Maisha, Mapenzi na Utajiri wa Alikiba; Kuna mengi ya kujifunza

Traveller X

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2017
Posts
271
Reaction score
305

Naan kama ilivyo kwa wengine pia mimi ni mpenzi mkubwa sana wa BongoFlavor, Na leo nilikua nafatilia kwa kina kuhusu lifestyle ya mwanamuziki ALIKIBA ambae kwa kawaida ni ngumu kujua details zake kutokana na usiri wake, nilishawahi kuandika hapo nyuma kuhusiana na msanii DIAMOND PLATNUMZ maisha yake na mafanikio yake katika muziki, na leo nikashawishika kumfuatilia ALIKIBA na kusema ukweli kuna mengi ya kujifunza kupitia huyu bwana mdogo,

Melezo katika video

Alikiba pia ni moja ya wasanii wenye mkwanja mrefu kuliko boss wako (napendaga kusema hivyo) na mafanikio yake yalianza kuonekana kuanzia mwaka 2014 alipoamka rasmi na kurudi kwenye game kwa kishindo na ngoma yake ya "MWANA" hapo ndipo milango yake ya mafanikio ikaanza kufunguka na matuzo ya kila pembe ya dunia hii yakaanza kumsogelea, pia ni katika kipindi hichi alikiba alijizolea mamilioni ya mashabiki japo wengi wa mashabiki zake wamemfuata kutokana na chuki walizonazo kwa mpinzani wake, yani DIAMOND PLATNUMZ,

Mafanikio ya alikiba pia yaliongezewa nguvu na ile deal aliyopata ya kujiunga na label kubwa kabisa ya muziki duniani yani "SONY MUSIC" hakuna anaejua amechota kiasi gani katika deal hii lakini kwa hakika ni mpunga mrefu,

Maisha yake ya mapenzi wengi wanafahamu ana watoto wanne na inasemekana kila mtoto na mama yake

Sitaki kuweka maneno mengi lakini mwisho niseme tu inapendeza na kutia moyo kuona vijana wetu wanapata mafanikio makubwa kutokana na kazi zao inatia moyo sana ukilinganisha na kipindi cha nyuma, kwasasa mziki wa tanzania unazalisha mamilionea kila kukicha ni kitu kizuri sana
 
[emoji16][emoji16][emoji16] kweli kama ulivyoanza kwa kusema ngumu kupata details za huyo jamaa....matokeo yake hakuna jipya uliloandika kuhusu jamaa zaidi ya vile vile viduchu tunavyovijuaga...sema yooooow
 
Ali Kiba hiyo nyumba kaipata wapi? Msanini mwenye mjengo wa hivyo hapa Bongo ni Navy Kenzo.
 
Sauti anayo kwakweli ila pesa hana ana maisha ya kawaida anajidai hatak show off lkn kiukweli hajui kujiongeza pesa anayo simba mweny majumba yake Na kampuni inyosaidia wengi ...Sony nakaaya alienda,mwansiti,Rozi muhando na Davido aliyejitoa je walipata utajir kwa hawa Wa nyumbani?Yoooooo
 

kusema alikiba hanapesa uo ni uzushi tu, alikiba ana mamilio ya mashabiki wanaomsapoti kwenye kazi zake, kila siku ana fanya mashoo karibu kila kona ya dunia na ana mkataba na makampuni kibao sasa utasemaje hana pesa??
 
Kuimba anaimba pesa hakuna....hivi unaona chibu anavyositawi kajenga kwao,nyumba south,madale bado ana majumba mengine kibao hajayatangaza wanaishi wafanyakazi Wa WCB kiba ana nn yeye zaidi tu ya yooooooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…