Maisha na uchumi

idiomer

Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
53
Reaction score
18
Uchumi na maisha

Utangulizi

Maisha ni kuzaliwa kukua kujifunza kuzeeka na hatimaye kufa. Sio kila mmoja wetu anapitia hatua hizi. Baadhi hufa kabla hata hawajaliwa. Wengine mara tu baada ya kuzaliwa. Kadhalika wengi huish kwa siku, wiki , miezi, miaka , muongo na hata karne. Maisha ni juhudi za moja kwa moja . Juhudi huweza kumnufaisha anayejibidisha au watoto wake. Chochote unachotumia leo ni juhudi za mtu fulani.

Uchumi hutekwa na wenye nguvu na dhaifu huwa tegemezi na ngumu tegemezi kuuteka uchumi. Je mtu anawezaje kuuteka uchumi wa eneo lake? Jibu ni kama ifuatavyo . Fursa nyingi huja kupitia kusoma sana. Mfano ili uweze kulima zao fulani lazima ujue taarifa za kukua kwa zao hilo sehemu fulani.

Uchumi na elimu
Elimu na uchumi ni sawa na mwanadamu na Pumzi kwan nii vitu viwili vinavyotembea sambamba. Ni jukumu letu sote kama wadau kuhakikisha kila kimoja kinaenda katika mihimili isiyopishana sana. Hivyo ningependa kutoa pendekezo au mawazo kuwa mda ambao wanafunzi wanasubiri matokeo ya kujiunga masomo endelevu ya kuvuka madaraja mfano likizo ya darasa la saba, likizo ya kumaliza kidato cha nne na cha sita zitumike kusoma kozi fupi kama Kompyuta au udereva. Hii itakua imewasaidia kupata ujuzi utakao wasaidia wakati wote. Na kwa jicho la pili itasaidia kuwaepusha vijana kujikita katika makundi hatarishi kama ulevi, Uvutaji wa bangi na wizi. Na kozi hizi fupi zinaweza kuwasaidia kujiingizia kipato apo badae.

Sheria na uchumi
Nchi inatakiwa kuweka mikakati, sheria na sera tofauti tofauti zitakazo hamasisha uwajibikaji katika Nchi hasa upande wa vijana kwani ndio nguvu kazi ya taifa ilipo. Mfano wa Sera kama "KIJANA CHANGAMKIA FURSA " au "KIJANA SHUPAVU NI MJASIRIAMALI" vinaweza kuwahamasisha vijana kujishughulisha na kujiajiri kuliko kusubiri ajira.Pia Nchi inaweza kuweka sheria ambazo zitamfanya kijana aweze kutumia mda wake vizuri.Mfano kijana akifikisha miaka 25 lazima awe na leseni ya udereva. Hii inaweza kusaidia kwani kuna kundi kubwa la vijana wanashindwa kufanya maamuzi sahihi kujifunza na kuishia kupoteza muda wake.

Haraka haraka haina baraka

Watu wengi hapa dunia tunataka kupata fedha kwa haraka. Mtu anataka kupata watu wanaomfuatilia kwenye mitandao ya kijamii wengi lakini hajui hatanufaika nao vipi. Mtu atafikiri njia fupi ni kununua akaunti ya mtu na kumlipa fedha. Hivyo atabadili jina mtu ataona gafla akaunti inaanza kuweka bidhaa ambazo mtumiaji wa awali alikuwa haweki. Hivyo mfuatiliaji au wengi wa wafuatiliaji walikuwa wanapenda jumbe za kumahaba na mtumiaji mpya anaweza matangazo ya biashara. Kwa mantiki hii biashara yake inaweza kuathiriwa kwa kuwa na wafuatiliaji wasiofurahishwa na jumbe na wengine huamua kuachana na akaunti hiyo.

Anza na kidogo

Jambo lolote zuri huanzia chini mtoto wako kama hafanyi vizuri ni wakati wa kuweka malengo na kuhakikisha kuwa matokeo yanapanda. Mfano badala ya kutoa adhabu kali unaweza kumwambia ukifaulu kwa daraja la kwanza hela ya matumiz shuleni kwa mwezi itapanda kutoka 20000/= hadi 30000/= . Hii inaweza kumchochea zaidi kufanya vizuri. Wazazi wengi wanaweka malengo yao makubwa na mazuri. Mfano mwaka huu hauishi kabla sijahamia kwenye nyumba yangu. Wazazi wengi wanashindwa kuwawekea watoto mipango na malengo toka mapema. Mtoto umleavyo ndio akuavyo.

Uchumi na ukuaji wa mtoto kielimu

Mtoto afundishwe uchumi akiwa mdogo hata kama uwezo mzazi anao. Mfano ukinunua umeme yuniti 14 kwa shilingi elfu tano (5000/=). Hivyo mtoto ajue yuniti moja ni shilingi ngapi na yuniti hizo 14 zinakaa kwa siku ngapi? Nyumbani ninatumia gesi muoneshe mtoto wakati umenunua na ni shilingi ngapi hivyo ikiisha ajue imetumika kwa siku ngapi na hivyo kwa siku mnatumia kiasi gani cha gesi. Hivi na vitu vingine vingi vitamfanya mtoto kupanuka kimawazo na kujua hisabati kujua namna ya kufikiri.

Mtoto mfano unamlipia ada mfano 70000 mwambie hii hela ni sawa na mbuzi mmoja na ukimfuga kwa miaka minne atakuwa ameleta faida. Hivyo basi hakikishwa unasoma kwa bidii ili Mungu akiachilia baraka zimwagike kwako. Ninataka matokeo ya kimwili, kiroho na kiakili.

Hitimisho

Maisha ni uchumi, hakuna kitu chochote hapa duniani kinafanikiwa bila uchumi. Lazima uweke mfumo mzuri wa kunufaika kiuchumi.

Mwl. Calvin Mmary

Mtaalam wa masuala ya Elimu.
 
Upvote 1
Sasa utashangaa kukuta mwalimu aliyeandika makala hii anavyochapika na maisha.

Bongo raha sana.πŸ˜€πŸ˜€
 
Sasa utashangaa kukuta mwalimu aliyeandika makala hii anavyochapika na maisha.

Bongo raha sana.πŸ˜€πŸ˜€
Naomba pigia kura andiko langu bonyeza alama ^ hii chini ya andiko
Ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…