Maisha na Bajeti

Maisha na Bajeti

Said Shagembe

Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
23
Reaction score
35
Katika jamii yetu kawaida ya watu wanashindwa kufikia malengo Yao kutokana na kile wanachoamini kuwa kipato hakitoshi.

Kiuhalisia ukimuuliza matumizi yake ni shi ngapi kwa mwezi au kwa siku hawezi kulipa jibu la moja kwa moja kwani wengine wao hutumia kulingana na kile anachokipata kwa siku hiyo. Yupo yule anaweza kujibana na kutumia 2000 kwa siku nzima na akatimiza Mahitaji yake, lakini huyo huyo kesho anaweza tumia mpaka 20000 kwa matumizi Yale Yale aliyotumia 2000 ikakidhi. Moja kwa moja hapa unagundua kuwa mtu anatumia kulingana na kile anachokipata.

Akipata 5000, hiyo hiyo itatosha matumizi. Akipata 7000 bado ataitumia yote kwa matumizi Yale Yale. Na ukiwa na hiyo tabia ni ngumu sana kuweza kuweka akiba kutokana na kutofanya mambo kwa Bajeti.


Wapo watu walikaa mitaani kabla ya kupata ajira na waliweza kuishi kwa 4000 wakiamini kuwa siku wakikaa kwenye system maisha yatakuwa mazuri kwani watakuwa na uhakika wa kipato Cha Kila mwezi. Ajabu wameingia kwenye system bado mambo ndo yamegoma kabsa licha ya kuwa na uhakika wa kipato Cha Kila mwezi.
Jibu hapa ni Moja tu, hatuna utamaduni wa kuishi kwa Bajeti ila tunatumia kulingana na kile tunachokipata.


Tuishini kwa kupangilia wa Bajeti na hakika hatutojutia kwa hela tunazopoteza kwa matumizi yasiyo ya msingi (yasiyo ya lazima)
 
Back
Top Bottom