Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
Hata utumie huo muda kukaa na watoto!. subiri waanze kujitegemea utaona!Na mjipange kweli vinginevyo mjigawe, mtafute hela ya matumizi ya akiba ya baadae na utumie Muda wako wote wa ziada kujenga upendo kwa wanao ili Hata ukizeeka wakutunze au hata kukutembelea tuu na wajukuu.
Am ready..
.niko huku Iraq vitani my wife to be
Swaiba wangu Mpemba yeye aliondoka 1995 akiwa mkimbizi wa Tanzania kwa ticket ya CUF wakati ule upinzani unaanza. Alikwenda Scandinavia na mabinti wanne wakiwa chekechea wengine madarasa ya awali.Hata utumie huo muda kukaa na watoto!. subiri waanze kujitegemea utaona!
Wanakuja wanabeba mama yao motooo!
Kisha wanakuachia efu ishirini wanasepa!
Natafuta hela ujanani ili uzeeni niishi kama mfalme bila kutegemea mfuko wa mtu.
ntakuwa mzee kapuya wa pili full kujibinyia vitoto vibichi vibichi
Ni kweli miaka ya zamani ilikuwa Baba anaheshimika sana.Swaiba wangu Mpemba yeye aliondoka 1995 akiwa mkimbizi wa Tanzania kwa ticket ya CUF wakati ule upinzani unaanza. Alikwenda Scandinavia na mabinti wanne wakiwa chekechea wengine madarasa ya awali.
Wale watoto wanafanya kazi prodlfessinal sasa na wanamkumbuka Baba yao Pemba kwani alirudi. Anaishi vizuri kabisa. Inategemea ulivyo walea.
Daah sisi wenye watoto wa kiume tupu imekula kwetu. Ngoja nianze kukamilisha lodge yangu ili nikistaafu niwe nafyonza mdogo mdogo.Ni kweli miaka ya zamani ilikuwa Baba anaheshimika sana.
Ila sasa hivi Mama anaangaliwa sana.
Iko hivi watoto wa kike si rahisi kuwaacha baba zao.
Ila watoto wa kiume sio rahisi kuwaacha Mama zao. Mtazamo tuu
Kwetu wa Africa watoto ni kama investment,
Sifahamu nianzie wapi na habari hii. Tulipokuwa wadogo jirani yetu alikuwa mama mrembo tukizoea kumwita auntie. Auntie alikuwa mzaliwa wa mikoa yenye wanawake warembo. Auntie aliumbika, alikuwa na miguu chupa ya bia, rangi ya chungwa na hakuwa mfupi wala hakuwa super tall.
Auntie aliishi kwenye nyumba ya msajili lakini hakuwa na kazi. Alikuwa mchepuko wa mzee mmoja maarufu na tajiri sana wa enzi hizo Mhindi. Mhindi huyu aliishi Masaki na familia yake, pale kwa auntie alionekana kwa nadra sana.
Mara nyingi auntie akiwa mpweke alituita watoto twende kwake. Nyumba ilikuwa safi na nadhifu, tulipenda sana kwenda kwa auntie. Enzi zile za ujamaa TV hazikuruhusiwa lakini auntie alikuwa na TV ya black and white, alikuwa na deck tuliona cartoon za Tommy and Jerry.
Auntie alikuwa anakwenda Nairobi shopping kila baada ya miezi mitatu, alirudi na sabuni, dawa za meno, mafuta ya kula na ya kujipaka. Sisi tulifurahia BigG na Cadbury chocolates wakati wazazi walipewa dawa za meno na mafuta. Hizi ni zile enzi uhusiano wetu na Kenya ulivunjika na mipaka kufungwa.
Yule mzee wa Kihindi alifariki, na pale ilikuwa ni siri yake. Wakati huo tukiwa boarding tuliambiwa auntie alishindwa kuishi pale ilibidi ahame. Baadae tulisikia auntie alishindwa kabisa kumudu maisha utu uzimani. Watoto aliotulea tulijikusanya na kumsaidia. Tulimudu kumlipia kodi na hela ya kula. Utu uzima ulivyozidi aliamua kurudi kwao lakini auntie alitusisitiza tuwe na familia, Alisema watoto ndiyo urithi mkubwa duniani.
Sio mtazamo ndio hali halisi mzee baba. Ukizaa majike katika uzao wako shukuru maana wakiwa na akili ukubwani kwao utakuwa umeula.Ni kweli miaka ya zamani ilikuwa Baba anaheshimika sana.
Ila sasa hivi Mama anaangaliwa sana.
Iko hivi watoto wa kike si rahisi kuwaacha baba zao.
Ila watoto wa kiume sio rahisi kuwaacha Mama zao. Mtazamo tuu
Hahahah tatizo vidume wanaenda kuoa so ratiba inakuwa mama na mke wake. Mzee baba utasugua kama baba Platinumz omba mama yao asije akakupakazia tu!Daah sisi wenye watoto wa kiume tupu imekula kwetu. Ngoja nianze kukamilisha lodge yangu ili nikistaafu niwe nafyonza mdogo mdogo.
Asikudanganye mtu,mtoto ndio kila kitu! Hata kama dunia nzima itakutenga ila mtoto au watoto wako hawatokutupa kamwe!Kuna waswahili watakwambia kuzaa si kupata....
Siku zote namuomba mungu pamoja na vyote nilivyonavyo anipe uzee mwema unikute nikiwa na haiba kama niliyonayo sasa.
Siijui kesho yangu japo naindaa na kujipa moyo itakuwa kama nilivyopanga.
Alamsiki.
Asikudanganye mtu,mtoto ndio kila kitu! Hata kama dunia nzima itakutenga ila mtoto au watoto wako hawatokutupa kamwe!
Pole bibi