Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Najaribu kupita mtaa kwa mtaa, sioni zile pukurushani za mwezi wa kumi na mbili, zile shamra shamra za maandalizi ya sikukuu, nyimbo hazipigwi, sijui tatizo ni nini?
Ninachoona tu, ni wazazi kupambana kununua madaftari, sare za shule, wengine wako kwenye foleni za kulipia ada za mwakani.
Wakati huko duniani, wako bize kwenye kupendezesha miji, kupamba miti ya sikukuu, wengine wanatoka sehemu moja hadi nyingine n.k, muhimu tu nafsi zao zifurahie mapumziko ya Disemba pamoja na sikukuu tarajiwa.
Sasa najiuliza, huu ubize wetu wa kupambana kipindi hiki cha maandalizi ya sikukuu, kwa kununua madaftari, sare za shule n.k na kuacha kufanya maandalizi ya sikukuu kama wengine huko Duniani, ina maana sisi tunajua sana elimu kuliko huko duniani?
Je hicho kinachotuweka bize, kimetusaidia kuvumbua nini kuliko wale wa huko duniani?
Cha kushangaza, huko duniani unakuta kijana wa miaka 16 anarusha ndege angani, je sisi kwa umri huo pamoja na ubize wetu anafanya nini?
Maisha ni haya haya, kuleni bata katika kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka.
Wazungu wanasema usiwe, 'busy for nothing'.