Maisha ni ya ajabu sana, Timu kubwa inajiandaa kucheza fainali ya kombe la shirikisho Afrika, wengine wako bunju wanajiandaa kupambana na Ruvu🤣🤣

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Ukipanda bangi siku zote usitegemee kuvuna Mahindi na ndivyo ilivyo kwenye maisha, ukichezea maisha ya ujana usitegemee kufanikiwa uzeeni.

Kwenye mpira pia iko ivyo, Simba wamekuwa wakiishia robo fainali ya michuano ya kimataifa kwa misimu 4 na wamekuwa wakitamba ya kuwa ni mafanikio makubwa kwao, lakini leo hii icho kichaka kimefyekwa na Timu ya wananchi uku ikijiandaa kuweka rekodi nyingine ya kibabe kwa kucheza fainali ya kombe la shirikisho barani Africa.

Wakati ayo yakiendelea wenzao sasa hivi wako bunju wanajiandaa kucheza na ruvu shooting kukamilisha ratiba ya ligi kuu ambayo awana chao tena, wakiwa wametoka patupu bila kombe ata la kunywea kimpumu.

Na ndiyo maisha ayo ya mpira matunda ya usajili ndiyo yanalipa kwa sasa, wengine walisajili kina sawadogo lakini wengine wakasajili kina mayele na tofauti inaonekana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…