Maisha ndo haya haya, tuache majivuno

ntuchake

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2024
Posts
408
Reaction score
1,549
Leo nimepokea kwa masikitiko habari za kufulia kwa mkaka niliyewahi kuwa nae kwenye uhusiano kwa muda wa miaka 3. Nasikia amefulia ameuza kila alichokuwa nacho amebaki na komwe lake tu. Huyu kaka alininyanyasa sana kipindi ana vijipesa mi nikiwa kajamba nani. Alininyanyasa kisaikolojia kuna baadhi ya vitu nikikumbuka hadi leo nakuwa mnyonge.

Kuna siku nilimnunulia zawadi akaniuliza bei ya zawadi nilivyomwambia bei yake akanijibu i dont use cheap things keep it for yourself 🥲

Siku anaachana na mimi akaniambia relationship yetu illkuwa just for fun nothing was serious and it wasnt even a relationship it was a situationship 🥲 Kumbuka hapo wakati anaongea haya tulikuwa pamoja kwa miaka 3. Halafu akaongeza nimekuwa nakuonesha signs zote za kutotaka kuendelea kuwa nawe lakini bado ukaendelea kuniganda. Naomba kuanzia leo usinitafute kwa namna yoyote ile its over!!

Katika maisha yangu yote hakuna kipindi moyo uliniuma kama siku ambayo alinitamkia maneno haya. Mungu si Athumani, sasa hivi amepigika maisha yanamnyoosha tu. Licha ya mambo yote aliyonifanyia nimesikitika sana. Mwanga wa Mungu umuangazie arudi katika hali yake ya zamani. Tuweni humble jamani maisha ndo haya haya tuache kudharau watu katika maisha haijalishi ni maisha ya kimapenzi au kikazi, hakuna mtu anayeijua kesho yake.

NB: Roby nitafute nikupe mchongo, mimi sina roho mbaya kama yako!
 
Falsafa ya mtu mweusi yaani ukipata matatizo wanakuja Kwa wingi tena watakaa muda mrefu sana kujifanya wanakupa pole, ukifanikiwa kuwazidi wala huoni wakija kujifunza zaidi watakupongeza kiaina kutoa lawama chap wanaondoka
 
Bila shaka ni mtu wa kanda ya ziwa huyo
 
Sasa huyo roby ndo yuko humu?

Pole sana cabo tumia akili siku nyingine Bufa usiendekeze hisia bro utakufa
 
Falsafa ya mtu mweusi yaani ukipata matatizo wanakuja Kwa wingi tena watakaa muda mrefu sana kujifanya wanakupa pole, ukifanikiwa kuwazidi wala huoni wakija kujifunza zaidi watakupongeza kiaina kutoa lawama chap wanaondoka
Mbona umeandika kinyume? Ukipata matatizo wanakimbia, huoni mtu. Ukipata wanakuja ''kukupongeza'' na kujifanya wako karibu na wewe. Utasikia wanasema ''ahaa, yule fulani mwenye mabasi ya kwenda Mwanza? Jamaa ni rafiki yangu sana yule'' Kumbe mlikutana siku moja tu bar mkapiga story za kusogeza muda.
 
Hata kama ni kuachana ila shombo hazifai. Anakula matunda ya tabia zake
 
Ukiwa na tatizo utapewa pole Kwa muda mrefu, ukifanya vizuri pongezi wanazitoa Kwa muda mfupi sana hii falsafa unaielewa lakini au
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…