SoC02 Maisha mapya ya Teknolojia

Stories of Change - 2022 Competition

Antonia lujabuka

New Member
Joined
Aug 20, 2022
Posts
2
Reaction score
0
MAISHA MAPYA YA TEKNOLOJIA

Daah!!! Alishtuka ghafla na kushika simu yake iliyoingia ujumbe ambao ulimpa mawazo na kumnyima usingizi, ilikuwa mida ya saa nane usiku. Ujumbe huo ulimueleza kuhusu kifaa chake kimoja kimekamatwa na kukipata kifaa chake inaweza kumgharimu pesa nyingi Sana na alisisitiziwa afanye kwa wakati akichelewa inaweza mpa hasara kampuni nzima kuteketea.

Mwanzo wa simulizi
Mwaka 1984, Jephoni alifanikiwa kuweza kumaliza masomo yake ya chuo kikuu ambayo alisomea masuala ya kompyuta. Alikuwa na umri wa miaka 27. Aliporejea nyumbani alipokelewa na mama yake pamoja na ndugu zake watatu ambao ni Jonson,Jeremi pamoja na Jestina ; wakiume wawili na wakike mmoja.

Jonsoni ambaye ni mdogo mtu walipishana miaka miwili ambaye alikuwa ni kijana wa vibarua apa na pale hakufanikiwa kusoma mpaka sekondari. Kipindi Hilo kilikuwa kigumu kwa mama yao kwa sababu kazi nyingi zilikuwa zinamuelemea mwenyewe na hakuweza kuajiri mtu wa kumsaidia kutokana na pesa ilikuwa haitoshi.

Kutokana na Hali ya nyumbani ilimpa mawazo Jephoni. Hivyo Jephoni kutokana na ujuzi alionao alipata wazo, Jephon alikuwa ni mtu wakutengeneza viroboti Kama umbo la mbwa na vilikuwa ni viroboti vidogo vidogo, vilikuwa vunafanya kazi Kama kumuamsha asubuhi, kumpatia taarifa ya mabadiliko ya Hali ya hewa. Alipata wazo jipya ambalo alihitaji alifanye ili kuweza kumsaidia familia na watu walio karibu pia.

Jephoni aliungana na mama ake katika kumsaidia uuzaji kwenye hoteli wakati huo Jephoni akilini aliwaza malengo yake lazima yatimie. Japo mama ake alifurahi kusaidiwa Ila hakufurahi kwa elimu aliyonayo Jephoni akae pale na kuhudumia hotelini. Hata ndugu zake walianza kumdharau Kaka yao kutokana na alichokuwa akifanya. Jephoni hakujali lolote linalotokea juu yake aliendelea kupiga kazi.

Ulipota miezi sita Jephoni alipata kiasi Cha pesa ambacho kilifikia robo ya like hitaji lake, alipata wazo la kwenda kukopa Benki na mashirika mbalimbali ili aweze kupata pesa ya mtaji. Alifanikiwa ndani ya miezi mitatu kupita na bila kupoteza muda Jephoni alianza kukununu vifaa pamoja na sehemu ya kufanya ufundi wake. Alianza kubuni maumbile mbalimbali ya roboti Kama watatu ambao aliwafanya kuwaongoza na kuwapa uwezo Kama ilivyo kompyuta inavyoweza kufanya kazi.

Ndani ya mwaka kupita Jephoni aliomba kibali Cha kutengeneza roboti na uuzaji nacho alifanikiwa, hayo yote yaliendelea Ila ndugu zake hawakujua kinachoendelea juu yake. Jephoni alifanikiwa kutangeneza na kuuza roboti wanne kutoka nje ya nchi jirani. Alipata pesa nyingine ya kujiendeleza na hivyo aliongeza idadi ya kutoa roboti nane nje ya nchi jirani.

Hivyo hakutaka iwe ni Siri yake maana maisha yake yalianza kubadilika hivyo alimwaminisha mama ake kwa mtengenezea roboti wawili ambao ni wa kumsaidia kazi pale hotelini. Mama alifurahi na hakuweza kuamini kilichotokea alimshukuru Sana Jephoni. Hapo ndipo Jonson nae alishuhudia pongezi zote zikienda kwa Kaka ake alijifanya nae Kama kafurahi lakini haikuwa Kama kafurahi alijiskia vibaya Sana maana bado anakinyongo kuwa Kaka ake kwa Nini amesomeshwa kwa gharama Sana kuzidi wao.

Mwaka 1986 , Jephoni alianza shughuli yake ya kuanzisha kampuni, aliwashirikisha pamoja na ndugu zake pamoja na viongozi baadhi wa nchi kwa sababu ilikuwa ni kampuni ambayo haijawahi tokea katika nchi yao. Ilitumia gharama nyingi na mda mrefu mpaka kufikia mwaka 1989 kampuni ikazinduliwa rasmi.

Kampuni iitwayo LOGIX ROBONEERS COMPANY. Ilikuwa chini ya Jephoni na kipindi chote hicho alitengeneza roboti ambae alikuwa ni Kama mfano wa binadamu na ndio alikuwa Chip Master. Alikuwa pamoja nae Kama mlinzi wake.

Jina la huo Chip Master alimwita Jephorea. Mda wote Jephoni na Jephorea walikuwa pamoja. Jephoni alimwekea Jephorea mitambo ambayo inamfanya Jephorea apate kumbukumbu na pia kumtambua mtu alivyo na anahitaji Nini asaidiwe.

LOGIX ROBONEERS COMPANY iliwasaidia watu wengi wenye uhitaji wa wafanya kazi katika mahotelini, viwandani, maofisini pia na hospitali mbalimbali. Jephorea pia alikuwa Mara nyingi akishinda katika ndani ya kampuni mida ya usiku kwa sababu ya ulinzi.

Jonson hakutaka yote Yale yampite aliwatuma vijana wake waende ndani ya kampuni ka kumchukua Jephorea. Jonsoni alijua mbinu zote za kumzima Jephorea hivyo walifanya. Hivyo Jonson alimtafuta Kaka ake usiku huo wa saa nane ili aweze kuntisha na kumpatia kiasi Cha pesa ili amrudishe Jephorea.

Daah!!! Alishtuka ghafla na kushika simu yake iliyoingia ujumbe ambao ulimpa mawazo na kumnyima usingizi, ilikuwa mida ya saa nane usiku. Ujumbe huo ulimueleza kuhusu kifaa chake kimoja kimekamatwa na kukipata kifaa chake inaweza kumgharimu pesa nyingi Sana na alisisitiziwa afanye kwa wakati akichelewa inaweza mpa hasara kampuni nzima kuteketea. Jephoni aliumia Sana aliwatafuta Tena na kuwahaidi anawapatia kiasi chochote Cha pesa wanacho taka Ila wasimfanye kitu Jephorea. Jonson aliona mishe yake imetiki bas aliendelea kuntisha Jephoni ili awahi.

Jephoni kwa kuwa alikuwa na mfumo mzima wa Jephoria katika kompyuta yake na hakuna mwingine anayeweza kumzima hivyo alicheki na kuona kwamba Jephorea yupo wapi na alimtambua Mdogo wake Jonson kuwa anahusika kwa kumteka Jephorea, hivyo alienda mpaka walipo bila ya wao kumwelikeza wajistaajabika Sana na Jonson alishikwa na aibu Sana, hivyo aliwahi kumwaomba Kaka ake msamaha nae Kaka ake hakuwa na neno Ila alimatia pesa Kama alivyohitaji ili nae akafanye shughuli zake na maisha yake.

Jephoni alimchukua Jephorea na kurudi nyumbani. Ilikuwa ni usiku wa maswali mengi kwa Jephoni Ila yote hakupata majibu kulikucha na maisha yaliendelea kawaida. Uuzaji wa roboti uliendelea na matajiri wengi waliona faida kubwa ya kuwa na roboti Mana chakula chake ni umeme, Wala haumwi, hafiwi, Hana ndugu wa kusalimia, haendi likizo, Hana hisia Kama kiburi, hasira. Roboti alikuwa na faida kubwa Sana. Na pia hoteli ya mama Jephoni ilikuwa Sana na waeja walikuwa wengi Sana na wengine walikuja kufurahia kutokana na vituko walivyokuwa walifanya maroboti.

Jephoni alifurahia maisha mapya ya teknolojia alipenda Sana maisha hayo mpaka kufikia mwaka 2021 umri wa Jephoni ulienda hivyo alikuwa na Jephorea karibu kwa ajili ya kumpatia huduma mbalimbali na familia yake, watoto, na wajukuu pia walipendezwa Sana na kufurahia maisha ya teknolojia.
 
Upvote 0
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…