Maisha rahisi yapo utotoni, ukubwani kila mtu hula kulingana na urefu wa kamba yake

Maisha rahisi yapo utotoni, ukubwani kila mtu hula kulingana na urefu wa kamba yake

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
MAISHA RAHISI YAPO UTOTONI, UKUBWANI KILA MTU HULA KULINGANA NA UREFU WA KAMBA YAKE.

Ifike muda ukubali kula kulingana na urefu wa kamba yako na ukiona havikutoshi basi pambana kuongeza urefu wa kamba ili ule vya mbali.

Utotoni ndio kuna urahisi kwa sababu kazi yako ni kulishwa tu na wengine hivyo wao ndio walikuwa na jukumu la kuongeza kamba ili wakulishe bila wewe kujua ugumu uliopo kwenye kutafuta.


Sasa upo kwenye zama za KILA MTU KULA KULINGANA NA UREFU WA KAMBA YAKE.

Endapo utatamani ule vya mbali ilihali huna jitihada za kuongeza urefu wa kamba basi utaishia pabaya sana na mwisho wa siku utatolewa mchezoni.

Mambo ni mawili tu URIDHIKE NA UREFU WA KAMBA YAKO AU UONGEZE UREFU WA KAMBA ILI ULE VYA MBALI.

#fikia ndoto zako
 
Vipi ukiridhika na urefu wa kamba iliyopo? Maana hata ukiiongeza urefu bila kuridhika hutapata utulivu
 
Kuna wengine maisha magumu toka utotoni mpaka mauti yanapofika.

Ni kama vile kama ilikatwa kabla hata ya kuja duniani.
 
Back
Top Bottom