0685377092
New Member
- Jul 28, 2022
- 1
- 0
Kwenye maisha kuna vitu vinakuja na kuondoka wakati tukiwa bado tunavihitaji, pia kuna wakati unapaswa kufanya maamuzi magumu kwa ajiri ya mtu mwingine, haijarishi yatakuathiri kiasi gani. Lakini hiyo ndio maana halisi ya maisha na utu.
Nitawapa kitu kilichotoka kwenye shajara yangu. Ilikuwa asubuhi nzuri sana! Nikiwa katika mizunguko yangu ya kila siku, nilikutana na kijana mmoja alikuwa mzuri sana alikuwa na asili kama ya kiarabu lakini hakuwa mwarabu. Tulianzisha urafiki mwisho wa siku tukaingia kwenye mahusiano.
Siku zilienda akaenda kunitambulisha kwao, walionekana watu wazuri niliwapenda kwasababu walikuwa wakarimu nilifurahi kupata wakwe wa namna hiyo.
Tukapanga twende kwetu pia wakamjue mpenzi wangu, kabla hatujaenda kwetu kuna kitu kikubwa kilitokea , ilikuwa asubuhi simu yangu iliita niliiangalia nikaikata kwasababu ilikuwa namba ngeni, nikatumiwa ujumbe "naomba unifungulie geti" ujumbe ulisomeka namna hiyo sikutaka kujiuliza ni nani katuma huo ujumbe nilienda moja kwa moja hadi getini na kufungua, nilistaajabu kuona mwanamke akiwa amesimama mbele yangu na alikuwa akilia sana ......sikutaka kumuuliza kwa wakati huo alikuwa akilia nini!
Nilimkaribisha ndani nikamtuliza akanyamaza ndio nikawa namuuliza amefuata nini kwangu na kwanini analia! Yule dada akasema Mimi naishi na mwanaume ambae ni mume wake wa ndoa, kiukweli nguvu ziliniisha akaendelea kusema kwamba mume wake amemtelekeza yeye na watoto, ameenda nyumbani kwa mama mkwe wake amefukuzwa kaambiwa kwamba hawamjui ukiangalia alikuwa akienda kila uzazi kwa mama mkwe lakini kafukuzwa.
Nilishikwa na hasira sana nikahisi kama yule dada katumwa nikamfukuza nikamwambie asije kwangu tena, yule mwanamke aliondoka nikachukua simu nikampigia mpenzi wangu alikuwa hapatikani kwa muda ule, nikampigia mama wa mpenzi wangu alipokea simu nikamuelezea kilichotokea yule mama akanijibu hata mimi nitaachwa tu! Kiukweli niliumia sana nikakosa hata nguvu ya kwenda kazini nikarudi kulala, jioni mwanaume akaja nikamfukuza nilimwambia simuhitaji kwenye maisha yangu arudi kwa mkewe. Kwenu wanawake Sikujua alienda kwa mkewe au kwa mama yake.
Niliumia sana kwasababu nilimpenda nilitumaini siku moja atakuwa mume wangu lakini niliona kama alikuwa mwanaume mwenye roho ya kishetani, kama aliweza kumuacha mkewe wa ndoa kwa kushirikiana na mama yake mzazi basi nilijua hata mimi ningeweza kuachwa muda wowote ndo maana niliamua kuondoa tatizo nyumbani kwangu, kwasababu yeye si baba Bora na hawezi kuwa baba watoto wangu.
Kwenu wanawake "ukiona mwenzako ananyolewa zako tia maji"maana yangu ni kwamba kuna baadhi ya wanaume wanashirikiana na wanawake wenzetu kuharibu ndoto za watu japo si wote wanashirikiana,hii kitu nimbaya sana iko zaidi ya ushirikina. Usifurahi kuwa na mme wa mtu ety oooh! Ananipenda ndio maana kamuacha mke wake, unajidanganya siku utakuja kutafuta mchawi wa ndoa yako na umkose, kwasababu hiyo taraka na wewe utapewa. Mwanaume aliyekamilika hawezi kuiacha familia yake ya mwanzo labla awe na mapepo tena mengi!
Furahia kuona mwanaume yuko na familia yake ya mwanzo na bado yuko na wewe Ina maana utakuwa na tumaini kubwa la kutokuacha hii ni kwa ndugu zangu waislamu kwa wakristo sidhani kama hichi kitu chapaswa kufanyika.
Kuna wakati wanawake tunaingia kwenye vitu vibaya kwa kuogopa maisha.maisha ni mepesi sana ukiamua kuishi maisha yako bila kuangalia maisha ya mtu mwingine lakini ni magumu ukiishi kwa kuyapenda maisha yako na kutamani maisha ya mtu mwingine. Kingine ni tamaa kwa sisi wanawake hatupaswi kuwa na tamaa tulizike na tulivyopewa Mwenyezi Mungu kwasababu mwisho wa siku tutakuja kutamani visivyotamanika. Ukiona mwanaume yuko na mke muheshimu kwasababu alimpenda mkewe ndio maana akamuoa kwahiyo hawezi kukupenda, lakini kuna baadhi ya watu wanashindwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa sababu ya kuzama pasipo sahihi.
Kwenu wanaume! Sio kwamba nataka kuwatukana lakini mmezidi, mmeshindwa kuamini kwamba wanawake wote wako sawa. Hampaswi kuhangaika kwasababu mihangaiko yenu inaharibu baadhi ya ndoto za watu, wanaume mmekosa mapenzi kama enzi za mababu zetu na mmeshindwa kuwa na hofu ya Mungu!
Sio wote lakini kuna baadhi yenu mmekuwa mashetani kwa kushindwa kudhibiti hisia za mwili hadi kupelekea kuharibu familia yenu. Ikumbukwe hakuna kitu Bora kama cha mwanzo hivyo acheni kabisa kuharibu vitu vya mwanzo kwasababu hicho ndo muhimu kuliko chochote, haribu kuzuia hisia za ovyo wahenga wanasema "viazi vilivyofunikwa vinaiva" achaneni na wavaa uchi kwasababu wamekosa maajabu.
Mtunzi: phoibemkwawi88@gmail.co
No:0685377092

Upvote
0