Maisha ni zawadi tuishi kwa upendo na kuhurumiana

General Akudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2017
Posts
560
Reaction score
827
Sisi binadamu ni viumbe dhaifu na wasahaulifu, na kuna maamuzi mabaya uwa tunayachukua kwa hasira na hisia hivyo kupelekea kuumiza wenzetu.

Nipo kwenye group la WhatsApp ambapo hivi karibuni mwenzetu mmoja katangulia mbele za haki. Hata namba yake admins wameshindwa ku-remove sababu ya majonzi na simanzi.

Kupitia tukio hili la simanzi, mmoja wetu alileta ajenda ambayo iliendelea kututoa jasho kidogo.

Wengi wetu umri kuanzia miaka 30's kuendelea, kwamba baada ya miaka 40 ijayo huenda wakabaki memba wachache tu wengine wote tukawa tumetangulia mbele za haki.

Lengo tuishi kwa upendo unaweza shangaa wale wanaolumbana ndiyo watabaki kutufungia group.

Hakika sisi sote marehemu watarajiwa tuishi vizuri, upendo na amani vitawale maisha yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…