Maisha ni haya haya, kuleni bata katika kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Najaribu kupita mtaa kwa mtaa, sioni zile pukurushani za mwezi wa kumi na mbili, zile shamra shamra za maandalizi ya sikukuu, nyimbo hazipigwi, sijui tatizo ni nini?

Ninachoona tu, ni wazazi kupambana kununua madaftari, sare za shule, wengine wako kwenye foleni za kulipia ada za mwakani.

Wakati huko duniani, wako bize kwenye kupendezesha miji, kupamba miti ya sikukuu, wengine wanatoka sehemu moja hadi nyingine n.k, muhimu tu nafsi zao zifurahie mapumziko ya Disemba pamoja na sikukuu tarajiwa.

Sasa najiuliza, huu ubize wetu wa kupambana kipindi hiki cha maandalizi ya sikukuu, kwa kununua madaftari, sare za shule n.k na kuacha kufanya maandalizi ya sikukuu kama wengine huko Duniani, ina maana sisi tunajua sana elimu kuliko huko duniani?

Je hicho kinachotuweka bize, kimetusaidia kuvumbua nini kuliko wale wa huko duniani?

Cha kushangaza, huko duniani unakuta kijana wa miaka 16 anarusha ndege angani, je sisi kwa umri huo pamoja na ubize wetu anafanya nini?

Maisha ni haya haya, kuleni bata katika kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Wazungu wanasema usiwe, 'busy for nothing'.​
 
Kwa anayefuga na kulima, atasema; nyama nitatoa bandani/zizini, mchele nitatoa shambani, viungo nitatoa bustanini.
Sisi tulio ajiriwa tuna feli wapi?​
Mishahara mbuzi ,mbona mibwana midogo iko TANROAD na TRA tunaishi nayo inabadili magari tu na bata ndefuu.Tuongezeeni mishahara na posho muone vurugu zetu.
 
Njoo Arumeru huku kumeanza kunoga, tunapanda mitarakwa, unaijua?
 
Kwa anayefuga na kulima, atasema; nyama nitatoa bandani/zizini, mchele nitatoa shambani, viungo nitatoa bustanini.
Sisi tulio ajiriwa tuna feli wapi?​
Hakuna upumbavu sitaki kuusikia kama kilimo.Ufugaji naukubali sana.Nilishawahi kujaribu kulima matikiti nusu heka tu ,nikaambulia matiki nane tena madogooo kama nyanya chungu.Na hamu na kilimo mimi?! Nilikula za usooo.
 
Hakuna upumbavu sitaki kuusikia kama kilimo.Ufugaji naukubali sana.Nilishawahi kujaribu kulima matikiti nusu heka tu ,nikaambulia matiki nane tena madogooo kama nyanya chungu.Na hamu na kilimo mimi?! Nilikula za usooo.
Lakini kuna msemo usemao, mvumilivu hula mbivu.
 
Nyama sahii 12k ikija iyo day nahisi 15k na ushee πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸΏ uzuri fam inasepa Kijiji me ntakula kwa mama ashibae Cha buku jero imeisha iyo
Kwa mazingira hayo, ni bora kwenda kusherehekea kijijini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…