Mamshungulii
Senior Member
- May 3, 2023
- 175
- 88
Kama mtu anavyofikiri, ndivyo mtu anakuwa, ni methali ulimwenguni na ni halisi kabisa
Wakati fulani hivi umeme ukikatika jijini kwetu , kwa hiyo kama kawaida jambo la kwanza lilikuwa kutafuta mishumaa.
Tunamshukuru Mungu kwa uwepo wa mishumaa mara zote dharura ya umeme hutokea. kwa kunyata nikiwa peku kuelekea kwenye chumba cha kuhifadhia vitu, nilikuwa nikishangaa tu jinsi watu wasioona wanavyoweza kuishi na kumudu na kuongoza taasisi zao huku ni vipofu kama wa TLB(Tanzania league of Blind) na TAB(Tanzania Association for Blind ) au yule aliyegundua maandishi ya watu wasiiona ilhali naye akiwa haoni mpaka sasa anaenziwa duniani kila mwaka kwa kutumia jina lake (BRAILLE DAY).
Kama nilivyoelekezwa nilikuta mshumaa ukiwa mahali pazuri pamoja na kiberiti, nilitabasamu kwamba watu nyumbani kwangu wanafanya kazi kwa weledi.
Tulipowasha mshumaa ,huku tukila chakula cha jioni, mwangaza wa mshumaa ulitufanya tuweze kuona kivuli kikubwa pembeni ya meza ya kulia chakula.Tukila chakula tulijikuta tukitengeneza mikao tofauti ya mikono iliyotuonyesha kama wanyama tofauti ukutani kwa sababu ya mwanga wa mishumaa.
Baada ya kumaliza kula sikuwa na lakufanya sababu umeme ulikatika, na tumezoea sana teknolojia, nilikaa kwenye sofa langu nikiwaza na kuwazua nikapata wazo la kuandika mawazo yangu kwakutumia mwanga wa mshumaa, mawazo yalikuwa namna mshumaa huja akilini endapo umeme hukatika ,vivyohivyo maishani huwa tunakumbuka watu pale tu wanapohitajika .
Katikati wanasahaulika/kupuuzwa kwa mema yao tunasahau hata kuwapongeza/kuwatambua au kuwatangaza bali tunatangaza mabaya na maovu ya watu hao na kuyaenzi mabaya hayo. katika maisha tunakutana na viumbe wengi, tunaingia kwenye mahusiano tofauti, watu wengi wanatugusa, na wachache tunaleta mabadiliko ,maisha yanasonga lakini mahusiano hayo na kumbukumbu bado zipo mahali fulani na tunafufua tu ikiwa tunazihitaji .
Kwanini waandishi wa habari hutangaza sana mabaya na badala yake kuacha kutangaza mazuri na watu ambao wameleta mabadiliko bora katika maisha yetu, kama vile mshumaa huu unaoleta mwangaza wakati unahitajika zaidi.
Kwanini tunasahau umuhimu wao na jukumu lao katika maisha yetu .Wanaweza kuwa marafiki wetu wa chuokikuu, walimu, maprofesa, wauguzi, wanasheria, na jamaa wa mbali katika sehemu yetu ya asili ambapo tumeishi utoto wetu, mahali tulipohamishwa,tulipofanyia kazi au kutembelea wakati wa maisha yetu ya kibinadamu .
Orodhesha majina ya watu kama hao, wapigie wasiliana nao,wapongeze ,watambue,wapandishe vyeo,waongezee tija katika maisha yao .
Huwezi kujua wanakusubiri au wito wako wa kuhamasishwa na mabadiliko ungeleta hamasa kwa wengine. Tunaposhiriki kuigusa mioyo ya wengine uchanya unatawala. na maisha huanza kupata maana yake .Lakini wakati tunapogusa mioyo ya wengine kwa mazuri ndio wakati tunapoanza kuishi.
Asubuhi na mapema majira ya baridi, nikiwa nimemaliza kumwagilia miti na kukaa kwenye bustani yangu nikipumzika, nikaona uso ninaoufahamu, alikuwa mwalimu wangu wa zamani wa masomo niliyemuona baada ya miaka 45. Alikuwa akinifundisha tangu nikiwa na miaka 4 na amekuwa sehemu ya familia kama alivyokuwa akija hakuwahi kuacha na kila siku kwa masomo tofauti anawafundisha sasa wajukuu wangu.
Kwa kuwa nilikuwa na muda na wazo zuri kama hilo nikaanza kuliandika kwamba jinsi uhusiano fulani unavyokuja katika maisha yako unakuwa wa umuhimu sana lakini baada ya miaka michache auhitajiki hata kidogo au unaweza ukauhitaji kwa ajili ya maisha ya watu wengine au maisha yako.Inatokea hata kwamba uhusiano au mtu ambaye hatukuwahi kumtilia maanani, kwaghafla, anakuwa sehemu muhimu ya Mahusiano, hayayote sio bahati mbaya ya maisha lakini yanakusudiwa kutokea katika maisha yako ili kukukuza na kukusaidia kufikia kusudi la maisha.
Nilijikuta nasafiri kwenye maisha yangu ya zamani na kujaribu kuwakumbuka wale watu wote maishani mwangu ambao wakati fulani walikuwa muhimu sana, walicheza jukumu muhimu, walinifundisha njia-za-maisha, walinigusa wengine hata kuniumiza - lakini baadaye nilielewa kuwa yote yalikuwa kwa faida yangu.
Baadhi yao huwa muhimu kwa wengine, ni kana kwamba YULE aliye juu yetu aliwaondoa kwa vile jukumu lao lilikuwa limekwisha kuwatosheleza katika mchezo wa kucheza wa maisha wa mtu mwingine .Niliwakumbuka watu wote waliowahi kunihudumia,sikuweza kukumbuka hata thumni.
Wengi Wamekuja kama taanzuri za barabarani ili kuangaza njia yako na kufanya safari yako iwe rahisi Wakati mwingine, inastaajabisha jinsi mtu anayefanya haya yote; anaweka watu sahihi katika wakati sahihi , kisha huwachukua kwa wakati unaofaa na kuweka wengine katika nafasi ya mtu mwingine Je! Inawezekenaje hivyo?
Ni kama mwonekano wako, mali na nafasi uliyonayo kazini au katika sehemu yeyote ile, hata mamlaka na madaraka uliyopewa - hupaswi kujivunia, mahusiano yako pia - ni ya kigeugeu kama njia za kuhama za jangwa, zikitoka sehemu moja hadi nyingine.
Kwahivyo wakati mwingine unapopoteza au kupata uhusiano, usihesabu tu maisha ya uhusiano huo, lakini ni maisha mangapi uliyoyagusa kwa ajili ya uhusiano huo, na kumbuka wanapoendelea na kuguswa kwako inamaanisha walikamilisha sehemu ya fumbo la maisha yako na kusonga mbele ili kutatua yajayo.
Tulipata Wageni kutoka Kigoma ambao walikuja Mwanza, Baba wa miaka 55 na binti yake Kaisiki wa miaka 20 ,walienda katika hospitali ya rufaa ya kanda Bugando kwa ajili ya upasuaji wa tezi dume .
Wakati wanatoka hospitali wakiwa maeneo ya Nata walipata ajali .Baba akiwa mbele ya siti ya gari alipigwa na kioo na kuvuja damu nyingi kwenye paji la uso.Katika butwaa binti yake hakujua nini afanye.Alitoa khanga iliyokuwa kwenye mkebe kumpatia babaye azuie damu kutoka.Wengine wakiwa wanarekodi kupitia simu zao yeye akawabize kutafuta usafiri ilhali ni mgeni hakufanikiwa.Hakuna aliyeweza kuwasaidia kwa haraka wengi waliendelea na maisha yao.
Punde tu akatokea malaika,Mamantilie aliyekuwa anaenda kuuza chakula akaacha chakula na kumsaidia binti kutafuta usafiri na kumrudisha baba hospitali. Hakuwaacha pekee alikaa nao muda wote wa matibabu,akampigia meneja wake, kuomba ruhusa na kuendelea kuuguza.Huyu Dada :aliratibu vizuri mahusiano ya wageni” . uhalisia wa maisha ni “,wakati unapohitaji ushauri, kila mtu yuko tayari kukusaidia”, “lakini unapohitaji msaada, kila mtu yuko tayari kukushauri”. Mamantilie angeweza kushauri na kuondoka lakini alisaidia wakati muafaka. maisha yanayohitaji msaada, watu wengi hukusaidia pale inapowafaa, lakini ni wachache sana wanaokusaidia pale inapokufaa au unapohitaji.
Kuna watu kama mamantilie ambao wanadhani wanaishi maisha mara moja tu, kwa hiyo, ikiwa kuna wema wowote unaweza kuonyesha, fanya sasa, kwa maana huwezi kujua ni muda gani utakuwa umechelewa. HUSIKA; fahamu huwezi jua Mungu anapokupa nafasi ya malaika.ambaye anasema malaika hawapo, wanaishi lakini wakati mwingine hawana mbawa.

Upvote
5