kama hauna shughuli ya msingi ya kufanya. Lakini tunajua kuwa familia zinahidaji kujiongeza kiuchumi kwa kutafuta riziki na katika kufanya hilo lazima mtu atoke. Kama ukitoka na kwenda uendako basi fanya haya;

  • Kwanza hakikisha umevaa barakoa (Mask) ukiwa unatoka; Hii itakusaidia kujinda wewe na kuwalinda wengine. Itakulinda pale mtu atakapokohoa karibu yako na pia itasaidia wengine wewe ukikohoa na wakati huo itakusaidia kuzia kujishika mdomo na pua
  • Unapokuwa nje epuka kutumia vidole au mikono. Mfano unapokuwa unafungua milango au kubonyeza kifute cha ‘lift’ au sehemu yoyote tumia sehemu nyingine ya mwili wako. Unaweza kutumia kiwiko, magoti au nako (Knuckles). Unaposhika kitasa unaweza kutumia glovu au unashauriwa kutumia sehemu ya nguo yako
  • Hakikisha unakwepa mikusanyiko katika sehemu za Umma, Wataalamu wanashauri kuweka umbali wa Mita 2 baina yako na wengine na hata kuiwa unaenda kupata huduma sehemu, benki, hospitali, au kwenye mall jitahidi kwenda muda ambao hauna watu wengi
  • Ukiwa nje ya nyumba angalia wapi unashika, wapi unaweka simu yako na hakikisha unaosha mikono kila baada ya muda kwa kutumia maji tiririka na sabuni au sanitizer ili kuwa salama pale utakapojisahau na kugusa macho
  • Ikiwa umetoka na hauna barakoa, ili kuwakinga wengine ukipiga chafya au kukohoa hakikisha unafanya hivyo kwa kujificha ndani ya kiwiko.
  • Jiwekee utaratibu wa kuwa na ‘napkins’ na tissue kwenye begi au kwenye mkoba wako kukusaidia katika kufungua vitu au kushika sehemu unazohitaji kushika

Kurudi nyumbani
  • Kitu cha kwanza kabisa baada ya kuwa umerudi nyumbani ni kusafisha mikono yako kwa maji tiririka na sabuni au kutumia sanitizer kabla ya kuingia ndani
  • Kwa kuwa unashauriwa ukitoka uwe umevaa barakoa, vua barakoa kwa kufuata miongozo na ushauri unaotolewa na Wataalamu na itupe vile inavyotakiwa
  • Unashauriwa kubadilisha nguo kwenye chumba kisicho na muingiliano na watu. Kisha oga kabla ya kukutana na wanafamilia wengine. Nguo ulizovua zinaweza kufuliwa kwa kutumia sabuni za kawaida za kufulia nguo. Usiweke nguo hizo sehemu ambapo kama zina virusi vinaweza kugusa nguo nyingine. Usivue nguo na kuikung’uta ili kupunguza kusambaza virusi
  • Tafuta sehemu ya kuweka vitu kama mikoba na mabegi, inaweza kuwa box kwa ajili ya kuvipulizia sanitizer baada ya kurudi nyumbani
  • Kifaa kama simu unaweza kukifuta kwa kutumia ‘sanitizer tissue’ au kutafuta kitambaa kisafi laini kisha kupulizie sanitizer na kufuta simu yako

Manunuzi

Kwa kipindi cha Corona watu wengi wamejikuta wakienda sokoni kununua vitu vya kukaa navyo ndani na wengine wanachukua tahadhari kwa kutokwenda sokoni na kuagiza vitu na kisha kuletewa wakiwa nyumbani.

Zifuatazo ni njia au namna nzuri ya kuweza visafisha vitu hivyo

Chakula

Kama ni chakula umeagiza na umeletewa, ondoa vifungashio vyote visivyo vya lazima na vitupe moja kwa moja kwenye kifaa cha uchafu. Kifaa cha uchafu kinatakiwa kiwe na mfuniko

Baada ya kuondoa vifungashio hivyo nawa mikono yako. Kama ni chakula kinachotakiwa kuliwa cha moto hakikisha umekipasha moto kisawasawa kabla ya kula.

Vyakula vilivyo kwenye makopo; safisha makopo hayo kwa kutumia sanitizer haitakuwa na madhara

Vyakula kama matunda na mboga za majani hakikisha umeviosha vizuri kwa maji tiririka kabla ya kuzihifadhi kwenye jokofu

Katika kuandaa chakula mara zote tumia chombo kisafi. Usisahau kunawa mikono baada na kabla ya kuanza kuandaa chakula. Tumia walau sekunde 20 kunawa

Vitu visivyo vya kula

Vitu vingine vyote ambavyo sio chakula na havipo kwenye mfumo wa maji maji au vipo kwenye maboksi vinaweza kupuliziwa sanitizer na kisha kuingizwa ndani
 
Upvote 0
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom